LGE2024 Manyoni: Jeshi la Polisi linamshikilia Askari aliyesababisha kifo cha mgombea wa CHADEMA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
#TANZANIA: ASKARI MAGEREZA ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA KUMUUA MGOMBEA WA CHADEMA
Jeshi la Polisi linamshikilia Askari Magereza kwa tuhuma za kusababisha Kifo cha George Juma (41), aliyekuwa Mgombea wa Kitongoji cha Stendi kupitia CHADEMA katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Taarifa ya Polisi imesema marehemu alijeruhiwa na Risasi katika purukushani zilizotokea baada ya Wafuasi wa CHADEMA kuwavamia Wafuasi wa CCM waliokuwa katika Kikao cha Ndani na hivyo Askari Magereza walipigiwa Simu na kufika eneo hilo lakini walishambuliwa kwa Mawe ambapo walipiga Risasi hewani ili kuwazuia wafuasi wa CHADEMA.
Taarifa imeongeza kuwa katika purukushani hizo, Risasi moja ilimpata Marehemu George Juma.
Aidha, Polisi imesema uchunguzi bado unaendelea ili kufanikisha kuwakamata waliosababisha vurugu hizo.
 
Wanachekesha au wanaleta hasira????
 
Inashangaza.

Ina maana hapo Singida ikitokea dharura ya kipolisi ccm wana namba za askari magereza wakuja kukamata watu na kutuliza vurugu?
Ni upuuzi sana! Magereza wanahusika vipi? Wanaacha majukumu Yao ya kudili na wafungwa wanatoka nje kudili na raia? Nchi hii ni ya hovyo sana!
 
Mwenye jibu tafadhari anisaidie ili tujue kwamba askari kuua ni jambo la kawaida na hawabanwi na sheria yeyote!
 
Kazi ya jeshi la magereza ni kushughulika na wafungwa, sio raia. Ilikuwaje huyo mbwa akampiga raia risasi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…