ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 9,091
- 21,087
HuniweziUmekuja na hangover za kule michezoni?
Huku utapewa za uso mpaka ukae sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HuniweziUmekuja na hangover za kule michezoni?
Huku utapewa za uso mpaka ukae sawa
Wanachekesha au wanaleta hasira????#TANZANIA: ASKARI MAGEREZA ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA KUMUUA MGOMBEA WA CHADEMA
Jeshi la Polisi linamshikilia Askari Magereza kwa tuhuma za kusababisha Kifo cha George Juma (41), aliyekuwa Mgombea wa Kitongoji cha Stendi kupitia CHADEMA katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Taarifa ya Polisi imesema marehemu alijeruhiwa na Risasi katika purukushani zilizotokea baada ya Wafuasi wa CHADEMA kuwavamia Wafuasi wa CCM waliokuwa katika Kikao cha Ndani na hivyo Askari Magereza walipigiwa Simu na kufika eneo hilo lakini walishambuliwa kwa Mawe ambapo walipiga Risasi hewani ili kuwazuia wafuasi wa CHADEMA.
Taarifa imeongeza kuwa katika purukushani hizo, Risasi moja ilimpata Marehemu George Juma.
Aidha, Polisi imesema uchunguzi bado unaendelea ili kufanikisha kuwakamata waliosababisha vurugu hizo.
Ni upuuzi sana! Magereza wanahusika vipi? Wanaacha majukumu Yao ya kudili na wafungwa wanatoka nje kudili na raia? Nchi hii ni ya hovyo sana!Inashangaza.
Ina maana hapo Singida ikitokea dharura ya kipolisi ccm wana namba za askari magereza wakuja kukamata watu na kutuliza vurugu?
Kazi ya jeshi la magereza ni kushughulika na wafungwa, sio raia. Ilikuwaje huyo mbwa akampiga raia risasi?TAARIFA KWA UMMAJeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia Askari mmoja wa Jeshi la Magereza kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwananchi mmoja tukio ambalo lilitokea Novemba 26,2024 majira ya saa 5:00 usiku huko katika Kitongoji cha Stendi, kata ya Mkwese Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida.
Chanzo cha tukio hilo ni kwamba katika eneo hilo kuna wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM walikuwa katika nyumba moja wakiwa na kikao chao cha ndani. Wakati kikao hicho kikiendelea walivamiwa na kundi la wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vurugu kubwa kutokea ambapo askari magereza ambao wapo katika gereza ambalo lipo karibu na eneo hilo walipigiwa simu kujulishwa juu ya vurugu hizo ikabidi watoke kwenda kuona hali ilivyo huku wakiwasiliana na polisi, walipofika eneo la tukio walianza kushambuliwa kwa mawe jambo lililowalazimu kupiga risasi hewani kuwatahadharisha na kuwazuia watu waliokuwa wakiwashambulia kwa mawe.
Aidha, Katika purukushani hizo, risasi moja ilimjeruhi George Juma, (41), ambaye alikuwa mgombea wa kitongoji cha Stendi kupitia CHADEMA. Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kufanikisha kuwakamata wale wote waliosababisha vurugu hizo.
Jeshi la Polisi Singida linatoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuendelea na shughuli za upigaji kura kuwachagua viongozi wao kwa amani na utulivu kwani Jeshi la Polisi liko imara katika ulinzi kipindi hiki cha kupiga kura na kutangaza matokeo kwa viongozi watakaochaguliwa.
Pia Jeshi la Polisi Singida linatoa onyo kwa mtu yeyote atakayevuruga zoezi la uchaguzi kwani halitasita kumchukulia hatua za kisheria.
Imetolewa na Amon Daudi Kakwale - SACP
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.
Kuhusu kifo cha kada wa CHADEMA, soma LGE2024 - TANZIA - Manyoni: George Juma Mohamed, Mgombea wa CHADEMA auawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia tar 27, 11, 2024