Hii dhana inatesa watu wengi sana hasa hapa nyumbani Tz.
Katika mtiririko wa mahitaji ya muhimu kwa binadamu nikiyataja kwa preference ardhi/nyumba/malazi ni ya mwisho ie
1. Chakula
2. Mavazi
3. Malazi/nyumba/ardhi.
Walio wengi wenye ardhi/nyumba hawawezi kumudu mlo bora wa kila siku kwa uhakika, na sababu kubwa wameanza kukidhi haya mahitaji kinyume ie 3-2-1 ama 3-1-2 au 2-3-1 nk nk.
Ukienda vijijini ardhi hata haina maana halisi ya utajiri inapatikana almost for free na hata thamani yake kwa maana ya asset ni ndogo sana,hivyo haimaanishi ni mafanikio kuwa nayo.
Kwa kijijini mfano ni rahisi kumiliki ardhi kuliko kumudu mahitaji ya kila siku ya chakula. Kijijini pia hawakopeshani kwa dhamana ya ardhi sababu ardhi kwao almost haina real value.