Nimemkumbuka yule mwalimu alomwambia mwanafunzi "Baba yako aliuza ng'ombe wengi ili asomeshe ng'ombe mmoja?"
Ww nawe kama una hela unanunua vyote vp bana!Unamaanisha nisile, nisivae vizuri niwe nadhifu nisitibiwe nikiugua ili ninunue ardhi?[emoji13][emoji13]
Kama ni ardhi hapo handeni heka moja ni laki mbili.
Sio ishu sanaaaaa ardhi.
ulichelewa mkuu. Hata mimi nimepata nikiwa 27 nimechelewa.sio kweli, nimepata ardhu nikiwa na miaka 35
Hii dhana inatesa watu wengi sana hasa hapa nyumbani Tz.Ili mtanzania aendelee pamoja na mengine anahitaji kipande cha ardhi. Bila kujali ni 1*1 au hekari 1000. Haiwezeksni Mungu akuumbie dunia umiliki lakini wewe huna. Leo Mungu akisema kila mmoja asimame kwake ukabaki unatangatanga atakuchapa bakora kwa uovu wa kutomiliki ardhi aliyokupa.
Wakuu tumiliki ardhi. Una uwezekano wa kufa masikini ikiwa katika umri wa 25 huna ardhi au huna mpango mkakati wa kumiliki ardhi.
🤣🤣qummer
Sasahuoni kama unaniunga mkono hoja yangu.Hii dhana inatesa watu wengi sana hasa hapa nyumbani Tz.
Katika mtiririko wa mahitaji ya muhimu kwa binadamu nikiyataja kwa preference ardhi/nyumba/malazi ni ya mwisho ie
1. Chakula
2. Mavazi
3. Malazi/nyumba/ardhi.
Walio wengi wenye ardhi/nyumba hawawezi kumudu mlo bora wa kila siku kwa uhakika, na sababu kubwa wameanza kukidhi haya mahitaji kinyume ie 3-2-1 ama 3-1-2 au 2-3-1 nk nk.
Ukienda vijijini ardhi hata haina maana halisi ya utajiri inapatikana almost for free na hata thamani yake kwa maana ya asset ni ndogo sana,hivyo haimaanishi ni mafanikio kuwa nayo.
Kwa kijijini mfano ni rahisi kumiliki ardhi kuliko kumudu mahitaji ya kila siku ya chakula. Kijijini pia hawakopeshani kwa dhamana ya ardhi sababu ardhi kwao almost haina real value.
umeandika ujinga mkuu.vijana tujaribu kutembea sehemu mbali mbali tuone wenzetu navyo wanavyoishi...kuna elimu kubwa sana kwenye kusafiri kuliko hata io gedree ya DUCE....apa na wew unajiita msomi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na wale wenye forty-five na wanaishi kwao na hawana hata kakipande ka ardhi wanaruhusiwa ku-comment hapa..???Wakuu tumiliki ardhi. Una uwezekano wa kufa masikini ikiwa katika umri wa 25 huna ardhi au huna mpango mkakati wa kumiliki ardhi.
"Nchi za kimasikini"[emoji23][emoji23][emoji23]Hivi unadhan kijana wa kiarabu wa 24-30 priority yake ni ardhi??au kijana wa Denmark awaze ardhi ya 10m??ebu kua serious kidogo mkuu,nkienda apo Kisarawe napata kiwanja cha 100k-300k kikubwa tu!!umeandika ujinga mkuu.
inaonekana ni mzoefu wa kutembelea nchi masikini ambazo hazina ardhi free kama bongoland
Mawazo ya kizamani hayo. Cha muhimu ni pesa benki. Cash is king. Ukiwa na pesa utanunua chochote utakacho wakati wowote. Ardhi hainunui chochote wakati wowote.
Kama pesa ndio kitu pekee ulichonacho, wewe ni maskini tu.... hata ardhi ni mali ya serikali.
hao wasubiri kugombania urithi.Na wale wenye forty-five na wanaishi kwao na hawana hata kakipande ka ardhi wanaruhusiwa ku-comment hapa..???
kweliSio kweli Ila kizazi Cha Sasa ndio Kuna pupa za kupata Mali kwa muda mfupi na umri mdogo. Wanapenda kujadili mafanikio ya wenzao hapo ndio shida.
Sisi tulifanikiwa kuwa na ardhi tukiwa na miaka 40+.
Miaka 25 Bado ni umri wa kutafuta na sio kumiliki...