Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mama Samia nakusalimia kwa jina la JMT mama kipindi utakapokutana na viongozi wa vyama vya siasa usisahau kuwaambia wakongwe wang'atuke mama haileti picha mbaya kung'ang'ania Taasisi za umma miaka karibia 20 na wengine 26 kwa mfano huyu wa Chadema amekifanya Chama kama mali ya familia au kampuni yake binafsi anajiona mjuaji mama Peleka sheria bungeni itakayoyaondoa haya madikteta fanya hvy mama Sasha tunajua wewe ni mpenda demokrssia
 
Wewe unamtafuta malaika?
Wa nini?
Utampata wapi dunia hii?

Kiongozi yeyote hawezi kukosa lawama, hata angefanya mazuri kiasi gani.

Tunataka kiongozi anayejali maslahi ya Tanzania na waTanzania wote, hata hao ambao hawashibi wakishaiba mali zetu.

Tunataka kiongozi asiyevumilia kabisa uchafu wa ufisadi, rushwa, ubadhirifu na matakataka yote. Hao ambao ni sugu na hawasikii kitu awashughulikie kwa sheria zilizopo; kama hazitoshi, awape Bunge watunge za kuwakomesha wanaohujumu nchi yao, ikilazimu hata wanyongwe kama ndiyo njia ya kuwatia akili.

Tunataka kiongozi anayewaunganisha waTanzania, kama taifa moja la watu wanaotambua thamani ya uraia wao na kuuonea fahari.

Kiongozi asionee watu asiowapenda na kuwafanya maadui, kwa vile hawakubaliani naye.

Kiongozi ajue, uongozi wake ni kuwatumikia waTanzania, na siyo kuwafanya wawe mateka wake wa kumsifia hata anapotenda yasiyostahili.

Tunataka kiongozi ambaye anao uwezo wa ushawishi na kuheshimiwa na viongozi wenzake wa mataifa mbalimbali. Anayeweza kuitetea Tanzania bila ya kujionyesha yeye ni bora kuliko wengine

Na zaidi ya yote, tunataka kiongozi atakayewafanya waTanzania kuwa na uthubutu wa kusema wanaweza kufanya mema kwa nchi yao. Kwamba wanaweza kujiletea maendeleo wao wenyewe, na siyo kutegemea watu wengine watoe misaada kwao.
Watu wanaolinda maslahi ya nchi yao, wakichukizwa na vitendo vya wachache kunufaiki na utajiri wa nchi huku wengi wao wakisononeka na kughubikwa na umaskini.

Kiongozi ahimize kila mwananchi wake anatimiza wajibu wake wa kujiletea maisha bora na kuiendeleza Tanzania kiujumla

Nina hakika kiongozi mwenye sifa hizo zote hayupo, lakini anayejitahidi katika mengi ya hayo atafaa sana kwa taifa hili sasa na kwenda mbele.

Je mama anazo kiasi gani ya sifa hizi? SIJUI! Lakini nasubili nione anaweza nini.
 
Mbona Jiwe hakuwa na sifa hata moja kati ya hizi ulizotaja ? Yeye alikuwa Barbarian .
 
Reactions: BAK
Wewe kwako democrasia ni kuondolewa hao, kwani hata walioporwa ushindi na hata fomu uliona ni democrasia
 
Wewe utakuwa mgogo au mnyiramba maana CCM imewapa ufukara wa kutosha mpaka akili hamnaga tena.
 
Ukifanya hivyo mama wapenda demokrasia kote duniani watafurahi sana,maana hao wanaofanyiwa udikteta huu ni watanzania ambao kiuhalisia ni watoto wako,maana wewe ndo mama wa Watanzania wote.
Nakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mimi kama mwanaChadema makini naunga mkono.
 

Mwambie kwanza aondoe udikteta CCM:

**Mgombea uenyekiti ccm huwa hapingwi.

**Kuna wabunge ccm wamekaa majimboni maisha yao yote,wengine over 20 yrs!

#MATAGA bwana#!.
 
Nyiye Mataga kweli propaganda zenu ni za lkitoto sana!

Wewe amekufanya nini Mbowe?

Hivi hujawaona akina Mrema na Cheyo, ambao wamevifanya vyama vyao kuwa "their personal properties" ila wewe unalia na Mbowe tu!
 
una elimu gani?
 
Kila anapohutubia anazungumzia watu. Maslahi ya wafanyakazi, malipo ya wakandarasi, manyanyaso ya walipa kodi, kubambikiwa kesi, mafaili ya kesi yasiyokwisha upelelezi, punguzo la vifungo 5000 haijapata kutokea, uhuru wa kuongea (vpn kufunguliwa), vitendea kazi kwa watumishi.
Kuhusu demokrasia walao vyama vimeingia gereji kutengeneza vyama vyao.
 
Kuzungumza ni kitu kimoja na kutenda ni kitu kingine. Japo ''kuzungumza'' ni dalili nzuri lakini maisha yamenifunza niamini kuwa siyo kila dalili inatoa matokeo husika. Watanzania ni wepesi wa kudanganywa kwa sababu wanaamini vitu kwa haraka bila kutafakari na kujipa muda. Uzoefu umenifunza kuwa kila rais mpya anayeingia huingia na hamasa mpya lakini baada ya muda kila kitu huyeyuka. Simhukumu mama Samia lakini natoa tahadhari kuwa tuwe wavumilivu na wachunguzi bila kutoa hitimisho kwa haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…