Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Binafsi nafurahia sana utawala wa Rais wetu mpendwa SAMIA suluhu hasani, humuoni sana mitaani, waziri mkuu anafanya kwa niaba ya Rais

Hatembei na maburungutu ya hela na kugawa hovyo kupitia mlango wa juu wa gari..
Uongozi ni mfano, ukikaa ofisini tu kupitia mafile hata wa chini yako watafanya vivyo hivyo, na kinyume chake pia. Rais kutoka mtaani na kukagua kazi haimaanishi Waziri nae kazuiwa kufanya hivyo. Kila mmoja anajua mipaka yake..
 
Mama SSH kama uchaguzi ukifanyika kura zooote za Chadema zinakwenda Ccm.

Sisi makamanda tunakukubali sana maana wewe sio Dikteta, wewe sio mpora uchaguzi wewe ni mpore sana.

Kwa hiyo ili ukonge mioyo yetu tusaidie ufanye mzunguko wa pesa uwe mkubwa ili tuanze matanuzi.

Sisi makamanda tunapenda bata kwa kwenda mbele. Bila kukosa mikonyagi na nyama choma.
 
Habari wanabodi..!
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu .Jana kwenye mkutano wa viongozi wa CCM na waandishi wa habari moja ya swali lililoulizwa na mwandishi wa habari ni kwamba,je kama CCM wapo pamoja
Hakuna hofu sana hata kama kuna ma pro JPM bado kwasababu katiba ya Jamhuri imempa nguvu nyingi sana Rais na ile ya CCM imempa nguvu mno Mwenyekiti wao. Bahati nzuri Rais ndiye Mwenyekiti wa ccm pia.

Ni rahisi sana kulisambaratisha kundi lolote lile la kisiasa ndani ya nchi kwa kutumia nguvu za Rais na nguvu za Mwenyekiti.

Kundi LA JPM moyoni ni kundi LA watu ambao walikuwa wananufaika na miradi ambayo ingekamilishwa na JPM kama angekuwa hai. Kundi hili wengi wao wako kanda ya kati na kanda ya ziwa. Hawa ni watu ambao walikuwa wanufaika wa moja kwa moja na alichokuwa anakifanya JPM kwenye maeneo, wilaya, mikoa au kanda yao.
 
1. Futa mwenge wa uhuru kwa mwaka 2021. Huwezi kusema unapambana na corona wakati huo unaruhusu mbio za mwenge. Kwa kawaida wakati wa mbio za mwenge kuna kuwa na mikusanyiko mikubwa inayoweza kuchochea maambukizi ya corona.

2. Piga marufuku tabia inayoendelea kwa sasa ya kuwachangisha watumishi fedha kwa ajili ya mbio za mwenge. Kumbukua watumishi hao hawajaongezewa mishahara kwa miaka 6,hivyo siyo sawa kabisa kuwaomba michango kuchangia mbio za mwenge.

Na hata kama wangekuwa wameongezewa mishahara bado siyo ustaarabu kuchangisha fedha toka kwa watumishi kwa ajili ya mwenge.

Ni hayo kwa leo.
 
Kamati haikuona umuhimu wakuzuia mikusanyiko?
Hili jambo in aibu kuruhusu mikusanyiko wakati kuna UVIKO no 3 tena Kali sana.
 
Mama naye sometimes anademka!

Unawavalisha watu barakoa na kujifanya kuunda tume ya wataalamu wakushauri cha kufanya kwenye korona halafu hapohapo unaruhusu Mwenge wa uhuru utakaokusanya mamilioni ya watu?

Mimi ninaye ndugu yangu anayeumwa Korona kwa sasa, Hii maana yake ni kuwa wimbi la tatu la huu ugonjwa huenda liko in the making, Kwa nini kipindi hiki unnecessary gatherings kama hizo za Mwenge wa uhuru zisizuiwe?, otherwise haya mabarakoa anayovaa ni usanii!

Samia kwenye ishu ya Korona ni bora akaamua, ama awe baridi au moto, siyo vuguvugu!, Akiwa vuguvugu ataonekana kituko!
 
Mama naye sometimes anademka!

Unawavalisha watu barakoa na kujifanya kuunda tume ya wataalamu wakushauri cha kufanya kwenye korona halafu hapohapo unaruhusu Mwenge wa uhuru utakaokusanya mamilioni ya watu?...
Huyo ndugu yako hajafa tu na hiyo corona? Kwa sababu toka mwaka jana unamtangaza kila mara!! Nasikia umepata tenda ya chanjo kama wakala ni kweli mkuu??
 
Nyie moderator msiunganishe huu uzi.

1. Futa mwenge wa uhuru kwa mwaka 2021. Huwezi kusema unapambana na corona wakati huo unaruhusu mbio za mwenge. Kwa kawaida wakati wa mbio za mwenge kuna kuwa na mikusanyiko mikubwa inayoweza kuchochea maambukizi ya corona...
Mwendazake alistopisha mbio za Mwenge kisa Covid 19 japo hakuipa kipaumbele hapo baadae hiyo UVIKO, Ila Mama kaipa kapaumbele sana UVIKO ila chaajabu ameruhusu mbio za Mwenge ziendelee.

Sijui
 
Mwendazake alistopisha mbio za Mwenge kisa Covid 19 japo hakuipa kipaumbele hapo baadae hiyo UVIKO, Ila Mama kaipa kapaumbele sana UVIKO ila chaajabu ameruhusu mbio za Mwenge ziendelee.
Sijui
Mama atakuwa katonywa. Huo mwenge unamambo yake. Na haujawahi kutokimbizwa, JPM yeye akaamua kustopisha. Kila kitu kina miiko yake.
Tambiko la toka uhuru. Mhhh!
 
Back
Top Bottom