Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Sina taarifa kuhusu mikutano hiyo ya Chadema, point yangu ni kufuta mikusanyo aina yoyote ile.

ni vema ungefanya upekuzi wa taarifa vizuri kwanza, so that you can present something clean
 
Corona haipo!! Tumia sababu nyingine kjfuta mwenge. Hak wanaovaa barakoa ni kimkakati zaidi ili kuwafurahisha mabeberu. Na mara nyingi huvaliwa muda mfupi kabla ya kamera ili kuwafurahisha wazee!!
 
Wanajamvi nawasalimu.

Ninaambiwa wakati mwingine ukimpendekeza mtu kwa Rais ateuliwe kumsaidia kazi za siasa ni kwamba unamharibia kwa maana kwamba umemfundisha kazi (priempt).

Hata hivyo kutokana na utawala wa Mwendazake hata hiyo vetting haikufanyika kwa haki. Hivyo sioni makosa kutumia platform hii kutoa maoni yangu.

Mhe Raia, ndani ya CCM kuna vijana wengi weledi na makini hasa kwa kazi za chama. Orodha yao ni ndefu lakini leo nimtaje mmoja tu, BOLLEN NGETTI.

Kipindi chote mimi nilijua yuko jela kutokana na kwamba alichukiwa sana na JPM kutokana na uhusiano wake na JK, Kinana, Membe nakadhalika.

Mara ya mwisho nilimsikia kupitia gazeti fulani (nimelisahau). Ni miongoni mwa waliyofanya kazi kubwa ya kumwingiza JPM madarakani kupitia kalamu na propaganda yake. Ni kiboko ya Upinzani kwa hoja. Ni muumini hasa wa demokrasia.

Rais JPM alimnyanyasa na kumpoteza kisiasa. Ninashangaa kumuona kaibuka mitandaoni kukipigia debe CCM yake iliyomtesa. Kumbuka 2017 aliposwekwa ndani kwa kukosoa Serikali, mawakili wa Chadema wakiongozwa na Tundu Lissu na Peter Kibatala ndio walimtetea bure lakini nia ilikuwa ni kumteka aje Chadema. Hakufanya hivyo, aling'ang'ania CCM hadi leo. Mtumie chamani si Serikalini. Ama kweli sikio la kufa! Ova
#FreedomIsBack
 
Unamjua Bollen ww? Acha ujinga, acha kabisa, CCM inajua mtu hadi kiini chake na mwenyekiti wetu mpya, usimpangie au kumpendekeza nani wa kumteua
 
Hivi corona ipo dar tu? Mbona huku hata ma hospitalin sisikii hata ka umbea kama zamani?

Kwani yeye remot control anasemaje?
 
Mama naye sometimes anademka!

Unawavalisha watu barakoa na kujifanya kuunda tume ya wataalamu wakushauri cha kufanya kwenye korona halafu hapohapo unaruhusu Mwenge wa uhuru utakaokusanya mamilioni ya watu?...
Mwenge ndio sehemu ya upigaji isiyohojiwa... katika mbio hizo mambo ya kishetani hufanywa... ulipaswa kufutwa kabisa...
Walioshauri mwenge kukimbizwa wakati huu wana lao jambo
 
Ngoja ije ikutembelee hapo Namtumbo ndiyo utajua corona ipo.
Sikatai ila najiuliza, kwa nini awali taarifa tulizipata hata kutoka mahospitalini mbona sasa hivi hakuna hata uvumi? January , feb March, taarifa tulizipata kutoka kwa watu baki, watumishi etc kwa nini sasa hivi kimya na unajua mbongo huwezi mzuia kusema kinachoendelea.

Huu ugonjwa upo ila niwakutengeneza.
 
Mama naye sometimes anademka!

Unawavalisha watu barakoa na kujifanya kuunda tume ya wataalamu wakushauri cha kufanya kwenye korona halafu hapohapo unaruhusu Mwenge wa uhuru utakaokusanya mamilioni ya watu?

Mimi ninaye ndugu yangu anayeumwa Korona kwa sasa, Hii maana yake ni kuwa wimbi la tatu la huu ugonjwa huenda liko in the making, Kwa nini kipindi hiki unnecessary gatherings kama hizo za Mwenge wa uhuru zisizuiwe?, otherwise haya mabarakoa anayovaa ni usanii!

Samia kwenye ishu ya Korona ni bora akaamua, ama awe baridi au moto, siyo vuguvugu!, Akiwa vuguvugu ataonekana kituko!
Mama anafanya hivi ili kuyahadaa mabeberu kuwa na yeye anacheza ngoma yao
 
Sikatai ila najiuliza, kwa nini awali taarifa tulizipata hata kutoka mahospitalini mbona sasa hivi hakuna hata uvumi? January , feb March, taarifa tulizipata kutoka kwa watu baki, watumishi etc kwa nini sasa hivi kimya na unajua mbongo huwezi mzuia kusema kinachoendelea.

Huu ugonjwa upo ila niwakutengeneza.
Cha muhimu tuchukue tahadhari.
 
Nyie moderator msiunganishe huu uzi.

1. Futa mwenge wa uhuru kwa mwaka 2021. Huwezi kusema unapambana na corona wakati huo unaruhusu mbio za mwenge. Kwa kawaida wakati wa mbio za mwenge kuna kuwa na mikusanyiko mikubwa inayoweza kuchochea maambukizi ya corona.
2. Piga marufuku tabia inayoendelea kwa sasa ya kuwachangisha watumishi fedha kwa ajili ya mbio za mwenge. Kumbukua watumishi hao hawajaognzewa mishahara kwa miaka 6,hivyo siyo sawa kabisa kuwaomba michango kuchangia mbioa za mwenge. Na hata kama wangekuwa wameongezewa mishahara bado siyo ustaarabu kuchangisha fedha toka kwa watumishi kwa ajili ya mwenge.
Ni hayo kwa leo.
Mimi nilishaga goma kuchangia mwenge kama serikali haina hela waachane nao kwanini tuchangishane mimi siuhitaji waliouleta ndo watoe pesa
 
Imani za kiji

Imani za kijinga.
Nikusaidie kidogo kudharau utamaduni wa kiafrica ni umbumbumbu! Unajua Mila, na desturi vipo ktk jamii yoyote ile. Angalia nchi zote zilizopiga hatua ya maendeleo hazikuwahi kukana mila na desturi zao. Iwe China, India, Ulaya na hata America.
Mtu mweusi anadhani kukana mila au utamaduni wake ndo ataonekana mjanja au wa kisasa. Ulaya wanafanya sana mambo ya Ramli. Mbona hatusemi ni ujinga?
 
Nikusaidie kidogo kudharau utamaduni wa kiafrica ni umbumbumbu! Unajua Mila, na desturi vipo ktk jamii yoyote ile. Angalia nchi zote zilizopiga hatua ya maendeleo hazikuwahi kukana mila na desturi zao. Iwe China, India, Ulaya na hata America.
Mtu mweusi anadhani kukana mila au utamaduni wake ndo ataonekana mjanja au wa kisasa. Ulaya wanafanya sana mambo ya Ramli. Mbona hatusemi ni ujinga?
Narudia kusema, kuabudu mwenge ni ujinga. Mila za mtu mweusi ni za kijinga ndiyo maana hatupigi hatua yoyote kwenye maendeleo.
 
Back
Top Bottom