Wakati napata taarifa kuwa,mrithi wa marehemu John Pombe Magufuli,ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
Binafsi sikuridhika kabisa,mpaka nilipo ota ndoto maalum iliyo nionyesha mfumo mzima wa uongozi katika serikali yake.
Katika mafundisho ya dini na imani yangu,nimefunzwa kuwa,Mwenyezi MUNGU anaweza kuwasiliana na binadamu kwa lengo la kufikisha ujumbe kupitia ndoto.
Kabla sija elezea hiyo ndoto,acha nielezee ulio kuwa wasiwasi wangu kuhusiana na uraisi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Wasiwasi wangu ulikuwa
Je, ataweza kudhibiti watu korofi,wababe,ambao wapo tayari kutumia,mamlaka yao,pesa zao au nafasi zao,ili kuwadhuru wanyonge waliopo Tanzania?
Huu ndio ulikuwa wasiwasi wangu
Maana binafsi nimeona dhuluma nyingi katika ardhi,n.K
Mfano baba yangu mzazi ali dhulumiwa ardhi mara kadhaa nilipo taka twende mbele ya sheria alinikataza,akiniambia acha tu,naacha maana yeye hataki mambo ya kesi.
Sasa nikiwa najihoji sana kuhusu uwezo wa Raisi Samia,usiku huo,nikaota ndoto kumhusu ifuatayo!!!
Nikamwona katika ndoto
Ameketi ikulu katika kiti cha utawala
Ikawepo sauti inayo niambia katika ndoto kuwa,
Huyu ni raisi ambaye hato fumbia macho maovu,
Ni raisi ambaye hato onea watu
Ni raisi atakaye wa adhibu waovu
Ni rais atakaye mpa kila raia haki yake anayo stahili,
Hata pendelea,
Anaye tenda maovu ata adhibiwa kwa maovu
Na anaye tenda mema atalipwa kwa mema
Na kupitia raisi huyu,uchumi wa Watanzania utastawi.
Jamani hiyo ilikuwa ni ndoto yangu ya usiku
Si lazima kila mtu aisomaye ai amini
Ila mimi binafsi baada ya kuiota ndoto hiyo,
Moyo wangu umekuwa na imani kubwa kuhusiana na utawala wa Raisi Samia Suluhu Hassan.