Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hapana hakuwaamini wasaidizi wake ndo Mana alijitahidi kutafuta watu nje ya mfumo akiamini hawatofanya kimazoea sema ego yake ilimtawala ika mpofusha akashindwa kuwaamini hata hao na kudharau professional zao
Tutamkumbuka magufuli kwa uzalendo wake na ubaguzi ulio wazi kwa watanzania
 
Mama Samia tulimwambia kuwa mama unashangiliwa kwa maneno na wewe umekubali?

ulisifiwa kwa uongozi bora upi ambao hata ulikuwa haujashika mafile?

sisi wenyewe tulikuwa tunashangaa ushangiliwaji wa namna ile haukuwa wa maana yoyote lkn haukutudikia na wewe ukaamua kuwavuruga wafuasi wako na serikali yako kwa maneno ya mafumbo yaliyolenga kudhalilisha utawala wenu na Magufuli

ulionyesha madhaifu makubwa sana sasa vijana wa Bavicha wameanza kuibua Kashifa wanaanza kutoa dozi

mm binafsi nitabaki mwana CCM lkn kamwe sitaendelea tena kujitoa kwa namna ambavyo una maneno fulani hivi hayanifurahishi

mm ni mfano wa wanaccm wengi tuliokatishwa tamaa na maneno yako yaliyotukatisha tamaa japo umeugundua ukweli kuwa ulituvuruga lkn itakuchukua muda kutujengea imani tena maaana kwa kweli ulituvuruga tulikuwa na majonzi ulituongezea majonzi

sasa wanakuita majina ya kila aina tulikuambia kuwa shetani hana rafiki hukutusikia
 
Wewe utakuwa unakunywa gongo,mimi naongelea mwenge wewe unaniletea habari za upekuzi.

we si umegusia covid eradication kwa kuepusha mikusanyiko isnt it? then mbna unakwepa maoni?
 
Kukimbiza mwenge ni ibada ya kishetani, sasa ili kumpa Mungu utukufu the moment nikichaguliwa kuwa rais wa nchi ni kupiga marufuku mbio za mwenge from day one. Itabaki tu kumbukumbu kwa waabudu shetani na wapagani wa nchi hii, mark my words...
 
we si umegusia covid eradication kwa kuepusha mikusanyiko isnt it? then mbna unakwepa maoni?
Ndiyo maana nimesema unakunywa gongo, kwani hujui likitolewa tamko kuzuia mwenge kwa sababu ya mikusanyiko,tamko hilo litaenda sambamba na zuio la shughuli nyinginezo zinazohusisha mikusanyiko mikubwa.Sijui huko shuleni mlienda kusomea nini.
 
Kukimbiza mwenge ni ibada ya kishetani, sasa ili kumpa Mungu utukufu the moment nikichaguliwa kuwa rais wa nchi ni kupiga marufuku mbio za mwenge from day one. Itabaki tu kumbukumbu kwa waabudu shetani na wapagani wa nchi hii, mark my words...
Kiufupi Mwenge hauna faida yoyote.
 
Akili ya Kawaida kabisa ingeweza kung'amua walioenda kuhudhuria msiba wa Magufuli, hawakuwa kwenye kitisho chochote cha kuuwawa na vyombo vya dola. Lakini waliotakiwa na Lisu kuandamana dhidi ya ushenzi kwenye uchaguzi ule...
Katika haya maisha, ogopa sana watu wanaokusifia mwanzoni mwa safari!
 
Narudia kusema, kuabudu mwenge ni ujinga. Mila za mtu mweusi ni za kijinga ndiyo maana hatupigi hatua yoyote kwenye maendeleo.
Hatupigia hatua kwani watu wengi kama wewe wasio jua kuchangia hoja bali matusi na kujidharau ndo wanafanya tusiendelee. Wakidhani kudharau mila na desturi ni ujanja. China wameendelea kwa tamaduni zao, India vile vile. Taifa lisilo na utamaduni ni mfu.
Hivyo mtu yoyote mwenye kudharau asili yake hatokaa apate maendeleo. Endelea kujidharau!
 
Wakati napata taarifa kuwa,mrithi wa marehemu John Pombe Magufuli,ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,

Binafsi sikuridhika kabisa,mpaka nilipo ota ndoto maalum iliyo nionyesha mfumo mzima wa uongozi katika serikali yake.

Katika mafundisho ya dini na imani yangu,nimefunzwa kuwa,Mwenyezi MUNGU anaweza kuwasiliana na binadamu kwa lengo la kufikisha ujumbe kupitia ndoto.

Kabla sija elezea hiyo ndoto,acha nielezee ulio kuwa wasiwasi wangu kuhusiana na uraisi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Wasiwasi wangu ulikuwa

Je, ataweza kudhibiti watu korofi,wababe,ambao wapo tayari kutumia,mamlaka yao,pesa zao au nafasi zao,ili kuwadhuru wanyonge waliopo Tanzania?

Huu ndio ulikuwa wasiwasi wangu

Maana binafsi nimeona dhuluma nyingi katika ardhi,n.K

Mfano baba yangu mzazi ali dhulumiwa ardhi mara kadhaa nilipo taka twende mbele ya sheria alinikataza,akiniambia acha tu,naacha maana yeye hataki mambo ya kesi.

Sasa nikiwa najihoji sana kuhusu uwezo wa Raisi Samia,usiku huo,nikaota ndoto kumhusu ifuatayo!!!

Nikamwona katika ndoto

Ameketi ikulu katika kiti cha utawala

Ikawepo sauti inayo niambia katika ndoto kuwa,

Huyu ni raisi ambaye hato fumbia macho maovu,

Ni raisi ambaye hato onea watu

Ni raisi atakaye wa adhibu waovu

Ni rais atakaye mpa kila raia haki yake anayo stahili,

Hata pendelea,

Anaye tenda maovu ata adhibiwa kwa maovu

Na anaye tenda mema atalipwa kwa mema

Na kupitia raisi huyu,uchumi wa Watanzania utastawi.

Jamani hiyo ilikuwa ni ndoto yangu ya usiku

Si lazima kila mtu aisomaye ai amini

Ila mimi binafsi baada ya kuiota ndoto hiyo,

Moyo wangu umekuwa na imani kubwa kuhusiana na utawala wa Raisi Samia Suluhu Hassan.
 
Asante mwanarakati huru wa raisi[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mkuu hiyo ndoto si yako peke yako tu na mi nimo humo tuishi wote humo
 
Taifa kuwa na tamaduni siyo kosa,tatizo ni kuenzi tamaduni za kijinga. Yaani wewe unaona mbio za mwenge ndiyo utamaduni wa kuuenzi.Alafu hao wazungu,wachina unaowatolea mfano ya kwamba wanaenzi tamaduni zao,huwezi kuta wanaenzi vitu vya kipuuzi.Mzungu,mchina siku zote wanaenzi sayansi,na ndicho kilicholeta mapinduzi kwenye mataifa yao.
 
Upo sahihi mtoa mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…