SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Wajane wa dhalim mwendazake bado mnateseka tu?Mama Samia amejipambanua wazi wazi hataki vya dhulma na yeye anafuata line to line maoni ya wafuasi wake wa Twitter na Instagram na Facebook kwamba uchaguzi wa 2020 uliporwa kwa mjibu wa wafuasi wake
Mama Samia ili usiendelee kung'ang'ania vya dhulma tunaomba uvunje bunge tuingie kwenye uchaguzi ili usiongoze nchi kwa dhulma la sivyo utakuwa na wewe unaongea na kufanya usilolijua
.Uchaguzi ulikuwa mzuri na wa haki kuliko chaguzi zote zilizowahi kufanyika. Sera kuu ya CCM ilikuwa ni kumalizia utekelezaji wa yale mazuri yalioanzishwa na serikali ya awamu ya tano, huku kwa upande wa upinzani sera zao zilikuwa ni kuruhusu ushoga nchini, kuruhusu uuzaji wa madawa ya kulevya kiholela mitaani nk. Kwahiyo wananchi walipima sera za wagombea na kuamua kuipa CCM ushindi wa tsunami,huku wapinzani wakiongozwa na viongozi wao wakiangukia pua katika majimbo yao.
Sawa tumia hii kama panado ya kutuliza maumivu, lakini tatizo lako lipo pale pale, maumivu yako hayaishi leo wala kesho! Bye the way, unakumbuka ile video yako ya kijinga ulikuwa Una-dance unasema “Magu hoyee, Taifa stars oyee!”? Wewe ni bure kabisa!
Wananchi walimuonesha Mbowe na Mrema wake kwamba siasa zao za ulaghai na demokrasia yao wa uongo uongo si lolote si chochote mbele yao. Kwahiyo maamuzi ikawa ni kumchinjilia mbali Mrema, na kumkabizi ubunge mwana CCM. Haiwezekani mwenyekiti anaepigania demokrasia nchini atoke huko alipotoka aje awachagulie wananchi mtu wasiemtaka kwenye jimbo lao awaongoze, kukubali kwao ingekuwa ni zaidi ya unyumbu aisee.Dr Charles Kimei Naye aliangukia pia, Leo ni mbunge. Kweli watakao uona ufalme wa mbinguni ni wachache sana.
Unao uwezo wa kulipia gharama zote za kuandaa uchaguzi mpya?,
Magufuli ameshaondoka na katiba unafanya kazi Ndio maana pengo lilizibwa upesi sana.
Na huyu mama anakitendea haki cheo kwani ni mzoefu wa siasa na utendaji. Anavutia wawekezaji kwa kutanguliza haiba ya kiungwana ya mtu anayeshaurika na kuingilika Kimawazo na kimtazamo.
Hayati alishindwa kupanda ndege na kwenda Ulaya na nje ya Afrika huyu mama atakwenda na kuifungua nchi kwa mapana.
Amka mleta uzi tupa blanketi pembeni jinyooshe sali Sala ya asubuhi na uifurahie siku mpya.
Mwenyekiti anaendelea kuitumikia kazi tuliyomtuma kwa uaminifu mkubwa. Najua 2025 atatutengenezea mazingira mengine ya ushindi mkubwa kama alivyofanya katika chaguzi zilizopita hasa hasa uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020. R.I.P kwa aliekuwa mpinzani wa kweli mch Mtikila na Chacha Wangwe. wapinzani wa kweli huwa hawaishi miaka mingi.
Kuna kazi itafanywa Kina hao hao wabungeWaliko mjengoni dodoma wajiandae kuwatumikia wananchi na kuonekana wanafanya kazi majimboni, ule wakati wa kusema nileteeni huyu nileteeni huyu haupo tena. Ule mpango wa kupitia bila kupingwa haupo tena. Jiandaeni kisaikologia mwaka 2025
Mataga kwangu ni msamiati nisioufahamu.Muambie mataga mwenzake, labda atakuelewa aache kuendelea kuweweseka na kuteseka.
Siasa Sio uadui mkuu..Mwenyekiti anaendelea kuitumikia kazi tuliyomtuma kwa uaminifu mkubwa. Najua 2025 atatutengenezea mazingira mengine ya ushindi mkubwa kama alivyofanya katika chaguzi zilizopita hasa hasa uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020. R.I.P kwa aliekuwa mpinzani wa kweli mch Mtikila na Chacha Wangwe. wapinzani wa kweli huwa hawaishi miaka mingi.
View attachment 1830637
View attachment 1830638
View attachment 1830639
ndefu sana sijasoma yote ngoja na Mimi nichangie kidogo, nyinyi wafanyabiashara hamtaki kufuata sheria inavyoelekeza mwezi uliopita nilikwenda kununua vifaa vya ujenzi nilivyoomba risiti nikarudishiwa hela na mzigo ukashushwa kutoka kwenye gari nilikuwa na nanunua simenti hii ni baada ya kukataa risiti iliyokuwa haendani na gharama niliyolipa je ni nani unataka ajenge nchi.Kwa heshima na taadhima, nanatoa pongezi kwa juhudi anazofanya Mheshimiwa rais hasa katika suala zima la weledi na usimamizi wa haki kwa kuimarisha utulivu na maendeleo ya taifa letu.
Pamoja na hatua ambazo ameelekeza zichukulilwe, zikiwemo za kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji, kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi na kujenga mazingira rafiki ya ulipaji kodi kwa walipa kodi, liko jambo moja muhimu la kuangalia zaidi ya TRA kama taasisi nalo ni WAFANYA KAZI WA TRA na si TRA ka
1. Uzembe na uonezi tRA uko matawini wakiongozwa na managers wa matawi.
2. Wanawabambikiza watu kodi ili kujenga mazingira ya rushwa na kuwakomoa walipa kodi wanapowasilisha malalamiko ya kwa uzembe wa matawi yao.
3. Ama kuwaongezea watu kodi zisizo halali imekuwa pia mbinu inayotumiwa katika kufikisha ama kuzidi malengo waliyopewa ili wajenge majina, na huu ni udanganyifu ambao unatengeneza jinai.
4. Wanawatishia watu kama wakienda kulalalmika kokote, wakatiwa hatianik hao wafanyabiashara watafanyiwa figisu hata na wenzao baada ya wao kwa kuwa wao wanamitandao mipana. Kama unataka jaribu uone utakavyoishia jela kwa kubambikizwa kesi za kutakatifisha fedha, kukwepa kodi n.k. Nachelea kutoa mifanyo halisi ya watoa taarifa hii walichoambiwa kwa kuogopa wasije wakalipizwa visasi wakitambuliwa na wahusika kwa matukio yalivyokuwa.
Mwananchi anayedunduliza vijicent vyake ili angalau watoto wapate hata mlo mmoja kwa siku, anajitahidi kwenda katika ofisi za TRA na kuonesha ushirikiano ili apigiwe hesabu zake sahihi za kodi alipe bila kusukumwa, anaishia kfanyiwa mizengwe na kutishiwa akichukua hatua atabambikizwa kesi. Taifa hli linaelekea wapi ?
Raia wanapoishi kwa machozi, siyo baraka kwa Mungu. TRA, wanapashwa kufanya kazi kwa weledi na haki, lakini hawa waliopo waliozowea na tayari wameshaota mizizi ya kunyonga watu hawawezi kubadilika kwa mabadiliko ya sera na maonyo. Hata sera zilizopo, haziwaongozi kufanya uharifu wa kalamu na kuwafunga watu midomo kwamba kusema kutawapelekea wambambikziwe kesi zisizo dhamana. Huu ni unyang'anyi na ujambazi.
Ombi langu kwa TRA,
1) Ingieni mkataba na Independent Consultant, awafanyie online survey kwa kupitia mitandao ya simu, ili walipa kodi wenu walio kwenye database yenu, wawaambie matukio yote kinaga ubaga ya uharifu wanayofanyiwa na Wafanyakazi wenu, kwa majina yao na maeneo yao, na vyeo vyao. (Ieleweke masanduku ya mawazo ya matawini hayafanya kazi na hata unapozingatia mtu ana hofu).
2) Waondoeni hao waharifu kati yenu, ajirini watu wapya kwa kuwa graduates wengi tu wapo mitaani hawana kazi ili kujenga taasisi imara, inayofanya kazi kwa weledi na uadilifu.
BILA KUCHUKUA HATUA HIZI MAHUSUSI, JUHUDI ZE KUBORESHA MAZINGIRA YA KODI NA KUPANUA WIGO NA KUACHA WATENDAJI WAHARIFU WAKITAMALAKI, HAZITAFANYA KAZI KWA KIWNGO KINACHOKUSUDIWA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kweli mkuu.. ila cha kushangaza Lisu alifanya siasa ni uadui kwa kupambana huko Ulaya ili Tanzania tuwekewe vikwazo na kunyimwa misaada kwa sababu zake za kisiasa.Siasa Sio uadui mkuu..
Acha dawa ikuingie tu. Wewe tulia. Kwa papara kama hizi ni dhahiri mmeshikwa pabaya. Mtu makini husoma na kuelewa kabla hajajibu. Vinginevyo endelea kuropoka bila kuelewa somo ujichore vizuri.ndefu sana sijasoma yote ngoja na Mimi nichangie kidogo, nyinyi wafanyabiashara hamtaki kufuata sheria inavyoelekeza mwezi uliopita nilikwenda kununua vifaa vya ujenzi nilivyoomba risiti nikarudishiwa hela na mzigo ukashushwa kutoka kwenye gari nilikuwa na nanunua simenti hii ni baada ya kukataa risiti iliyokuwa haendani na gharama niliyolipa je ni nani unataka ajenge nchi.
Magufuli alisema atapandisha salary siku anatoka madarakani na hapa tuna assume kama angekua mkweli maana alikua ana historia ya kusema uongo.Mkuu, pongezi za nini sasa! Hata magufuli angebaki hai mpaka leo, bado angetupandisha tu. Maana haki ya mtu inacheleweshwa tu! Ila mwisho wa siku ni lazima ipatikane.
By the way, siyo watumishi wote wenye sifa wamepandishwa mwezi huu. Sasa huoni haujatutendea haki sisi watumishi wenzako ambao tumepokea mshahara ule ule wa miaka yote!! Maana umesema watumishi wote tunampongeza!!
July wote itakua tayari,ni makosa ya kibinadamu yaliyotokea tuMkuu, pongezi za nini sasa! Hata magufuli angebaki hai mpaka leo, bado angetupandisha tu. Maana haki ya mtu inacheleweshwa tu! Ila mwisho wa siku ni lazima ipatikane.
By the way, siyo watumishi wote wenye sifa wamepandishwa mwezi huu. Sasa huoni haujatutendea haki sisi watumishi wenzako ambao tumepokea mshahara ule ule wa miaka yote!! Maana umesema watumishi wote tunampongeza!!