Kwa heshima na taadhima, nanatoa pongezi kwa juhudi anazofanya Mheshimiwa rais hasa katika suala zima la weledi na usimamizi wa haki kwa kuimarisha utulivu na maendeleo ya taifa letu.
Pamoja na hatua ambazo ameelekeza zichukulilwe, zikiwemo za kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji, kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi na kujenga mazingira rafiki ya ulipaji kodi kwa walipa kodi, liko jambo moja muhimu la kuangalia zaidi ya TRA kama taasisi nalo ni WAFANYA KAZI WA TRA na si TRA ka
1. Uzembe na uonezi tRA uko matawini wakiongozwa na managers wa matawi.
2. Wanawabambikiza watu kodi ili kujenga mazingira ya rushwa na kuwakomoa walipa kodi wanapowasilisha malalamiko ya kwa uzembe wa matawi yao.
3. Ama kuwaongezea watu kodi zisizo halali imekuwa pia mbinu inayotumiwa katika kufikisha ama kuzidi malengo waliyopewa ili wajenge majina, na huu ni udanganyifu ambao unatengeneza jinai.
4. Wanawatishia watu kama wakienda kulalalmika kokote, wakatiwa hatianik hao wafanyabiashara watafanyiwa figisu hata na wenzao baada ya wao kwa kuwa wao wanamitandao mipana. Kama unataka jaribu uone utakavyoishia jela kwa kubambikizwa kesi za kutakatifisha fedha, kukwepa kodi n.k. Nachelea kutoa mifanyo halisi ya watoa taarifa hii walichoambiwa kwa kuogopa wasije wakalipizwa visasi wakitambuliwa na wahusika kwa matukio yalivyokuwa.
Mwananchi anayedunduliza vijicent vyake ili angalau watoto wapate hata mlo mmoja kwa siku, anajitahidi kwenda katika ofisi za TRA na kuonesha ushirikiano ili apigiwe hesabu zake sahihi za kodi alipe bila kusukumwa, anaishia kfanyiwa mizengwe na kutishiwa akichukua hatua atabambikizwa kesi. Taifa hli linaelekea wapi ?
Raia wanapoishi kwa machozi, siyo baraka kwa Mungu. TRA, wanapashwa kufanya kazi kwa weledi na haki, lakini hawa waliopo waliozowea na tayari wameshaota mizizi ya kunyonga watu hawawezi kubadilika kwa mabadiliko ya sera na maonyo. Hata sera zilizopo, haziwaongozi kufanya uharifu wa kalamu na kuwafunga watu midomo kwamba kusema kutawapelekea wambambikziwe kesi zisizo dhamana. Huu ni unyang'anyi na ujambazi.
Ombi langu kwa TRA,
1) Ingieni mkataba na Independent Consultant, awafanyie online survey kwa kupitia mitandao ya simu, ili walipa kodi wenu walio kwenye database yenu, wawaambie matukio yote kinaga ubaga ya uharifu wanayofanyiwa na Wafanyakazi wenu, kwa majina yao na maeneo yao, na vyeo vyao. (Ieleweke masanduku ya mawazo ya matawini hayafanya kazi na hata unapozingatia mtu ana hofu).
2) Waondoeni hao waharifu kati yenu, ajirini watu wapya kwa kuwa graduates wengi tu wapo mitaani hawana kazi ili kujenga taasisi imara, inayofanya kazi kwa weledi na uadilifu.
BILA KUCHUKUA HATUA HIZI MAHUSUSI, JUHUDI ZE KUBORESHA MAZINGIRA YA KODI NA KUPANUA WIGO NA KUACHA WATENDAJI WAHARIFU WAKITAMALAKI, HAZITAFANYA KAZI KWA KIWNGO KINACHOKUSUDIWA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA