Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mimi Mmawia naendelea kuamini kuwa kesho yetu kama taifa itakuwa bora kuliko leo hii.

Nilisema tangu mwanzo wakati ameenda kumtazama mh Lissu pale Nairobi Hospital.

Nikasema alivyo kwenda kumtembelea mh Lissu pale Ubelgiji na nilikuwa mbishi na kuwapinga wanao mbeza mh Mbowe kisa kaenda ikulu.

Chini ya viongozi thabiti wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA chini ya mwenyekiti Mbowe kwa kushirikiana na mama Samia hakika tunaenda kuandika historia njema ya amani Tanzania.
 

Namba 8 umeongea point, kwingine huko umepuyanga.
 

Umesifia sana. All in All mama samia ni zaidi ya marais wote waliopita. Huyu mama atafanya mazuri hadi mumkubali
 
Toka tupate uhuru Tanzania hatukuwahi pata raisi mwenye maono na mchapakazi kama mama SSH samia suluhu

MUNGU ampe afya njema na ikiwezekana aongezewe muda zaiidi naandika haya nikiwa

Tainan city Taiwan
 
Nianze kwa pongezi,hakika leo nimemwelewa Mh Rais Samia alipokuwa akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo alipo kutana na wadau wa demokrasi.

Niungane nae,suala la vyombo vya habari ameliongelea vizuri sana Kwa maana ya uhusinao wa vyombo vya habari na vyama vya siasa,
Ni nadra sana kukuta Chombo Cha habari kama TBC one kikilipoti habari nzuri dhidi ya chadema,hata Tanzania daima dhidi ya ccm Ili ni kosa.

Siungaji nawe,wara kijiwe Cha wananongwa yaani hao walioitwa kikosi kazi dhidi ya suala la katiba mpya katiba mpya hatuiitaji kwa ajili ya uchaguzi la hasha tunataka katiba mpya kuweseha kuondoa viongozi wa ovyo inapotokea Taifa letu likewapata mathalani mwendazake, sabaya na makonda tungelikuwa na katiba wasingefanya waliyoyafanya.

The same bushit haiwezekani watu wamtusi Raisi wa nchi heti wanasamehewa na aliyetukanwa na baada wanateulliwa Tena kwa usafi gani tunaitaka katiba itakayo ondoa upuuzi huu.

Mh Rais Mimi ni miongoni mwa vijana walio furahi niliposikia unatafuta business partner wa bandari hasa upande wa mifumo,Tena Mimi ningeshauri uiuze tu moja kwa moja tule chetu mapema,kama hatutaki katiba Kwa Nini rasirimali zote tusiziuze tukala chetu mapema kabla ya uchafu au machafuko?

Mh Raisi katiba sio kwa ajili ya kulinda wanasiasa wapate madaraka, elewa hivyo jamani.

Mh Rais ninae mdau anataka tuibabue Tanesco baada ya kuona haifanyi vizur yeye ni kampuni ya solar inataka inunue Tanesco au awe business partner wako fanya fasta nipm hapo fasta upige pesa.

Mwisho kabisa Mimi sifileo ni mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi East Africa nimefanya vizuri sana kiulinzi wa Raia na Mali zao, Uganda na Kenya na Rwanda Sasa naitaji uniuzie jeshi la polisi Mimi ntanunulia na mitambo Yao yote na wanadamu wote ila mkubwa wao,kingai na wengine nitawastafisha haraka nataka Damu changa zipige mzigo hapo.


Niuzie jeshi la polisi nakuhakikishia nitawapigisha kazi jeshi la polisi wapige kazi na ntawaepusha kuacha kukusema wewe Mh Rais unaposema hawafanyi kazi Mimi wakinisema nawawashia moto dadeki na kuwasweka ndani Sina mjadara katika ilo
 
Bange bange bange, umesababisha niwe ndondocha, bange bange bange nitakutaliki tusiwe wote.... × 2 [emoji87]
 
Mchaga akishiba mbege akili inaruka juu

USSR
 
Nchi Sasa hivi inaendelea kwa kasi na katika nyanna zote kijamii, kisiasa na kiuchumi siyo kama.kipindi kilichopita ambapo nchi ilikuwa angalau inapiga hatua kiuchumi tu Mambo mengine ikatelekeza.

Sasa hivi kila mtu ana raha ndani ya nchii hii. Hakuna uonevu tena wa kunyanyasana na watu wasiojulikana ama kutumbuana bila sababu za msingi.

Sasa hivi mihimili yote inajitegemea na iko huru kabisa
 
Ila mbona furaha imezidi kupungua zaidi kwa mujibu wa research iliyofanyika.

Ila pia kuhusu mihimili kuwahuru Wala sio kweli, spika aliondolewa kwa kumpinga raisi
 
Ila mbona furaha imezidi kupungua zaidi kwa mujibu wa research iliyofanyika.

Ila pia kuhusu mihimili kuwahuru Wala sio kweli, spika aliondolewa kwa kumpinga raisi
Zile research Ni za wazungu hazireflect ukweli.
 
USIYOYAJUA JUU YA DARAJA LA TANZANITE - KONGOLE RAIS SAMIA KWA KUKAMILISHA MIRADI!

Na Mwl Udadis,

Daraja limejengwa mita chache kutoka daraja la zamani la Salenda. Lina Urefu wa takribani Mita 1030, Upana wa Mita 20.3 na Urefu wa Barabara Unganishi yenye KM 5.2 zilizojengwa kwa kiwango cha lami. Daraja limekamilika kwa asilimia 100%.

Tofauti na madaraja mengi ya namna hii barani Afrika, Watumiaji hawatalipa tozo yoyote pindi watumiapo daraja hili (TOLL FREE). Pia, Daraja hili lenye uwezo wa kuhimili tani 180 za uzito litaweza kusafirisha watu wapatao 55,000 kwa siku.

Kwa Takwimu zilizopo, Daraja hili litakuwa kati ya madaraja 10 marefu zaidi barani Afrika likiwa nyuma ya Daraja la Wouri kutoka Cameroon lenye urefu wa takribani Mita 1800 likiwa katika nafasi ya nane kwa urefu Afrika.

Gharama za ujenzi zimetolewa kwa ushirika kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Korea. Ujenzi ulioanza rasmi mwaka 2018 umeigharimu serikali ya Tanzania kiasi cha takribani dola za kimarekani milioni 104.5.

Hadi kufikia mwaka 2017, Takwimu zilionyesha watumiaji wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kufikia kiasi cha magari 42,000 kwa siku. Barabara hii ni kati ya Barabara muhimu kiuchumi lakini pia ni kati ya Barabara zenye foleni, hivyo kukamilika wa Tanzanite Bridge ni mafanikio makubwa kiuchumi.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika mwaka 2021, wakazi wa Jiji la DSM wenye kipato cha TZS 90,000 hupoteza hadi kiasi cha 39% ya mapato yao kutokana na gharama zinazosababishwa na foleni. Daraja la Tanzanite ni kati ya mipango mingi madhubuti ya kukabiliana na foleni ndani ya Jiji.

Mwisho nimpongeze Rais Samia Suluhu kwa kutekeleza ahadi ya kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli inatekelezwa. Mh. Rais anazidi kuonyesha umahiri mkubwa katika uongozi wake. Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele tumebarikiwa kuwa na viongozi makini.

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
 
Najua wewe unajua kama sisi tujuavyo, kuwa sifa nyingi sana unazopewa kwa sasa zimepitiliza ukweli halisi na kufanya zionekane kama komedi ya aina fulani hivi.

Mtangulizi wako naye alisifiwa sana kwa nyimbo na mapambio, lakini uliona mwenyewe jinsi ambavyo walimnanga muda mfupi tuu baada ya kufariki (ukiwemo wewe mwenyewe) hadi kufikia kutamkwa kuwa UNAPONYA NCHI.

Mambo ya mwendazake yanajirudia tena sasa kwa kasi zaidi, SIFA ZA HOVYO. Umewahi kutafakari hao wanaoendesha kampeni hii ya sifa wana malengo ya kuifaa nchi au ni agenda zao binafsi za "kushibisha matumbo" yao?

Je, unakumbuka ushauri wa Askofu Dr Shoo kuhusu kukubali umungu mtu? Kwa maoni yangu, hao (ambao naamini ni wanaccm) wanakupoteza na utazoea tabia hiyo kama Hayati Magufuli na pale Wapinzani watakapo Anza mikutano yao na kukosoa utendaji wako utaishia kuchukia na kutumia madaraka hayo vibaya nawe kuishia kuwa kiongozi mbaya.
 
Kwa unyenyekevu kabisa tumieni mwezi mtukufu wa ramadhani au siku ya sikukuu kuwaachia wafungwa ambao wamebakiza siku au miezi michache kumaliza kifungo chao ,pia ukiongezea na kwenye siku ya Xmass ili walioko kifungoni na weshatumikia nusu na robo ya kifungo chao,wapate msamaha na kuwakumbusha kuwa dini zinawakumbuka na kuwataka watende mema watokapo na kufika uraiani.
Ni hilo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…