Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kitu ambacho nakiona ni kuwa sectors binafsi zimeanza kupata pumzi hilo ndo naliona
 
Samia mitano tena
 
Kwa mfumo wa nchi yetu mkuu huwezi kuitanganisha serikali na rais ndo maana wakati wa magu alipiga marufuku ajira na hazikutoka, mbona sasa serikali haikutoa hizo ajira kama ilikuwa inajitegemea bila rais??? Usijitoe ufahamu hizi ajira zina vibali na hivyo vibali maanake haiviwezi kutoka bila bajeti, na bajeti haiwezi kutengwa bila waziri wa fedha kuhusishwa na waziri hawezi kujitengea bajeti bila Rais kujua! Usijitoe ufahamu mkuu
 
Sasa hivi kila kona ni ajira tu

1. MUHAS wamemwaga ajira kibao

2. Elimi wamemwaga ajira kibao

4. TAKUKURU ndo usiseme.

5. Polisi nako ni fire

Asante Mungu kutuletea Samiw

Huyu ndo mtetezi wa wanyonge sada na siyo yule alikuwa anawanyonga wanyonge
 
Reli ya Dodoma hadi Mwanza bado inajengwa?
 
Kwa anavyosifiwa kufanya miujiza, sina shaka. Napendekeza mtukufu, mpendwa, mbeba maono, daktari bingwa, mwanafalsa, gwiji, mweledi, msafi kulhali, mnyenyekevu, mwenye mapenzi makubwa kwa watanzania hata wadudu, msikivu, mwenye akili zisozo za kawaida, mwenye elimu ya juu kuliko hata maprofesa, muumini nk nk Daktari, profesa Samia Suluhu Hassan aruhusiwe kuigeuza Tanzania nchi ya kifalme ili wazawa wake watumie vipawa adimu walivyojaliwa kuendelea kuitawala hata atakapokuwa ametoweka. Je mnasemaje wana bodi?
 
Samia ni kama mama mdogo wangu.

I support you madame.

Go goo.
 
๐—ฅ๐—ฎ๐—ถ๐˜€ ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ป๐—ถ ๐—–๐—ต๐—ฎ๐—บ๐—ฝ๐—ถ๐—ผ๐—ป๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐—จ๐—ฐ๐—ต๐˜‚๐—บ๐—ถ ๐—•๐˜‚๐—ป๐—ถ๐—ณ๐˜‚ (๐˜พ๐™ง๐™š๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ซ๐™š ๐™€๐™˜๐™ค๐™ฃ๐™ค๐™ข๐™ฎ).
๐™ฝ๐šŠ. ๐™ฐ๐š–๐š˜๐š— ๐™ฝ๐š๐šž๐š–๐šŠ .

Zamani za kale na hata sasa dhana ya Uchumi imekuwa ikijikita katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa na huduma ,kwamba chanzo kikuu cha uchumi ni bidhaa au huduma lakini katika ulimwengu wa sasa upo Uchumi Bunifu ( Creative Economy) uchumi ambao Ubunifu/kipaji ndio bidhaa inayouzwa,kuingiza pato na hata ajira kwa vijana wengi .

Uchumi Bunifu( Creative Economy) unahusisha Ubunifu kama bidhaa adhimu ya kutengeneza fursa,mapato na ajira katika Jamii ikihusisha Muziki,Filamu ,Fasihi pamoja na Sanaa nyengine ikiwemo Maonesho ,Uchoraji pamoja na Uchongaji .Aidha Uchumi Bunifu umekuwa ni mhimili muhimu na kutegemewa katika nyakati hizi za Teknolojia ya Habari (TEHAMA) pamoja na Tatizo la Ukosefu wa Ajira ulimwenguni kote ,kwani ni Sekta inayoweza kuhusisha na kutoa ajira kwa watu wengi zaidi.

Uchumi Bunifu unaajiri watu wengi ikiwemo Wasanii, Wapiga picha ,Wachoraji (Graphic Designer) ,Wachongaji ,Wanamitindo wa mavazi ,Madereva ,mameneja n.k .Kazi moja ya Sanaa inatoa ajira kwa watu wengi zaidi na mapato kwa msanii na Taifa kwa ujumla kupitia kodi ,hivyo Taifa lolote linalowekeza na kuinua sekta ya sanaa na Uchumi Bunifu inaandaa kesho njema ya Taifa hilo .

Tanzania tunapaswa kujivunia na kutambua mchango mkubwa wa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika ukuzaji na uendelezaji wa Uchumi Bunifu katika Nchi yetu ambao utaleta maendeleo endelevu ya kiuchumi ,maendeleo ya jamii ,utunzaji wa utamaduni na ujumuishaji wa Jamii(Social Inclusion).

Kwanini Rais.Dkt.Samia Suluhu ni Championi katika Maendeleo ya Uchumi Bunifu Nchini ?, ni kama ifuatavyo kwa uchache ;-

๐”๐ฐ๐ž๐ณ๐ž๐ฌ๐ก๐š๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐Š๐ข๐Ÿ๐ž๐๐ก๐š ( Mikopo).
Fedha ni rasilimali muhimu katika uwekezaji wowote ule na chini ya Uongozi wa Dkt.Samia Suluhu wasanii wamepatiwa mikopo nafuu ili kuendeleza kazi zao na uchumi wao kwani wasanii wengi walikuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo matumizi ya vifaa duni na ukosefu wa mitaji katika kazi zao .

๐Œ๐š๐Ÿ๐ฎ๐ง๐ณ๐จ ๐ง๐š ๐”๐ฐ๐ž๐ณ๐ž๐ฌ๐ก๐š๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐Š๐ข๐ญ๐š๐š๐ฅ๐š๐ฆ๐ฎ .
Chini ya Uongozi wa Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan wasanii wamepata mafunzo ,semina na fursa ya kupata changamoto na kujifunza kutoka kwa wasanii wa Kimataifa katika sehemu mbalimbali Duniani.Mfano Wasanii wa Bongo Movie walipatiwa fursa ya kuenda kujifunza katika moja ya Studio kubwa ya Filamu Nchini Korea .

๐”๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐ณ๐š๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐Œ๐ข๐จ๐ง๐๐จ๐ฆ๐›๐ข๐ง๐ฎ ๐ฒ๐š ๐“๐„๐‡๐€๐Œ๐€ .Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni mdau tegemezi katika Uchumi Bunifu kwani kazi za sanaa kwa kiasi kikubwa zinategemea matumizi ya Vifaa vya Elektonic na Programu Tumizi( Application) na Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka nguvu kubwa katika usimikaji wa TEHAMA katika
Shule za Msingi ,Sekondari na Vyuoni ili kuwapa Wanafunzi na Vijana fursa ya kujifunza na kubobea katika matumizi ya TEHAMA na fani zao za Sanaa.

๐”๐ฅ๐ข๐ฉ๐š๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐Œ๐ข๐ซ๐š๐›๐š๐ก๐š ๐ง๐š ๐‡๐š๐ค๐ข za ๐–๐š๐ฌ๐š๐ง๐ข๐ข.
Ili kuhakikisha kuwa Wabunifu( wasanii) wanakuwa kiuchumi na kukuza sekta ya Ubunifu ,Serikali chini ya Uongozi wa Mhe.Dkt.Samia kupitia Ofisi ya Hatimiliki Tanzania( COSOTA) imelipa Leseni na Mirabaha kwa wasanii kutokana na matumizi kazi za wasanii katika Taasisi mbalimbali za Umma ikiwemo TAA inayohusika na Viwanja vya Ndege ,zote hizi ni udhihirisho wa dhamira ya Mhe.Rais kuona sekta ya Uchumi Bunifu inakua .

๐Œ๐ข๐ค๐ฎ๐ญ๐š๐ง๐จ ,๐Œ๐š๐š๐๐ก๐ข๐ฆ๐ข๐ฌ๐ก๐จ ๐ง๐š ๐Œ๐š๐ญ๐š๐ฆ๐š๐ฌ๐ก๐š ๐ฆ๐›๐š๐ฅ๐ข๐ฆ๐›๐š๐ฅ๐ข .
Pamoja na uwepo wa Mitandao ya Kijamii, Matamasha ni moja ya maeneo ambapo dhamira ya sanaa ya kuelimisha na kuburudisha jamii inafanyika ,Tamasha ni soko kwa Mbunifu pale mchoraji na mchongaji na msanii yeyote atauza bidhaa zake za kiubunifu atapata kipato ,serikali itapata pato na uchumi wa msanii na Taifa utakua .Kupitia mikutano mbalimbali ya Kimataifa iliyofanyika na inayofanyika nayo imekuwa fursa ya soko kwa wasanii kufanya biashara .Pongezi Mhe.Rais kwa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kiwango cha kuridhisha .

1๐™๐™ž๐™ข๐™ค๐™ฉ๐™๐™š๐™ค 5:8 .
" Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini ".
Pongezi nyingi
๐™ˆ๐™๐™š.๐˜ฟ๐™ ๐™ฉ. ๐™Ž๐™–๐™ข๐™ž๐™– ๐™Ž๐™ช๐™ก๐™ช๐™๐™ช ๐™ƒ๐™–๐™จ๐™จ๐™–๐™ฃ ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali na kuwaendeleza Wasanii na Watanzania walioajiriwa katika sekta hii kubwa.Dhamira ni njema,matokea tunayaona ,matumaini ni makubwa zaidi siku za usoni kwa uwezo wa Mungu .


KaziIendelee
MitanoTena .
 

Attachments

  • IMG-20250123-WA0377(1).jpg
    108.3 KB · Views: 1
  • IMG-20250123-WA0376(1).jpg
    96.3 KB · Views: 1
 

Attachments

  • 5938169-3f8437b06df44d0a7c8b8e175f481762.mp4
    23 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ