Amani iwe nawe Mhe. Rais,
Naomba nikushauri yafuatayo kwa mustakabali wa nchi yetu Kiuchumi ili kutengeneza Tanzania imara kiuchumi.
1. Kwa upande wa Baraza la Mawaziri- Wateue Wabunge waliotoka kwenye private sectors na kuziongoza kwa Mafanikio kuwa Mawaziri wa Fedha na Viwanda na Biashara. Ondokana na hawa maprofesa waliokulia vyuoni kwenye hayo maeneo. Hii ni Kwa sababu watu hawa wataweka sera nzuri za fedha, uchumi na Biashara na kuiwezesha Tanzania kupaa kiuchumi.
2. Kwenye mashirika yetu ya kimkakati ( Tanapa, ATCL, Ngorogoro na Mengineo) , tafuta watu safi kutoka private sector( Makampuni na Mabenki) wenye rekodi ya kuendesha taasisi zao kwa faida na mafanikio na uwape haya mashirika. Najua tunao kina Nehemia Mchechu hapa na Charles Singili na wengineo wengi. Hutajutia huu uamuzi Kwa sababu sector hizi zinahitaji kuongozwa na watu wazoevu kwenye biashara ili kupata tija na mafanikio. Inawezekana usisite.
3. Kwenye sector za usimamizi wa Biashara na uchumi mf. BOT, TRA na kwingineko Pia, tafuta wataalamu wenye rekodi ya kufanya sekta binafsi Kwa mafanikio makubwa.
4. Kwa Bandari, tafuta mchumi mahiri kutoka JWTZ na awe seniour Officer, mpe Mamlaka ya Bandari aiongoze. Ila kwenye usaidizi muwekee timu ya wataalamu kutoka private sector wenye rekodi ya mafanikio kwenye biashara ili wamsaidie.
Mwisho hili liko nje ya mada ila nalo naomba lizingatie mama.
Kwenye utumishi wa umma hasa nafasi za RAS, DAS, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi nyeti ikiwemo za ulinzi na usalama zingatia sana seniority kwenye teuzi zako ili kuepuka power struggle. Kuna watu wapo kwenye maofisi na ni ma seniour sana, inapokuja kwenye nafasi wanazotakiwa kuwapa, wape tu, hii itaondoa vita kwenye taasisi zetu kuu za serikali hasa vya madaraka na uadui.
Mwisho hata kwenye wakuu wa mikoa na wilaya tafuta makada kutoka Chama chako au vyama vyenye mlengo tofauti wenye hekima, busara na weredi na waweke kwenye hizi nafasi wakusaidie.
Uwe na usiku mwema Mh. Rais