Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa heshima zote naomba uupokee ushauri huu ukiona ni vema. Ninajua kuna wasaidizi wako wengi humu mitandaoni esp babalao JF.

USHAURI: Uza ndege zote, pesa itakayoatikana anzisha kilimo cha umwagiliaji. (Biashara ya usafiri wa anga achia sekta binafsi, wawekee mazingira rafiki ya biashara kisha wewe (serikali) utakuwa ni mkusanyaji wa kodi. Katika hilo uboreshe viwanja vya ndege). Anzisha irrigation system schemes za uhakika. Tuanzishe plantations za mazao mbalimbali ambapo tutaweza kupata malighafi kwa ajili ya viwanda vyetu na tutauza mazao mengine nchi za nje kisha tutapata fedha za kigeni. Ardhi nzuri ya kutosha yenye rutuba tunayo, maji tunayo. Mungu ametujalia haya.

Duniani kote mapinduzi ya viwanda yalitokea baada ya mapinduzi ya kilimo. Kilimo na viwanda vitakuwa ni mwarobani wa tatizo la ukosefu wa ajira.

Usiogope kuona tofauti na mtangulizi wako. Sio dhambi kuona tofauti na aliyekutangulia.

Bila unafiki naomba kuwasilisha.

YESU NI BWANA NA MWOKOZI!
😡😡😡😡😡😡😡😡
 
Ushauri mzuri kuwekeza kwenye kilimo.

Japo ni ku-challenge, kwanini shirika kuliko liendele kujiendesha kwa hasara kwa nilisitishe au kupunguza huduma zake kupisha covid-19 pandemic to pass?

Kingine wananchi tumeambiwa lockdown hakuna kwanini asituletee chanjo itakua jambo jema sana, chanjo mwili huku watu wanaendelea na uchapa kazi wanaouhamasisha kila siku.
 
Mkuu chanjo yenyewe haizuii kitu kama covid utapata usipovaa mask
 
Mkuu chanjo yenyewe haizuii kitu kama covid utapata usipovaa mask
Covid ata ukivaa mask risk ya kuipata ipo palepale lakini chanjo ni second protection inahitaji mkuu, kuna watu wanafanya kazi kwenye vitu vya afya wako kwenye risk kuliko wengine.

Usiamini sana uzushi unaoenezwa na mataifa,sasa ivi kuna chanjo nyingi sana kila taifa linajaribu ku-market chanjo yake ili kupata profit,ndio maana hear say ni nyingi mno.
 
Mama pia atambue akivaa Barakoa kwasababu yeye ni Kiongozi Wananchi wengi watamuiga Hilo litapunguza maambukizi
 
Leo niseme Tu ukweli kuwa wewe si mtu wa maneno maneno,,, ila your actions speak louder.. kitendo cha kumtumbua mkurugenzi wa TPA ni chakupongezwa...
kazi uliyobakisha sasa ni kuhimiza watu wavae barakoa na wafuate ushauri wa wataalam wa afya.
Wewe uwe mfano kwenye hili..vaa barakoa
 
Kwenye Corona, naomba tu usahau. Sera itabakia kuwa ile ile kama ya mtangulizi.

Dalili ya mvua ni mawingu. Hivyo kila mtu aendelee tu kuchukua tahadhali binafsi.
 
Leo niseme Tu ukweli kuwa wewe si mtu wa maneno maneno,,, ila your actions speak louder.. kitendo cha kumtumbua mkurugenzi wa TPA ni chakupongezwa...
kazi uliyobakisha sasa ni kuhimiza watu wavae barakoa na wafuate ushauri wa wataalam wa afya.
Wewe uwe mfano kwenye hili..vaa barakoa
Mtaharibu hapa mnapotaka kumpangia!
 
Asitembee na mabegi akigawa pesa barabarani, hiyo sio njia ya kumaliza matatizo ya wananchi
 
Uvaaji wa barakoa bila sosho distansing ni illihical, does not make sense na sio effective katika kupambana na korona

Ni muhimu kuja na mbinu shirikishi za kupambana na UVIKO 19 ambazo zitafanya kazi bila kuathiri uchumi binafsi, familia na Taifa kwa ujumla.

Kukopi moja kwa moja mbinu wanazotumia nchi nyingine inaweza kutofanya kazi, inabidi kujifunza walipokosea na walipoweza na kuzipersonalize mbinu hizo locally kama taifa, na zinaweza kuwa tofauti kati ya mkoa na mkoa, wilaya na wilaya, na hata kijiji na kijiji kama itabidi kulingana na mazingira halisi.
 
1. Ajira kwa wahitimu
waliorundikana mitaani hasa wale wa taaluma ya ualimu
2. Kupandisha mishahara na madaraja kwa wafanyakazi ambayo haijapanda tokea mwaka 2015
3. Uhuru wa vyombo vya habari
4. Bunge live
5. Uhuru wa kufanya siasa kwa vyama vyote
6. Kuendelea kujenga miundo mbinu
7. Kufuta kitambulisho Cha machinga au wajasiriamaliK Na Kuondoa mrundikano wa Kodi
8. Kurudisha FAO la kujitoa
9. Kurudisha Demokrasia ya kweli
10. Kupunguza riba kubwa ya bodi ya mikopo na kurudisha riba nafuu Kama ilvyokuwa kwa jk
N.k.

Kama Samia akiyafanya haya pamoja na mengine, nitakuwa wa kwanza kumsahau Hayati Magufuli kwani Mimi Ni mhanga wa mengi Kati ya hayo yaliyofanywa katika utawala wa Magufuli
 
Amani iwe nawe Mhe. Rais,

Naomba nikushauri yafuatayo kwa mustakabali wa nchi yetu Kiuchumi ili kutengeneza Tanzania imara kiuchumi.

1. Kwa upande wa Baraza la Mawaziri- Wateue Wabunge waliotoka kwenye private sectors na kuziongoza kwa Mafanikio kuwa Mawaziri wa Fedha na Viwanda na Biashara. Ondokana na hawa maprofesa waliokulia vyuoni kwenye hayo maeneo. Hii ni Kwa sababu watu hawa wataweka sera nzuri za fedha, uchumi na Biashara na kuiwezesha Tanzania kupaa kiuchumi.

2. Kwenye mashirika yetu ya kimkakati ( Tanapa, ATCL, Ngorogoro na Mengineo) , tafuta watu safi kutoka private sector( Makampuni na Mabenki) wenye rekodi ya kuendesha taasisi zao kwa faida na mafanikio na uwape haya mashirika. Najua tunao kina Nehemia Mchechu hapa na Charles Singili na wengineo wengi. Hutajutia huu uamuzi Kwa sababu sector hizi zinahitaji kuongozwa na watu wazoevu kwenye biashara ili kupata tija na mafanikio. Inawezekana usisite.

3. Kwenye sector za usimamizi wa Biashara na uchumi mf. BOT, TRA na kwingineko Pia, tafuta wataalamu wenye rekodi ya kufanya sekta binafsi Kwa mafanikio makubwa.

4. Kwa Bandari, tafuta mchumi mahiri kutoka JWTZ na awe seniour Officer, mpe Mamlaka ya Bandari aiongoze. Ila kwenye usaidizi muwekee timu ya wataalamu kutoka private sector wenye rekodi ya mafanikio kwenye biashara ili wamsaidie.

Mwisho hili liko nje ya mada ila nalo naomba lizingatie mama.

Kwenye utumishi wa umma hasa nafasi za RAS, DAS, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi nyeti ikiwemo za ulinzi na usalama zingatia sana seniority kwenye teuzi zako ili kuepuka power struggle. Kuna watu wapo kwenye maofisi na ni ma seniour sana, inapokuja kwenye nafasi wanazotakiwa kuwapa, wape tu, hii itaondoa vita kwenye taasisi zetu kuu za serikali hasa vya madaraka na uadui.

Mwisho hata kwenye wakuu wa mikoa na wilaya tafuta makada kutoka Chama chako au vyama vyenye mlengo tofauti wenye hekima, busara na weredi na waweke kwenye hizi nafasi wakusaidie.

Uwe na usiku mwema Mh. Rais
 
1. Ajira kwa wahitimu
waliorundikana mitaani hasa wale wa taaluma ya ualimu
2. Kupandisha mishahara na madaraja kwa wafanyakazi ambayo haijapanda tokea mwaka 2015
3. Uhuru wa vyombo vya habari
4. Bunge live
5. Uhuru wa kufanya siasa kwa vyama vyote
6. Kuendelea kujenga miundo mbinu
7. Kufuta kitambulisho Cha machinga au wajasiriamaliK Na Kuondoa mrundikano wa Kodi
8. Kurudisha FAO la kujitoa
9. Kurudisha Demokrasia ya kweli
N.k.

Kama Samia akiyafanya haya pamoja na mengine, nitakuwa wa kwanza kumsahau Hayati Magufuli kwani Mimi Ni mhanga wa mengi Kati ya hayo yaliyofanywa katika utawala wa Magufuli
Safi sana, itakuwa big step to the right direction.
 
Hakika mheshimiwa Rais umeanza kazi si kwa kishindo bali kwa haiba ambayo nimebahatika kuwashudia marais wa awamu kuanzia ya pila hadi leo hawakuwahi kuwa nayo .Kukubalika kwako na makundi yote iwe ndio fursa pekee ya kuhakikisha swala kuu kwa vijana linatatuliwa ingawaje kulimaliza ni ngumu kwani duniani kote ajira ni tatizo .Wakati wa utawala wa JK ajira sio kwamba zilikuwepo za kumwaga bali ni njia zilizotumika kujaza ajira serikali ndio iliyoonekana kuwa serikali kwa wakati huo ilikuwa inatoa ajira.Sifa kuu ya kupata ajira ilikuwa ni kwa njia ya ushindani na aliekosa ajira aliamini kuwa nafasi alikosa baada ya kufeli kwenye usaili.Piga marufuku ajira ambazo hazifuati utaratibu wa ushindani (interview)
 
1. Ajira kwa wahitimu
waliorundikana mitaani hasa wale wa taaluma ya ualimu
2. Kupandisha mishahara na madaraja kwa wafanyakazi ambayo haijapanda tokea mwaka 2015
3. Uhuru wa vyombo vya habari
4. Bunge live
5. Uhuru wa kufanya siasa kwa vyama vyote
6. Kuendelea kujenga miundo mbinu
7. Kufuta kitambulisho Cha machinga au wajasiriamaliK Na Kuondoa mrundikano wa Kodi
8. Kurudisha FAO la kujitoa
9. Kurudisha Demokrasia ya kweli
N.k.

Kama Samia akiyafanya haya pamoja na mengine, nitakuwa wa kwanza kumsahau Hayati Magufuli kwani Mimi Ni mhanga wa mengi Kati ya hayo yaliyofanywa katika utawala wa Magufuli
Akifanya mambo mawili tu kwanza!

1
Kukomesha watu wasiojulikana na kuruhusu uchunguzi huru kujua wanaofanya matukio hayo ambayo ni kama;
Kushambuliwa Mh Lisu
Kupotea Ben saanane
Azor gwanda nk.

2
Kuruhusu uhuru wa kufanya siasa kwa vyama vyote.

Mengine ni pamoja na kuchukuliwa hatua viongozi wote waliofanya kazi nje ya sheria ambao ni kama kina sabaya, huyu nanilii wa Mbeya na wengine wa aina hiyo
 
Back
Top Bottom