Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mwambie huyo jamaa asiye jifahamu yeye ni nani.
 
Yote yaweza kuwa sahihi lakini kwanini wanaotaka chanjo waambiwe waende nchi za nje? Kwanini zisije ili wanaotaka wapate badala ya kupangiwa na wasiozitaka! Inamaana dunia nzima haijipendi na tunaojipenda na wenye umakini ni sisi tu linalokuja suala la chanjo!
 
Sio kweli ,baada ya 2015 ndio upuuzi wa kuhamishia wafanyakazi toka halmshauri kuja kwenye mashirika ya umma ndio ulishamiri
Sasa mkuu hilo lina shida? Serikalini kuna nafasi zinatangazwa internally kwa watumishi kama una uwezo unaomba.

Mfano, jamaa yangu alitoka chuo akahamia kwenye misitu.

Naona umehama mada kutoka recruitment kuja transfer.
 
Utafiti umeonyesha watu waliochanja chanjo za kuzuia mafua (common cold) wana hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa ya njia ya hewa ikiwemo covid-19.

Hii kitaalamu inaitwa vaccine driven enhancement of pulmonary infections. Wizara ya afya wawe makini kufanya mass vaccinations ya korona ili kusije kuwa na shida kubwa huko mbeleni na kusababisha 'impairment of population immunity to pulmonary infections' jambo ambalo litapelekea watu kutegemea periodic boosters, yaani tutalazimika kuchanja kila baada ya miezi 6 kuweza ku-sustain immunity. Atakayehitaji chanjo anaweza kwenda kivyake vyake kuchanja na siyo serikali kufanya kampeni ya chanjo ya covid-19.
 
Mimi sitachanja kabisaaa
 
Nenda hapo Kenya zipo sisi TZ mpaka research zao zikamilike na kuwe na chanjo kamili siyo majaribio yao wanayofanya kwa sasa.
 
Nenda hapo Kenya zipo sisi TZ mpaka research zao zikamilike na kuwe na chanjo kamili siyo majaribio yao wanayofanya kwa sasa.
Acha kulazimisha kupangia watu. Unaposema sisi Watanzania nani kakupa haki ya kuwapangia wengine?
 
Shida ilianzia pale ugonjwa huu ulipobebwa kama ajenda kuu za kisiasa na wapinzani na watawala.
Ndio maana unaona hata humu kuna comments nyingi za vijiweni bila chembe ya utaalamu hata kidogo..”Oh sisi tunasema hivi”
 
Mama usituangushe tafadhali

Yaani mama kaanza vizuri huyu kaanza vizuri sana

Tumuombee apata VP mwenye kasi na mtazamo kama wake

Mataga sijui tukimbilie wapi maana kimeumana[emoji28][emoji23]

Kiukweli hii nchi tunahitaji sana maendeleo,haki,demokrasia na uhuru kwa mbali naiona Tanzania ikisonga mbele zaidi.

Nawaambia hata uchumi utaanza kukua nahisi hivyo yaani siku tatu tushafichuliwa madudu na ufisadi wa awamu ya tano A (2015-2021) hii ndoto niliiota mda sana nikitamani ufisadi wa awamu ya tano uje kuumbuka hadharani.

Mama piga kazi usiogope sasa wanaufyata na kuufyatua.

Naombeni wazee wa chama (JK, MALECHELA, MANGULA, SHEIN, AMANI KARUME,MAKAMBA)mshikeni huyu mama mkono msapotini kwa kila hali asonge mbele maana najua kuna magenge hayamtakii mema kabisa ndani ya chama

Samia hoyeeee
 
Daah kweli Mama hamtupi mtu Mungu ni mwema kwa kweli hicho kikundi cha wahuni kimetutesa sana ila machozi yetu na maumivu tuliyonayo sio ya kuisha leo.
 
Hivi huyo jamaa mwenye hips kubwa anaepata watoto kwa njia ya kupandikizwa yupo wapi?? Na je lile zuio la USA kuwa asiingie nchini mwao liliishia wapi!??
 
Mama atafanya vizuri kwa kuwa ni muumini wa haki, ukiwa mtenda haki Mambo huwa yanajiset yenyewe na unakuwa hutumii nguvu nyingi kwenye uongozi wako, kumbuka haki huinua Taifa. Tunaendelea kumuombea Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan ili Mwenyezi Mungu aendelee kumpa hekima na busara na pia maisha marefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…