Binafsi naanza kuona vijembe na mizaha jukwaani. Mara mwenye jinsia ya kike, Mara macho yamelegea, hii yote ya nini? Kweli hadi hapo bado unataka sifa za maumbile? Rais akumbuke kuna kundi pembeni linaangalia kama kabadilika tabia.
Tabia wanayoifahamu tangu akiwa waziri na baadaye Makamu wa Rais. Sasa kama kuna tabia hataziacha, huo ndo upenyo wa kuingilia kuharibu mambo. Tutaanza kuona tena nchi inaendeshwa kwa vimemo vya ikulu.
Mtangulizi alikomesha tabia fulani za mitaani kwa tabia yake ya kutotabilika. Dakika moja mzaha mara mtu katumbuliwa. Sasa huyu rais mpya akataposhindwa kuachana na tabia zake walizozizoea huko maofisini, itakuwa ni kuwaangusha akina mama wote wanaofuata nyayo. Asidhani hazitembei huku mitaani. Amepanda jukwaa, soon tutaanza kuambiwa hata yasiyofaa kwenye jamii hii yenye masculinity.