Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hawa wachonganishi ,kwa kawaida ni watu wenye wivu,fitina na roho mbaya.Hawa ni wengi sana makazini.Hawa ,baadae ndio watampinga mama pia.
 
Please I do not want your ignorance, and do not follow me the great mule you

Tuheshimiane tafadhari
Ukiandika ujknga lazima utapingwa kwa lugha ileile uliyo itumia.
 
Huwa napenda kuona mtu anayebalansi habari/uchambuzi.
Pakukosea anakosea na pa kusifia anasifia pia
 
RAIS SAMIA ATAFANYA YAFUATAYO KATIKA UONGOZI WAKE

1. Kudhibiti mfumuko wa bei.

2. Kuboresha mazingira ya uwekezaji.

3. Kuimarisha uzalishaji na usalama wa chakula.

4. Kuimarisha upatikanaji wa mbolea nchini.

5. Kuimarisha mbinu za kupambana na nzige.

6. Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.

7. Kuimarisha vyama vya ushirika.

8. Kuimarisha uzalishaji wa mbegu zinazoongeza upatikanaji wa malighafi zinazotumiwa kutengeneza mafuta ya kula.

9. Kuhamasisha ufugaji wa kisasa.

10. Kuimarisha uvuvi wa bahari kuu.

11. Kuimarisha sekta ya utalii.

12. Kuimarisha uwekezaji wa kimkakati katika madini.

13. Kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini.

14. Kusimamia masoko ya madini.

15. Kusimamia usambazaji umeme vijijini.

16. Kusimamia ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani (Tanga, Tanzania).

17. Kuimarisha sekta ya viwanda.

18. Kupanua wigo wa masoko ya ndani na nje ya nchi ili wakulima na wafanyabiashara wanufaike.

19. Kutekeleza mipango ya upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi.

20. Kujenga madaraja maeneo mbalimbali.

21. Kujenga na kukarabati viwanja vya ndege.

22. Kununua ndege tatu mpya.

23. Kujenga na kukarabati barabara.

24. Kujenga na kukarabati nyumba na majengo ya serikali.

25. Kuendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

26. Kuingiza nchini vichwa vya treni na mabehewa.

27. Kuboresha bandari za Dar, Mtwara na Tanga.

28. Kuongeza matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya kasi.

29. Kuinua kiwango cha ubora wa elimu.

30. Kuimarisha utoaji mikopo ya elimu ya juu.

31. Kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu ili kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu nchini.

32. Kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

33. Kutoa mafunzo kazini kwa walimu na wakufunzi.

34. Kukamilisha miradi 924 ya maji inayoendelea kujengwa nchini.

35. Kuanza utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 28.

36. Kuboresha huduma za maji jijini Dodoma kwa kujenga bwawa la Farkwa.

37. Kutekeleza mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu.

38. Kutekeleza miradi ya maji na mazingira Dar, Mara, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.

39. Kuendeleza utekelezaji wa Hospitali za Rufaa za Kanda mbalimbali na Hospitali maalumu.

40. Kuendeleza ujenzi na ukarabati wa hospitali za Halmashauri 102, vituo vya afya 487 na ujenzi wa zahanati 1,198.

41. Kununua mitambo 12 yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya mitungi 200 ya hewa ya oksijeni kwa siku.

42. Kuendelea kuimarisha huduma za kibingwa nchini.
43. Kuendeleza uboreshaji wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya unaoendelea kote nchini.

44. Kuendelea kuliimarisha na kuliongezea uwezo JWTZ na Majeshi mengine.

45. Kuendelea kuboresha mazingira ya kazi na wafanyakazi.

46. Kuziimarisha taasisi za Hifadhi ya Jamii ili ziwanufaishe wafanyakazi.

47. Kuhakikisha asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri inawafikia walengwa.

48. Kuendelea kuratibu utekelezaji wa masuala ya ukuzaji ajira na kazi za staha.

49. Kuuendeleza Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma.

50. Kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI.

51. Kuendeleza mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

52. Kuimarisha mikakati ya kuzuia, kupunguza, kujiandaa na kukabili maafa pindi yanapotokea.

53. Kuimarisha mikakati ya kuhifadhi mazingira.

54. Kuendeleza vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

55. Kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za muungano.

56. Kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na mataifa mengine pamoja na mashirika/jumuiya za kikanda na kimataifa.
57. Kuimarisha utamaduni, michezo na Sanaa.🇹🇿🇹🇿
 
Hizi kelele na miluzi mingi zitakuangusha ktk uongozi wako. Vunja Baraza la mawaziri unda upya, hizi kelele za kina musiba kibajaji, musukuma zitaisha. Watakuogopa.

Sasa hivi Kuna kelele nyingi wengine wanakukubali lakini lipo kundi la wachache hawakukubali kabisa.

USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA
 
Haitakiwi wamuogope inapaswa wamheshimu
 
Mbowe lini anavunja chadema ili aunde upya?
 
Tunafunga ramadhan kwanza. Muda huu tunatumia pia kuchuja maoni yote yakiwemo ya wenye mihemko kama wewe. Pia hatuongozwi na sosho midia isipokuwa utashi wa kiasi kadiri mama anavoamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…