Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hbr na habar za eid Wala wenzangu na Mimi!

Iwe alijua au hajajua amekuwa msikivu haswaa na huu ndo uadilifu wa kiongozi mkuu anavyotakiwa!
Yaan awe alipanga au hakupanga alimradi uitikio ameufanya ambayo Aya Mambo tuliyakosa muda mwingi saana.
Asnt mama!
 
Watu kama nyinyi mngefungiwa tu kuweka thread humu, sasa ndo nini hii umeandika?
 
Hbr na habar za eid Wala wenzangu na Mimi!

Iwe alijua au hajajua amekuwa msikivu haswaa na huu ndo uadilifu wa kiongozi mkuu anavyotakiwa!
Yaan awe alipanga au hakupanga alimradi uitikio ameufanya ambayo Aya Mambo tuliyakosa muda mwingi saana.
Asnt mama!
Yaani umeandika kana kwamba wote tupo kichwani mwako!! 😁😁😁
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Ushauri wangu ni kuwa awe makini katika kutoa maamuzi na zwe thabiti na maamuzi yake hayo kwani wote wanaomchukia marehemu JPM watayakubali tu. Kutoa maamuzi na kuyabadilisha keshoi yake ni dalili ya kupwaya ambayo siyo sifa ya ya mtu kuwa rais. Mifano ya teua+tengua na kodi_miamala+kodi_miamala_iangaliwe_upya ni dalili mbovu.
 
Hakuna mtu anayependa kulipa kodi, nadhani wewe mwenyewe umeshuhudia lawama unazopokea kwa sasa.

Iko hivi, hakuna mfanyabiashara duniani, anayetoa kodi kwa hiari na furaha, ni kwa sababu tu wanabanwa.

Wanasoka Nguli duniani, matajiri wanakwepa kodi licha ya utajiri wanaomiliki.

Sembuse Watanzania?

Mtangulizi wako baada ya kuwabana watu watoe kodi, wakakimbia nchi, nakushutumu mazingira mabaya ya biashara nchini. Mwenzako, akakomaa hivyo hivyo kubana, akapata pesa ya kupeleka maji sehemu zilizosahaurika kama Tabora.

Leo hii waliokimbia kutoa kodi, wanatuambia rais haleti maendeleo kinacholeta ni kodi, kodi ipi kama walikimbia kulipa kodi.

Mwisho, usipokaza utaendelea kuwanyonya maskini (Ambao ni 90%) ya watanzania. Na kuacha wenye kipato kikubwa wakitesa.
Utawala wa Samia utawafavor matajiri sio makapuku
 
Maskini safari hii mmeguswa! Kilio kila kona. Kama vipi tuungane basi kuiondoa ccm madarakani.

Maana karibia nusu ya makusanyo ya hizo kodi zenyewe kila mwezi, hutumika kulipia mishahara na kuendeshea serikali.
Maskini wapi unaowaongelea? Hawa Watanzania? Wapo tayari wanyonywe Hadi Senti ya Mwisho lakini usiiguse CCM
 
Ndugu Mheshimiwa Rais. Katika siku hii ya kuzaliwa na ya sherehe, ninakutakia afya njema, mafanikio katika kazi yako inayowajibika kwa ustawi wa Urusi, furaha ya kibinafsi na ustawi kwako na kwa wapendwa wako. Mei uwe na msaada wa dhati na kamili kutoka kwa wenzako na marafiki
 
Mh rais Samia suluhu Hassan ccm ni chama kinachoelekea kufa ndio maana kina hulka za kibabe na pia tabia za magufuli kutumia nguvu zisiweke kivuli kwenye haiba yako. Tumia busara kuliko nguvu. Mwisho wa siku utapimwa wewe Kama wewe.
 
Kishachafuka huyo Mkuu na si ndani ya nchi tu bali mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.

Mh rais Samia suluhu Hassan ccm ni chama kinachoelekea kufa ndio maana kina hulka za kibabe na pia tabia za magufuli kutumia nguvu zisiweke kivuli kwenye haiba yako. Tumia busara kuliko nguvu. Mwisho wa siku utapimwa wewe Kama wewe.
 
Chama ni kikubwa kuliko mtu bila CCM Samia si kitu CCM ipo pale na itakuwa pale ni sawa na Chadema leo umwambie Mbowe afanye mambo nje ya idiology ya Chadema haitowezekana
 
Mh rais Samia suluhu Hassan ccm ni chama kinachoelekea kufa ndio maana kina hulka za kibabe na pia tabia za magufuli kutumia nguvu zisiweke kivuli kwenye haiba yako. Tumia busara kuliko nguvu. Mwisho wa siku utapimwa wewe Kama wewe.
Kuandika kwenyewe hujui kuandika mbwa wewe halafu unasema utmbo gani???!!
 
Wewe ni Mama Raisi wetu mpendwa, kuwa na huruma Mwenyekiti wetu amatekwa na Mapolisi wa huko Mwanza.
 
Tatizo mwenyekiti alitaka kumpanda kichwani, kuna lugha za kimabavu zilikuwa zinatumika tofauti na enzi za mwendazake....ni kama walikuwa wanamuona ni dhaifu na kumletea dharau, nafikiri kaamua kuwaonyesha kuwa na yeye ana wembe ule ule, akiamua kuwanyoa anaweza !
 
Back
Top Bottom