Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Ni jasiri sana!! Haogopi dhoruba ya angani, January to December anakata mawimbi tu!! Leo yupo Paris. Ha ha haaaa
 
Kwa mvua kunyesha...
Kwa mvua kuacha kunyesha...
Kwa kusaidia miradi na kutoa hela zake mfukoni kutekeleza hii miradi ambayo MKAPA, JK JPM walishindwa...
Kwa kusafiri sana nje nchi kuliko rais yeyote yule aliyepita...
Kwa kuwakaribisha tena WAARABU kwenye sekta nyeti nchni...
Kuhakikisha watoto wa kike wanarudi shule baada ya kuzaa hata kama walijitakia wenyewe au MAFATAKI kuhusika!
Kwa kuwazawadia vyeo kina Makonda na Makamba hata kama wamevurunda...

Ndio lazima UANZE NA KUMSHUKURU DR SAMIA H S HASSAN HATA KAMA UMEPATA MLO WA SIKU!

KAMA KOREA KASIKAZINI! MTAISOMA NAMBA TU...
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Pongezi kwako Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT. Natoa pongezi jioni hii ili kuwahi asubuhi njema ijayo
 
WANAOMTUMA MANGE KIMAMBI WANAOGOPA MAMBO MAKUBWA ANAFANYA RAIS SAMIA

Anaandika Ben Mzalendo

Wote ni mashuhuda wa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliingia Madarakani na hofu mbalimbali zilizokuwepo miongoni mwa watanzania lakini ndani ya muda mfupi uongozi na style yake ya uongozi, mikakati mikubwa ya kimaendeleo na matokeo chanya yaliwaacha wengi midomo wazi.

Ni dhahiri sio wote wanapendezwa na mambo makubwa na matokeo yake anafanya Rais Samia kwa watanzania, option pekee waliyonayo ni kutumia watu aina ya Mange kimambi kumchafua Mitandaoni.

Rais Samia ndani ya Miaka mitatu ya Uongozi wake Sekta mbalimbali tumeshuhudia matokeo chanya na ya dhahiri leo nitagusia Sekta chache muhimu sana.

Kwa Upande wa Sekta ya Afya Nchini ambayo imekuwa kilio na changamoto nyingi ndani ya Miaka Mitatu Rais Samia amefanikisha Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika maeneo mbalimbali nchini ambao umewezesha Vituo vya kutolea huduma za Afya kuongezeka kutoka vituo 8,549 Mwaka 2021 hadi vituo 9,693 mwaka 2024.

Jitihada za Rais Samia zimefanikisha kuongezeka kwa Vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo; - MRI kutoka 7 hadi 13, CT-Scan kutoka 12 hadi 45, Digital X-RAY kutoka 147 hadi 346, Ultrasound kutoka 476 hadi 668, Echocardiogram kutoka 95 hadi 102, Cathlab kutoka 1 hadi 4, Pet Scan imenunuliwa 1 ambayo awali haikuwepo Katika kipindi cha miaka mitatu.

Jitihada za Rais Samia zimefanikisha Kuongezeka kwa idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka vitanda 86,131 mwaka 2021 hadi vitanda 145,374 Machi 2024.

Jitihada za Rais Samia zimefanikisha kuongezeka kwa idadi ya vitanda kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU) katika vituo vya umma kutoka vitanda 258 vya mwaka 2021 hadi kufikia vitanda 1,362 Machi 2024.

Kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa dawa na bidhaa za Afya (aina 290) katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma kutoka asilimia 58 kufikia asilimia 79 Machi 2024.

Kuongezeka kwa idadi ya Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa ya dharura (EMD) kutoka saba (7) mwaka 2020 hadi kufikia 116 Machi 2024.

Jitihada za Rais Samia zimefanikisha Kupatikana kwa huduma za ubingwa na ubingwa bobezi kwa gharama nafuu nchini na pia kuvutia wagonjwa kutoka nje ya nchi (Tiba Utalii) ambapo wagonjwa kutoka nje ya nchi wameongezeka kutoka 5,705 mwaka 2022 hadi 7,843 mwaka 2024. Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za afya vyenye uwezo wa kutoa huduma za dharura za uzazi ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (CEmONC) kutoka 388 mwaka 2021 hadi 523 mwaka 2024.

Jitihada za Rais Samia zimefanikisha Kupungua kwa vifo vya wajawazito kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 na kupungua kwa vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000. Kupungua kwa vifo vitokanavyo na UKIMWI kutoka vifo 29,000 mwaka 2022 hadi vifo 22,000 Machi 2024 na Kifua Kikuu kutoka vifo 25,800 mwaka 2022 hadi vifo 18,100 Machi 2024.

Kwa Upande wa Sekta ya Maliasili na Utalii ambayo kipindi Rais Samia anaingia Madarakani ilikua kwenye hali mbaya sana tena sana ndani ya muda mfupi wa miaka mitatu kwa juhudi zake amefanikisha.

Kuongezeka kwa idadi ya watalii ambapo idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 96 kutoka watalii 922,692 Mwaka 2021 hadi watalii 1,808,205 Mwaka 2023. Aidha, idadi ya Watalii wa Ndani waliotembelea vivutio vya utalii imeongezeka kwa asilimia 152 kutoka watalii 788,933 Mwaka 2021 hadi kufikia watalii 1,985,707 Mwaka 2023. Hii ni rekodi kubwa haijapata kufikiwa katika Nchi yetu.

Rais Samia amefanikisha Kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii ambapo mapato yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.4 Mwaka 2023 sawa na ongezeko la asilimia 161 kwa watalii wa kimataifa.

Rais Samia amefanikisha Kuimarika kwa ulinzi na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori kumeiwezesha Tanzania kuendelea kuongoza barani Afrika kwa kuwa na simba wapatao 17,000; nyati 225,000; na chui 24,000. Sambamba na hilo, takwimu zinaonesha kuwa faru wameongezeka kutoka 163 Mwaka 2021 hadi 252 Aprili, 2024.


Ndani ya Miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Sekta ya Mifugo na Uvuvi makubwa yamefanyika kwanza ni idadi kubwa ya Bajeti kupanda haijapata kutokea, kwa mwaka wa fedha wa 2023 /2024 ilipanda kwa asilimia 74, Bajeti ilikuwa Bilioni 295. 9 kutoka Bilioni 169 za mwaka 2022. Kwa mwaka wa fedha wa 2024 /2025 Bajeti imepanda zaidi hadi Bilioni 460.33 haijapata kutokea tangu Uhuru!!
Zaidi ya wafugaji 8413 wamenufaika na mikopo, thamani ya mauzo ya Uvuvi Nje ya nchi yameongezeka zaidi, Wavuvi zaidi ya Elfu 6, 444 wamenufaika na boti mpya za kisasa, hakuna kuchomewa nyavu tena!!

Ndani ya Miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Sekta ya Madini Imepata mafanikio makubwa ambayo haijapata kutokea, Watanzania zaidi ya Elfu 18,475 wameajiriwa kwenye migodi kwa mwaka 2023, Leseni zaidi ya Elfu 8,595 zimetolewa za utafutaji, uchimbaji, Biashara na uongezaji thamani madini. Bilioni zaidi ya 106.1 zimepatikana kutokana na mrahaba na Ada za ukaguzi kwenye mauzo ya dhahabu, bati, almasi na Tanzanite. Zaidi ya Vituo 100 vya madini vimeanzishwa na maeneo zaidi ya 37 yametengwa kurasimisha shughuli za uchimbaji ulio rasmi.

Ndani ya Kipindi cha Miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Sekta ya Utumishi yamefanyika makubwa ambayo yalikua hayajafanyika kwa muda mrefu sana.

Watumishi zaidi ya Elfu 375,319 wamepandishwa vyeo kwa gharama ya Shilingi bilioni 85.89.
Watumishi zaidi ya Elfu 142,793 wamelipwa malimbikizo ya Mishahara jumla ya Shilingi bilioni 240.7 zimetumika, watumishi 81,561 watapandishwa vyeo kabla ya Mwaka huu wa Fedha kukamilika jumla ya Shilingi bilioni 90.85 zitatumika. Ndani ya Kipindi kifupi cha Rais Samia Watumishi wa umma wapya Elfu 81,137 wameajiriwa katika Taasisi mbalimbali za umma.
Kubwa Zaidi Rais Samia ametenga Bilioni 230.03 kuajiri watumishi wengine Elfu 47,374 hii haijapata kutokea!!!

Wote ni Mashahidi namna Uongozi wa Rais Samia unavyogusa wananchi wa Tanzania kwa kuwaletea maendeleo kwa kasi kubwa. Rais Samia anaoongoza Nchi kwa ujasiri, umahiri akizingatia adhima yake ya maridhiano, mabadiliko, ustahimilivu na kujenga upya kwa kuzingatia utawala bora na kuchochea maendeleo kiuchumi na kijamii pamoja na kuifanya Nchi yetu kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Hatua zote hizi lazima baadhi ya watu waogope, wanune, wafadhaike na wajae sonona usoni wanabaki na option za kuwatumia akina Mange kimambi kumchafua Rais wetu na kujaribu kuharibu Taswira yake njema.

Haijapata Kutokea Rais wa Nchi kupata Degree za Heshima kutoka Vyuo Vikuu Vitano tofauti duniani ndani ya Miaka mitatu ya uongozi wake ila yametokea kwa Rais Samia.

Rai yangu kwa Rais Samia ni kusonga mbele na kupuuza makelele Watanzania tulio wengi tunakupenda, tunakuombea na 2025 tutakupigia kura nyingi za kishindo haijapata kutokea!!!
 

Attachments

  • IMG-20240604-WA0077.jpg
    IMG-20240604-WA0077.jpg
    30.5 KB · Views: 3
Nilitamani mama afanikiwe na bado natamani!

Mimi ni miongoni mwa wale tuliotolewa upinzani kwa nguvu na kujiunga CCM. Sijui leo nina sura gani, lakini kwa kuwa sura yangu ya kwanza ilikuwa kusema ukweli, basi hapo ndipo nitabaki na wala andiko hili lisihusishwe na chama chochote!

Maendeleo ni hatua, sio mafuriko! Marais wote tangu uhuru wamekopa trilioni 61 kwa miaka 60 hawakuwa wajinga. Tuliomba uhuru ili tujitawale, na ili tujitawale ni lazima tuwe na usemi juu ya uchumi wetu.

Bajeti ya Wizara ya Fedha ya mwaka 2024/2025 inasema bajeti nzima ni trilioni 18, ambapo malipo ya madeni ni trilioni 13. Hii ni nini? Kawaida nikifikia mahali kama hapa, naamsha jazba, lakini leo siziamshi.

Bajeti hii inasema tumebakiza asilimia 29 tu kama nchi kupigwa bei. Yaani, atakayeongeza hiyo asilimia 29, basi kama nchi tutaangamia. Kwanini tufike hapa? Vidole vinaingia baridi! Kwanini tunatamani maendeleo ya haraka ambayo hatuna uwezo nayo, kwanini tunageuka kahaba?

Kwa bajeti hiyo, maana yake tunakopa ili kulipa mikopo. Tunakopa kwa riba ili kulipa riba sehemu nyingine. Bajeti hii ni hatari sana kwetu, haitupi nafasi ya kupumua! Sio salama kwa usalama wa taifa.

Ukomo wetu wa bajeti kwa pato la taifa ni asilimia 80, leo tunachezea asilimia 71. What if? What if tukiingia kwenye janga kubwa la kitaifa? What if dunia ikiingia kwenye mdororo wa kiuchumi kwa sababu ya vita hizi zinazoendelea?

Mikopo hii! Sijui nisemeje, vidole vina ganzi! Leo serikali inataka kufanya biashara, NFRA inawafukuza wafanyabiashara wa kati ili wauzie WFP. Huu ni mfano tu, ipo mingi!

Unajua kwanini serikali duniani kote zilishindwa kufanya biashara na kuachia hiyo kazi wafanyabiashara? Yaani, badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma. Inakuwa kama tumevumbua jinsi ya kuwasha moto kwa ulimbombo na ulindi wakati dunia ilishatoka huko.

Aluta continua!

Victoria Aserta!
 
Nilitamani mama afanikiwe na bado natamani!

Mimi ni miongoni mwa wale tuliotolewa upinzani kwa nguvu na kujiunga CCM. Sijui leo nina sura gani, lakini kwa kuwa sura yangu ya kwanza ilikuwa kusema ukweli, basi hapo ndipo nitabaki na wala andiko hili lisihusishwe na chama chochote...
Wewe na Waziri wa Fedha mwenye PhD ya uchumi nani anajua zaidi? Nape kasema fanyeni kazi
 
Nani alikuambia serikali duniani kote zimeshindwa kufanya biashara?

Jielimishe dunia inavyoenda.Kufeli kwa ccm kufanya biashara haina maana serikali zote duniani zimefeli.
 
Nani alikuambia serikali duniani kote zimeshindwa kufanya biashara?
Jielimishe dunia inavyoenda.Kufeli kwa ccm kufanya biashara haina maana serikali zote duniani zimefeli.
Serikali gani imepatia?
 
Serikali gani imepatia?
Nilitegemea utatafuta maarifa mwenyewe ili kujua kama nilichokisema ni sahihi,badala yake unataka kutafuniwa kila kitu,jambo ambalo ni la kawaida kwa wasomi wajinga mliojaa nchi hii.

Nitakupa mifano michache;Ethiopia airways inamilikiwa na serikali mwaka jana imepata faida ya 800 usd.

DP World, US railway company,Algeria telecom, British airways na kampuni nyingi zinazomilikiwa na serikali zinapata faida, kwasababu zinaendeshwa na watu compentent tofauti na hapa kwenu.

Mwisho;jifunze kujitafutia maarifa mwenyewe.
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo...
Bila ya kuondoa kikokotoo kwa mara ya kwanza nitatumia haki yangu ya kikatiba kumkataa na chama chake. Hata kama yeye na chama chake CCM atachaguliwa na raia wote wa Tanzania moja ya hapana itakuwa ya kwangu.
 
Namkubali sana, Mungu aendelee kumpa maisha marefu, hekima na busara.

GOD BLESS ISRAEL
 
Nimetembea mitaani nimejuonea Kila mtz timamu hamkubali huyu mother.kila mmoja anasema huyu mama hamna kitu kabisa
 
Back
Top Bottom