Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Raisi amefikia kusikiliza washauri wake wanamwambia serikali inunue engine za diesel kwa ajiri ya kuendesha tren za umeme na mawazo hayo anaona nisahihi ! Badala ya kuboresha umeme wa uhakika yeye anaona Kila wazo linaloletwa na kadogosa lipo Sawa hata kweli huyu ccm huyo ndiye mnataka aendelee kutuongozea nchi yetu !
Raisi anapaswa kuwa na msimamo katika kuendesha nchi mawazo mengine ya viongozi wake inatakiwa ayachakate aone kama yanafaa au hayafai siyo Kila kitu kukubali ! Raisi unahujumiwa mbele ya wapiga Kura wako unaona Sawa.
Sgr hadi Sasa mkandarasi kakimbia site hakuna hela mradi umesimama siyo mwanza shinyanga wala tabora hakuna kinachoendelea.
Haya tumekubali leteni hizo nchini tunasubiri 2025

CCM wote wenye mapenzi mema na hii nchi tangazeni kugombea uraisi hata mkiwa kwenye mahoteli/nyumbani kwenu kama alichofanya tundu lisu kuelekea 2025 Hana cha kuwafanya huyo mama yenu hamzuiiwi kikatiba na hakuna form moja kama inavyosema.
Gentleman,
Diesel na Gas ni mbadala muafaka wa nishati ya umeme,

Kuna ubaya gani kua na alternative energies sources kuendesha machine kama sgr?🐒
 
Raisi amefikia kusikiliza washauri wake wanamwambia serikali inunue engine za diesel kwa ajiri ya kuendesha tren za umeme na mawazo hayo anaona nisahihi ! Badala ya kuboresha umeme wa uhakika yeye anaona Kila wazo linaloletwa na kadogosa lipo Sawa hata kweli huyu ccm huyo ndiye mnataka aendelee kutuongozea nchi yetu !
Raisi anapaswa kuwa na msimamo katika kuendesha nchi mawazo mengine ya viongozi wake inatakiwa ayachakate aone kama yanafaa au hayafai siyo Kila kitu kukubali ! Raisi unahujumiwa mbele ya wapiga Kura wako unaona Sawa.
Sgr hadi Sasa mkandarasi kakimbia site hakuna hela mradi umesimama siyo mwanza shinyanga wala tabora hakuna kinachoendelea.
Haya tumekubali leteni hizo nchini tunasubiri 2025

CCM wote wenye mapenzi mema na hii nchi tangazeni kugombea uraisi hata mkiwa kwenye mahoteli/nyumbani kwenu kama alichofanya tundu lisu kuelekea 2025 Hana cha kuwafanya huyo mama yenu hamzuiiwi kikatiba na hakuna form moja kama inavyosema.
 
Attachments

  • IMG-20241213-WA0037.jpg
    IMG-20241213-WA0037.jpg
    86.1 KB · Views: 3

Bila kujali hilo la mabehewa ya 'diesel'; Samia hajawahi kuiweza nchi kwa jambo lolote lile isipo kuwa kuinadisha tu basi.
CCM wote wenye mapenzi mema na hii nchi tangazeni kugombea uraisi hata mkiwa kwenye mahoteli/nyumbani kwenu kama alichofanya tundu lisu kuelekea 2025 Hana cha kuwafanya huyo mama yenu hamzuiiwi kikatiba na hakuna form moja kama inavyosema.
Wote hawa unao wategemea kumpinga Samia wapo kwenye sehemu walipo kwa sababu yake, Samia kama Mwenyekiti wao. Akikohoa leo wote wana lala chini!
Nani, akina Makamba, Nepi Nnauye, au nani ndani ya CCM unaye weza kumtegemea afanye kinyume cha Mwenyekiti?
Labda Luhaga Mpina peke yake!
 
Rais Samia Suluhu Hassan: Rais wa Kwanza Mwanamke wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan aliweka historia mwaka 2021 alipokuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania. Tangu wakati huo, ameendelea kusimamia mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii, akithibitisha kuwa uongozi wa wanawake unaweza kuleta matokeo bora kwa nchi nzima. Pia ni kiongozi wa tano mwanamke kutoka Afrika kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akitoa sauti kwa bara lake kwenye majukwaa ya kimataifa
 
Ipo hivi. Spain ina SGR electric train ambazo pia zina alternative engine za diesel. Umeme ukikatika, engine za diesel zinawashwa safari inaendelea,umeme ukirudi then electric engine zinaendelea kufanya kazi. Vinanunuliwa vichwa vichache vya dharula.Ila wabongo kwa kupinga hamjambo. Mtaendeleaje msipojaribu kila alternative.
 
Ameachia sana pesa mtaani, inabidi a-apply contraction monetary policy ku-balance heshima mtaani
 
1. Muundo wa wakuu wa idara ya msingi na secondary ndani ya Halmashauri,arekebishe!
Nikimaanisha hii iwe idara Moja TU. Kupunguza mzigo na matumizi makubwa ndani ya Halmashauri.

2. Kuna viongozi wanaoshinda mitandaoni,ilinkuonyesha wanafanya kazi ,kumbe wao kazi ni kunitangaza mitandaoni TU. Hawa awaondoee kabisa.

3. Takukuru ifutwe,Haina kazi Kwa Sasa,kiundwe chombo maalumu cha kufuatilia mifumo ya fedha,matumizi na mapato ya serikali na Halmashauri.
Takukuru nao siku hizi ni wachukua rushwa na kupeleka kesi za kuku mahakamani na kuficha kesi za Ng'ombe
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
1. Tume zinazoundwa nyuma ya mikamera majibu hizo tume nyuma ya pazia, yaani hakuna
Commission of inquiries are for public interest

2. Wasiojulikana ama wanaojulikana kuendelea kutojulikana
Nisawa na changamoto kuto tatuliwa kwa wakati
Problems are supposed to be resolved at desired time, (mapuuza husabisha majanga),
Similarly to, any decision you make in life you will be responsible for it
 
Sifa za Rais Samia Suluhu Hassan:

Uwezo wa Kujenga Uhusiano
: Rais Samia ni kiongozi anayejulikana kwa uwezo wake wa kujenga uhusiano mzuri na watu wa tabaka mbalimbali. Ana mtindo wa uongozi unaoonyesha kujali na kuheshimu wengine. Katika nyakati za changamoto, Rais Samia amekuwa na uwezo wa kujenga muungano wa kitaifa, na hii ni muhimu kwa nchi kama Tanzania, ambayo ina mchanganyiko wa makabila, dini, na tamaduni mbalimbali.

Ufanisi katika Usimamizi wa Serikali: Ana mtindo wa kuwa na nidhamu katika usimamizi wa serikali. Anajitahidi kuhakikisha kwamba sera na mipango ya serikali inaendana na malengo ya kitaifa, na pia anajitahidi kusimamia utawala bora kwa kutekeleza sheria na taratibu.

Mtindo wa Uongozi wa Amani na Kujenga Umoja: Rais Samia amekazia zaidi ushirikiano, amani, na mshikamano. Ametoa msukumo kwa ushirikiano wa kitaifa, na amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kudumisha umoja miongoni mwa Watanzania. Hii ni muhimu katika kuimarisha uthabiti wa kisiasa na kiuchumi.

Uongozi wa Kiutendaji na Ufanisi: Rais Samia ni kiongozi anayesisitiza utekelezaji wa ahadi na mipango ya serikali. Hata ingawa alikuta hali ya kiuchumi na changamoto za kijamii, ameonesha juhudi za kuleta mabadiliko ya kisera na kuhamasisha maendeleo ya sekta muhimu kama vile miundombinu, afya, elimu, na kilimo.

Uvumilivu na Uelewa wa Masuala ya Kimataifa: Rais Samia amekuwa na msimamo thabiti katika siasa za kimataifa, akiwa mstari wa mbele katika uhusiano na mataifa ya Afrika na ulimwengu kwa jumla. Amejenga uhusiano mzuri na nchi za kigeni, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo.

Kujitolea kwa Maendeleo ya Wanawake na Vijana: Rais Samia amekuwa mtetezi wa haki za wanawake na amekuwa akifanya juhudi kubwa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika nyanja mbalimbali za jamii, ikiwa ni pamoja na siasa, uchumi, na maendeleo. Pia, ameonyesha kujali maendeleo ya vijana, hasa katika kutoa fursa za ajira na elimu.

Kukabiliana na Changamoto za Kiuchumi: Katika kipindi chake cha uongozi, Rais Samia amekutana na changamoto za kiuchumi, hasa kutokana na athari za janga la COVID-19 na mabadiliko ya tabia nchi. Hata hivyo, amekuwa akifanya juhudi za kurekebisha hali ya uchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo na kuvutia wawekezaji.

Mtindo wa Uongozi wa Rais Samia:

Uongozi wa Kidiplomasia na Mazungumzo
: Rais Samia ana mtindo wa kuzingatia mazungumzo na kujenga makubaliano kati ya pande mbalimbali. Hii inajidhihirisha katika namna anavyoshirikiana na vyama vya upinzani, serikali za mitaa, na mashirika ya kiraia. Anaamini kwamba mazungumzo na majadiliano ni njia bora ya kutatua migogoro na changamoto.

Uongozi wa Kujenga Msingi wa Maendeleo Endelevu: Samia anasisitiza umuhimu wa maendeleo endelevu na mazingira bora kwa kizazi kijacho. Anaona umuhimu wa kuwekeza katika sekta za afya, elimu, na miundombinu, na pia ameweka mkazo katika kuboresha sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na kipato cha wananchi.

Tija na Ufanisi katika Serikali: Katika mtindo wake wa uongozi, Rais Samia anazingatia ufanisi wa utendaji kazi serikalini. Hii inajidhihirisha katika juhudi za kuimarisha mifumo ya serikali na kupunguza urasimu. Anajitahidi kuondoa vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kusikiliza na Kuelewa: Rais Samia pia ni kiongozi anayeweza kusikiliza maoni ya watu wake na kujitahidi kutatua changamoto zao. Hii ni muhimu katika kukuza uaminifu na kuongeza ushirikiano kutoka kwa wananchi.
 
Habari wakuu! Kiukweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama samia serikali yake ndani ya miaka mitano niipongeze kwa kutoa ajira nyingi kuliko awamu nyingine yoyote kwenye sekta mbalimbali! Kila siku utumishi wanaita watu kazini kwa kweli mama nampongeza mno kwenye hili!

Kuna baadhi ya taasisi ilikuwa ni vigumu kuona ajira zake zikitoka kwenye awamu zingine lakini awamu hii tunashuhudia zikitangazwa na vijana wengi wameajiriwa

Niipongeze pia sekretariati ya ajira kwa kuleta usawa kwenye soko la ajira maana leo ni kawaida kuona mtoto wa mlala hoi yupo BOT, TPA, TRA nk tofauti na zamani!

Note: kuna watu wamekariri kuwa ajira ni walimu pekee na afya( akili mgando) hapa nazungumzia ajira kwa ujumla mama kajitahidi sana na kwa hili vijana tunampongeza!
 
wewe Poyoyo Samia hamiliki serikali, acha upumbavu wako. Hapa ndio wengi mnapotea, how comes una address serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kama serikali ya Samia? Samia, Mimi na wewe na wengine serikali zetu ziko kwenye familia zetu, full stop. Kamwe huwezi kusikia Wakenya wakitamka huu upumbavu
 
Habari wakuu! Kiukweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama samia serikali yake ndani ya miaka mitano niipongeze kwa kutoa ajira nyingi kuliko awamu nyingine yoyote kwenye sekta mbalimbali! Kila siku utumishi wanaita watu kazini kwa kweli mama nampongeza mno kwenye hili!

Kuna baadhi ya taasisi ilikuwa ni vigumu kuona ajira zake zikitoka kwenye awamu zingine lakini awamu hii tunashuhudia zikitangazwa na vijana wengi wameajiriwa

Niipongeze pia sekretariati ya ajira kwa kuleta usawa kwenye soko la ajira maana leo ni kawaida kuona mtoto wa mlala hoi yupo BOT, TPA, TRA nk tofauti na zamani!

Note: kuna watu wamekariri kuwa ajira ni walimu pekee na afya( akili mgando) hapa nazungumzia ajira kwa ujumla mama kajitahidi sana na kwa hili vijana tunampongeza!
Haya baada ya pongezi, ingia sasa mtaani ili ukapambane na hali yako.
 
Back
Top Bottom