Maoni yangu kuhusu Suluhisho la Msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Nimeona jitihada zinazofanywa na wadau katika siku za hivi karibuni kutafuta suluhisho la tatizo sugu la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ikiwemo hatua ya kufunga kamera za ufuatiliaji barabarani.

Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, matumizi ya kamera hayawezi kuondoa tatizo la foleni kwa kiwango kikubwa; huenda mchango wake ukawa chini ya asilimia 2.

Mapendekezo ya Suluhisho la Kudumu:
  1. Uboreshaji wa Barabara za Mitaa:
    Barabara zote za mitaani zipaswe kuwekwa lami na ziwe katika hali nzuri ili zitoe njia mbadala kwa watumiaji wa barabara kuu. Kwa sasa, njia nyingi za pembezoni hazipitiki kwa sababu ya uharibifu mkubwa kama mashimo na makorongo. Kwa hiyo madereva wanahofia kupita huko.
  2. Uboreshaji wa Usafirishaji wa Mizigo:
    Ni muhimu kuhakikisha Bandari Kavu ya Kwala inaanza kutumika mapema na mizigo isafirishwe kwenda huko Kwala kwa treni badala ya malori kuingia jijini. Malori yanayoruhusiwa kuingia Dar es Salaam yawe ni yale tu yenye mizigo ya dharura, nayo yaingie usiku kuanzia saa 4:00 usiku na yatoke kabla ya alfajiri.
  3. Uhamishaji wa Dry Ports kutoka Mjini:
    Maghala (dry ports) ya kibinafsi yaliyopo maeneo ya mjini, hasa yale yaliyo karibu na barabara kuu kama kituo cha MCL kilichopo Tabata relini, yafaa yahamishwe kwenda maeneo ya nje ya jiji ili kupunguza msongamano wa magari makubwa katikati ya mji. Kwa mnaopita hapo mtakubaliana kwamba malori yanapaki main road pale kwa masaa mengi na kusababisha foleni Mandela road.
  4. Uboreshaji wa Usafiri wa Umma:
    Mabasi ya mwendokasi yaanzishe huduma kikamilifu na kwa kiwango kinachotosheleza mahitaji ya abiria. Daladala zote ziondolewe kwenye barabara kuu kama Morogoro Road, kwani nyingi hazina vituo rasmi na hupaki katikati ya barabara, jambo linalochangia foleni.
  5. Udhibiti wa Bajaj:
    Bajaj zipigwe marufuku kubeba abiria kwenye barabara kuu, kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mtiririko wa magari, hasa maeneo ya Morogoro Road. Hii i apply na Mbeya mjini.
 
6. Usafiri wa binafsi uwe discouraged kwa kuongeza/kupandisha packing fees
 
Suluhisho naloliona ni kuwa na barabara iliyoishia Kibaha(6 Lanes) ifike Chalinze.
Then, ziongezwe 2 kushoto na kulia, kila moja iwe ya njia 6. Mfano moja itokee Bagamoyo nyingine ijekutokea maeneo ya Temeke.
Hapo katikati ya hizo njia kuu 3 kuwe na muingiliano na barabara za njia 4 nyingi tu.
 
Nimeona jitihada zinazofanywa na wadau katika siku za hivi karibuni kutafuta suluhisho la tatizo sugu la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ikiwemo hatua ya kufunga kamera za ufuatiliaji barabarani.

Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, matumizi ya kamera hayawezi kuondoa tatizo la foleni kwa kiwango kikubwa; huenda mchango wake ukawa chini ya asilimia 2.

Mapendekezo ya Suluhisho la Kudumu:
  1. Uboreshaji wa Barabara za Mitaa:
    Barabara zote za mitaani zipaswe kuwekwa lami na ziwe katika hali nzuri ili zitoe njia mbadala kwa watumiaji wa barabara kuu. Kwa sasa, njia nyingi za pembezoni hazipitiki kwa sababu ya uharibifu mkubwa kama mashimo na makorongo. Kwa hiyo madereva wanahofia kupita huko.
  2. Uboreshaji wa Usafirishaji wa Mizigo:
    Ni muhimu kuhakikisha Bandari Kavu ya Kwala inaanza kutumika mapema na mizigo isafirishwe kwenda huko Kwala kwa treni badala ya malori kuingia jijini. Malori yanayoruhusiwa kuingia Dar es Salaam yawe ni yale tu yenye mizigo ya dharura, nayo yaingie usiku kuanzia saa 4:00 usiku na yatoke kabla ya alfajiri.
  3. Uhamishaji wa Dry Ports kutoka Mjini:
    Maghala (dry ports) ya kibinafsi yaliyopo maeneo ya mjini, hasa yale yaliyo karibu na barabara kuu kama kituo cha MCL kilichopo Tabata relini, yafaa yahamishwe kwenda maeneo ya nje ya jiji ili kupunguza msongamano wa magari makubwa katikati ya mji. Kwa mnaopita hapo mtakubaliana kwamba malori yanapaki main road pale kwa masaa mengi na kusababisha foleni Mandela road.
  4. Uboreshaji wa Usafiri wa Umma:
    Mabasi ya mwendokasi yaanzishe huduma kikamilifu na kwa kiwango kinachotosheleza mahitaji ya abiria. Daladala zote ziondolewe kwenye barabara kuu kama Morogoro Road, kwani nyingi hazina vituo rasmi na hupaki katikati ya barabara, jambo linalochangia foleni.
  5. Udhibiti wa Bajaj:
    Bajaj zipigwe marufuku kubeba abiria kwenye barabara kuu, kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mtiririko wa magari, hasa maeneo ya Morogoro Road. Hii i apply na Mbeya mjini.
hili ni tatizo la muda tu kwa sasa kuna juhudi kubwa sana zinafanywa na serikali,ndani ya miezi 3 ijayo litapungua kwa 90%
 
Kila ulichoandika ni sahihi kwa asilimia zote especially haya malori kuingia mjini. Huwezi kuona New York pale downtown Manhattan malori.
 
Malori yanaongeza foleni sana. Siku hizi hata Bagamoyo Road nayo ina Malori mengi tena yanapita wakati wa peak hours yanachangia ukali foleni, yaingie na kutoka mjini usiku kwa usiku, kwa yale tu yanayoleta mali mbichi...
 
Bajaji wanavurugu kuliko ata boda aisee
Ukienda Mwanjelwa Mbeya, Bajaj ni kero kubwa sana. Huwa najiuliza ina maana Mbeya jiji wameshindwa kuzifanya zitoe huduma pembezoni pekee mpaka zije katikati ya mji!? Mji umekuwa mchafu sababu ya Bajaj ambazo mbaya zaidi hasina mpangilio wala usimamizi wa kueleweka mixer stendi ya Kabwe kugeuzwa soko na maegesho ya magari binafsi!!

Kero nyingine ya Bajaj ni Morogoro Road hasa nyakati za jioni, wanapakilia abiria barabarani na kusababisha jam
 
Nimeona jitihada zinazofanywa na wadau katika siku za hivi karibuni kutafuta suluhisho la tatizo sugu la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ikiwemo hatua ya kufunga kamera za ufuatiliaji barabarani.

Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, matumizi ya kamera hayawezi kuondoa tatizo la foleni kwa kiwango kikubwa; huenda mchango wake ukawa chini ya asilimia 2.

Mapendekezo ya Suluhisho la Kudumu:
  1. Uboreshaji wa Barabara za Mitaa:
    Barabara zote za mitaani zipaswe kuwekwa lami na ziwe katika hali nzuri ili zitoe njia mbadala kwa watumiaji wa barabara kuu. Kwa sasa, njia nyingi za pembezoni hazipitiki kwa sababu ya uharibifu mkubwa kama mashimo na makorongo. Kwa hiyo madereva wanahofia kupita huko.
  2. Uboreshaji wa Usafirishaji wa Mizigo:
    Ni muhimu kuhakikisha Bandari Kavu ya Kwala inaanza kutumika mapema na mizigo isafirishwe kwenda huko Kwala kwa treni badala ya malori kuingia jijini. Malori yanayoruhusiwa kuingia Dar es Salaam yawe ni yale tu yenye mizigo ya dharura, nayo yaingie usiku kuanzia saa 4:00 usiku na yatoke kabla ya alfajiri.
  3. Uhamishaji wa Dry Ports kutoka Mjini:
    Maghala (dry ports) ya kibinafsi yaliyopo maeneo ya mjini, hasa yale yaliyo karibu na barabara kuu kama kituo cha MCL kilichopo Tabata relini, yafaa yahamishwe kwenda maeneo ya nje ya jiji ili kupunguza msongamano wa magari makubwa katikati ya mji. Kwa mnaopita hapo mtakubaliana kwamba malori yanapaki main road pale kwa masaa mengi na kusababisha foleni Mandela road.
  4. Uboreshaji wa Usafiri wa Umma:
    Mabasi ya mwendokasi yaanzishe huduma kikamilifu na kwa kiwango kinachotosheleza mahitaji ya abiria. Daladala zote ziondolewe kwenye barabara kuu kama Morogoro Road, kwani nyingi hazina vituo rasmi na hupaki katikati ya barabara, jambo linalochangia foleni.
  5. Udhibiti wa Bajaj:
    Bajaj zipigwe marufuku kubeba abiria kwenye barabara kuu, kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mtiririko wa magari, hasa maeneo ya Morogoro Road. Hii i apply na Mbeya mjini.
Magari ya bei rahisi kama vits na ist yathibitiwe kuingia Tanzania pia ushuru wa magari uongezwe kwa asilimia 200
 
Malori yataleta madhara muda si mrefu.
Haya yaingie usiku yapotee saa 12. Yarudi saa 4 asubuhi hadi saa 9 mchana
 
kabisa...yanasababisha foleni sana...suluhu yabebe mzigo kutokea bandari kavu nje ya jiji...yale ya bidhaa za chakula tu ndo yaingie town tena yaje usiku!
 
Sasa hivi yanakimbia foleni Mandela road yanapita katikati ya jiji. Unayakuta kariakoo. Hii ni hatari sana.
Mengine yamepaki ubungu maziwa. Kuna ajali fulani hivi itatokea muda si mrefu
 
Back
Top Bottom