N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Nimeona jitihada zinazofanywa na wadau katika siku za hivi karibuni kutafuta suluhisho la tatizo sugu la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ikiwemo hatua ya kufunga kamera za ufuatiliaji barabarani.
Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, matumizi ya kamera hayawezi kuondoa tatizo la foleni kwa kiwango kikubwa; huenda mchango wake ukawa chini ya asilimia 2.
Mapendekezo ya Suluhisho la Kudumu:
Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, matumizi ya kamera hayawezi kuondoa tatizo la foleni kwa kiwango kikubwa; huenda mchango wake ukawa chini ya asilimia 2.
Mapendekezo ya Suluhisho la Kudumu:
- Uboreshaji wa Barabara za Mitaa:
Barabara zote za mitaani zipaswe kuwekwa lami na ziwe katika hali nzuri ili zitoe njia mbadala kwa watumiaji wa barabara kuu. Kwa sasa, njia nyingi za pembezoni hazipitiki kwa sababu ya uharibifu mkubwa kama mashimo na makorongo. Kwa hiyo madereva wanahofia kupita huko. - Uboreshaji wa Usafirishaji wa Mizigo:
Ni muhimu kuhakikisha Bandari Kavu ya Kwala inaanza kutumika mapema na mizigo isafirishwe kwenda huko Kwala kwa treni badala ya malori kuingia jijini. Malori yanayoruhusiwa kuingia Dar es Salaam yawe ni yale tu yenye mizigo ya dharura, nayo yaingie usiku kuanzia saa 4:00 usiku na yatoke kabla ya alfajiri. - Uhamishaji wa Dry Ports kutoka Mjini:
Maghala (dry ports) ya kibinafsi yaliyopo maeneo ya mjini, hasa yale yaliyo karibu na barabara kuu kama kituo cha MCL kilichopo Tabata relini, yafaa yahamishwe kwenda maeneo ya nje ya jiji ili kupunguza msongamano wa magari makubwa katikati ya mji. Kwa mnaopita hapo mtakubaliana kwamba malori yanapaki main road pale kwa masaa mengi na kusababisha foleni Mandela road. - Uboreshaji wa Usafiri wa Umma:
Mabasi ya mwendokasi yaanzishe huduma kikamilifu na kwa kiwango kinachotosheleza mahitaji ya abiria. Daladala zote ziondolewe kwenye barabara kuu kama Morogoro Road, kwani nyingi hazina vituo rasmi na hupaki katikati ya barabara, jambo linalochangia foleni. - Udhibiti wa Bajaj:
Bajaj zipigwe marufuku kubeba abiria kwenye barabara kuu, kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mtiririko wa magari, hasa maeneo ya Morogoro Road. Hii i apply na Mbeya mjini.