Nimepitia mijadala kadhaa ya vijana mbali mbali nimeona Tatizo ama lipo katika syllabus tunayotumia kuwafundishia masuala ya kidipomasia ya mataifa mbali mbali ,vijana wengi sana hawana ufahamu Kabisa , vita wanaijadili kama Mpira kwamba yeyote anaweza kupigwa, Vita inajadiliwa kama hadithi za abunuasi , vita imejadiliwa Kwa mzaha sana , watu wanakurupuka tu humu,kwanza nataka mjue Urusi iko vizuri sana kijeshi tena kwenye rank za kidunia yupo namba mbili nyuma ya Marekani , lakini leo hii akiingia vitani hata na China ambaye yuko namba tatu atapigwa kwasababu ya uchumi wake mdogo, vita ni bajet yako kijeshi unavyo wekeza kwenye technology ya silaha na udadisi (intelligence). Na Muda katika kupigana vita ya mataifa makubwa hauwi week moja Au mbili ni miezi zaidi ya minne mpaka saba! Hapa lazima uwe vizuri kiuchumi ili uweze kuendesha mambo yote mawili Kwa wakati mmoja , Yaan vita iendelee huku shughuli zako za kiuchumi zisikwame!
Vijana tumekosa kujisomea maandiko mbali mbali na kudadis kupitia makala na scientific research mbali mbali .
Kuna comments moja niliiona sehemu kijana anasema eti alisema ''China itategea kipindi ambacho US ametingwa na uvamizi fulani wa nchi kubwa nyingine, alafu yeye ndo atatumia muda huo kuivamia Taiwan na ataichukua kwasababu kwasasa China yupo mbali sana kijeshi''
Nilimuelewesha mambo mengi sana akaonekana kukubaliana namimi,
Hata hapa JamiiForums sikuwa Mwanachama Nina miezi Kama minne ninejiunga ila napitia masuala kadhaa ya wachambuzi wa siasa zetu Kama kijana Au Mdogo wangu Pascal Mayalla ana makala nyingi sana hapa JamiiForums Kama wangekuwa wanawalipa wana makala basi angepata namba kuna wengine Kama Kiranga Kalamu1 Mag3 sijaona wakichambua masuala haya ya kimataifa na ningetegemea kuona mtizamo wao katika haya
Basi nawaambia kwamba
Watu wanaibeza sana US katika nyanja za vita, US hawana gwaride kuonyesha vifaa vyao ila vita vikianza utaona mengi ambayo macho hayajawahi kuona... Au Kama inafanyika inafanyika katika namna ambayo ni Siri sana !
Pia hatupaswi kuipuuza Urusi katika nyanja za kijeshi, lakini ni upuuzi kudhani Urusi inaweza mess up na Washington na Moscow ikabaki kama ilivyo... tunakosea sana! Hakuna Muungano ulikuwa unatisha kama USSR wadogo ninyi wengi humu !
Hakuna Taifa lilikuwa linatisha Kama Iraq ya Sadam Hussein! Au UMOJA wa waarabu chini ya Sadath wa Misiri. Lakin walikwama sehemu moja tu intelligence na uchumi…
Us kwa uchumi wake na teknolojia lazima Urusi itakuwa katika hali ngumu Kwa Urusi kusema iingie vitani nayo ibaki salama!!
Hata Asia ina safari ndefu kujifunza kutoka America na Ulaya kuanzia military technology,
Nitaendelea kwanini tunapaswa Kukataa vita! Maana nilivyoandika hapa kuna watakaosema natetea maovu Au vamizi za US kwingine Hapana nakemea sana kama nilivyokemea Afghanistan, LIBYA na sasa Nakemea Uvamizi wa Urusi Kwa Ukraine!!
Mimi Dr. Lwaitama