Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wewe ni kilaza swala ni Ukraine vs Urusi sio Urusi vs hao wasamalia wema wa Ukraine wew unawaita washirika sijui kwa mkabata ipi ?Mkuu, kwa bahati mbaya au nzuri nilipofungua tu, nikaona hiyo mistari hapo niliyokwoti kabla sijaenda kule juu. Nikasema ngoja nimalizane na hili kwanza.
Hakuna asiyekemea uvamizi wa nchi yoyote juu ya nyingine, hasa ukiwa ni uvamizi wa kuonea tu, au kwa maslahi ya pembeni zaidi yasiyohatarisha nchi inayoivamia nyingine
Lakini inabidi pia uangalie kwa makini sana tatizo lililopo hapa kati ya Urusi na washirika wa nchi iliyovamiwa.
Ni hivi: ni kama ile vita baridi ilikuwa bado haijaisha. Hawa jamaa wa magharibi ni kama walijikuta kama vile kuna kitu hawakukimalizia kabisa ili roho zao zitulie. Urusi yenye nguvu, hata kama imejiunga katika mfumo huo huo wa kidunia unaohimizwa na hawa walioshinda vita ya baridi, bado haiwapi utulivu juu ya Urusi yenye nguvu katika eneo hilo la Ulaya.
Bado hawa wakubwa wa Ulaya, wakiongozwa na mkuu wao, wanakuwa na wasiwasi na hili li-nchi kubwa la Urusi lenye nguvu, na ambalo pamoja na lenyewe kukubali kuendesha shughuli zake kama zinavyoendeshwa huko Magharibi, bado hawana utulivu wa moyo juu yake (kuhusu usalama wao, baadae, sijui?); lakini wanaliogopa sana li-nchi hili.
Zaidi ya hayo, huyu mkubwa kabisa aliyebaki kama kinara wa dunia, hata yeye hataki hadhi yake hiyo itiliwe mashaka. Isihojiwe na yeyote awaye. Akikataa jambo, kila mtu aingie mstarini. Ni hulka ya kibinaadam hiyo. Ususi yenye nguvu kila mara itakuwa upande wa pili. Unaikumbuka ilivyokuwa Syria? Au hukufuatilia sinema hiyo.
Nisiende mbali sana na jambo hili, lakini wewe jiulize. Vita Baridi wamekwishashinda. Mpinzani wao mkuu amekwishasambaratika. Kuna haja gani tena ya kwenda kumbanabana kwa kujitanua mpaka mlangoni kwake? Anawaomba 'guarantee' ya usalama wake, mnamzungusha kiujanjaujanja na uongo mwingi.
Jamaa kaweka mstari mwekundu chini, usiuvuke, wao wanadhani anatania!
Halafu ona sasa wanavyozidi kumchochea huyu kibaraka waliyemtoa kama sadaka. Watu wake wanaumizwa, wao wanazidi kuchochea kuni hao watu waumizwe zaidi kwa kutoa silaha na kumpa matumaini kibaraka yasiyokuwepo, kiasi kwamba hata mazungumzo ya kusitisha vita anakuwa hana msimamo wake thabiti wa kuwahurumia raia zake.
Mrusi anapigania usalama wake. Wanambanabana hadi wamtoe roho? Walijaribu kuihadaa Chrchinia, wakakwama, sasa wanatafuta njia za kuendelea kulegeza mrusi kwa wasiwasi wao tu usiokuwa na msingi.
Ni hayo tu mkuu, ngoja nikasome huko juu.
Unapopinga kichwa chako kisiwe referenceDr..pamoja kwamba uelewa wangu mdogo kwenye maswala vita,lakini hapa unanipa shaka kidogo juu ya uwelewa wako kuhusu haya mataifa km Urusi na Marekani kwenye nguvu za kijeshi walizonazo,kwa sababu ikitokea wakubwa hawa wakaingia vitani sidhani km vita hii itachukua zaidi ya week moja bila kupata majibu ya nan kashinda na nani ameshindwa..kwani tusitegemee kuona Ak 47 wala wanajeshi wa jeshi Fulani kuingia sehem fulan,hapa tutegemee kuona ulimwengu unafunikwa na Giza zito na madhara yake itakuwa hadithi ambayo haikuwahi kutokea kabla..kwahiyo swala la nchi kuwa na uchumi mdogo au mkubwa halina nafasi hapo.