Mkuu, kwa bahati mbaya au nzuri nilipofungua tu, nikaona hiyo mistari hapo niliyokwoti kabla sijaenda kule juu. Nikasema ngoja nimalizane na hili kwanza.
Hakuna asiyekemea uvamizi wa nchi yoyote juu ya nyingine, hasa ukiwa ni uvamizi wa kuonea tu, au kwa maslahi ya pembeni zaidi yasiyohatarisha nchi inayoivamia nyingine
Lakini inabidi pia uangalie kwa makini sana tatizo lililopo hapa kati ya Urusi na washirika wa nchi iliyovamiwa.
Ni hivi: ni kama ile vita baridi ilikuwa bado haijaisha. Hawa jamaa wa magharibi ni kama walijikuta kama vile kuna kitu hawakukimalizia kabisa ili roho zao zitulie. Urusi yenye nguvu, hata kama imejiunga katika mfumo huo huo wa kidunia unaohimizwa na hawa walioshinda vita ya baridi, bado haiwapi utulivu juu ya Urusi yenye nguvu katika eneo hilo la Ulaya.
Bado hawa wakubwa wa Ulaya, wakiongozwa na mkuu wao, wanakuwa na wasiwasi na hili li-nchi kubwa la Urusi lenye nguvu, na ambalo pamoja na lenyewe kukubali kuendesha shughuli zake kama zinavyoendeshwa huko Magharibi, bado hawana utulivu wa moyo juu yake (kuhusu usalama wao, baadae, sijui?); lakini wanaliogopa sana li-nchi hili.
Zaidi ya hayo, huyu mkubwa kabisa aliyebaki kama kinara wa dunia, hata yeye hataki hadhi yake hiyo itiliwe mashaka. Isihojiwe na yeyote awaye. Akikataa jambo, kila mtu aingie mstarini. Ni hulka ya kibinaadam hiyo. Ususi yenye nguvu kila mara itakuwa upande wa pili. Unaikumbuka ilivyokuwa Syria? Au hukufuatilia sinema hiyo.
Nisiende mbali sana na jambo hili, lakini wewe jiulize. Vita Baridi wamekwishashinda. Mpinzani wao mkuu amekwishasambaratika. Kuna haja gani tena ya kwenda kumbanabana kwa kujitanua mpaka mlangoni kwake? Anawaomba 'guarantee' ya usalama wake, mnamzungusha kiujanjaujanja na uongo mwingi.
Jamaa kaweka mstari mwekundu chini, usiuvuke, wao wanadhani anatania!
Halafu ona sasa wanavyozidi kumchochea huyu kibaraka waliyemtoa kama sadaka. Watu wake wanaumizwa, wao wanazidi kuchochea kuni hao watu waumizwe zaidi kwa kutoa silaha na kumpa matumaini kibaraka yasiyokuwepo, kiasi kwamba hata mazungumzo ya kusitisha vita anakuwa hana msimamo wake thabiti wa kuwahurumia raia zake.
Mrusi anapigania usalama wake. Wanambanabana hadi wamtoe roho? Walijaribu kuihadaa Chrchinia, wakakwama, sasa wanatafuta njia za kuendelea kulegeza mrusi kwa wasiwasi wao tu usiokuwa na msingi.
Ni hayo tu mkuu, ngoja nikasome huko juu.