Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Hivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!


Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.

Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.

Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo

Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024

View attachment 2927199

Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
Another bitter proof kuwa asilimia kubwa ya warembo wana mkaa kichwani badala ya akili
 
Hii ndio maana halisi kwamba elimu ya chuo kikuu haiwasaidii vijana wa kitanzania hawana uwezo wa kuona hatari mtu kama huyu anaweza kutunza siri za nchi kweli!?

Ushuzi wa bata kabisa hawa
Unaweza kukuta elimu hii hii tunayoidharau ndiyo hawa mapacha wameitumia vizuri na kuona loopholes za kisheria na kisha kucheza na akili za watu ili kutrend na hatimaye kufikia lengo lao wanalolijua wenyewe. Sidhani kwamba wameongea hivyo bila kujua legal implication na pia repercussion yake kwa ujumla kwenye jamii na mstakabali mzima wa maisha yao.
 
Back
Top Bottom