Hapana degree hata kama umejiajiri hujui utaitumia lini elimu maana yake inakupa wide options unaweza usiitumie leo kuna siku itakufaa tofauti na mtu asiyesomaWatu wenyewe wamejiajiri!
Hata wakinyang'anywa hawata pungukiwa na kitu!
HIZO NI FIKRA ZANGU TU!
Itabidi waseme tu hivyoWatakapohojiwa wanaweza kusema walitania tu kwa kuwa radio yenyewe ni ya udaku
Hapo ndio pagumu. [emoji3][emoji3][emoji3]Chuo kitawezaje kuthibitisha hili?
Katika sheria lazima kuwe na ushahidi wa bila shaka,kama nilivyokuambia lazima watajitetea.Kuna kuunganisha dots, kama kweli mmoja alipata supplementary kwenye mtihani tajwa na alipifanya akafaulu, huu nao ni ushahidi tosha dhidi ya kesi yao.
Hakiwezi labda wawe wajinga kwani hizo si ni story kama story nyingne tuuChuo kitawezaje kuthibitisha hili?
Hakuna kesi hapa.Maana hakuna ushahidi.Wanasheria wa Law school watoe statement.. kuna kesi hapo?
Kama wataamua kuwa serious kufatilia hili wataangalia mpaka miandiko yao.Hapo ndio ngoma. watathibitishaje huo uchunguzi wao?
Hand writing itawaumbua kweupe.Chuo kitawezaje kuthibitisha hili?
Hao ni mapacha ambao wanafanana sura sidhani kama miandiko yao inafanana pia. Wakitaka kutrace kwa mwandiko kama haifanani watakamatika tu.Ni ngumu kudhibitisha,un less chuo wa vidéo za CCTV. Halafu hao mapacha si wapumbavu,watajibu si kweli na walikuwa wanapamba content tu ili kuvuta hisia za watu.
Another bitter proof kuwa asilimia kubwa ya warembo wana mkaa kichwani badala ya akiliHivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!
Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.
Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.
Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo
Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024
View attachment 2927199
Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
ndio ilivyo mkuu kutojua nini cha kuongea kwa wakati gani na mazingira yapi inawagharimu watu wengiIla watu bhana maneno yako mwenyew yanakufunga mwenyew
Unatania kwenye media jambo serious kama hilo, hapo chuo ishabeba ushahidi tayari.Watakapohojiwa wanaweza kusema walitania tu kwa kuwa radio yenyewe ni ya udaku
Kupitia kauli yaoHapo ndio ngoma. watathibitishaje huo uchunguzi wao?
Unaweza kukuta elimu hii hii tunayoidharau ndiyo hawa mapacha wameitumia vizuri na kuona loopholes za kisheria na kisha kucheza na akili za watu ili kutrend na hatimaye kufikia lengo lao wanalolijua wenyewe. Sidhani kwamba wameongea hivyo bila kujua legal implication na pia repercussion yake kwa ujumla kwenye jamii na mstakabali mzima wa maisha yao.Hii ndio maana halisi kwamba elimu ya chuo kikuu haiwasaidii vijana wa kitanzania hawana uwezo wa kuona hatari mtu kama huyu anaweza kutunza siri za nchi kweli!?
Ushuzi wa bata kabisa hawa
Yani kama nawaona wanavyo tetema kama Mayele muda huu yani wanajuta hakikaHao ni mapacha ambao wanafanana sura sidhani kama miandiko yao inafanana pia. Wakitaka kutrace kwa mwandiko kama haifanani watakamatika tu.