#COVID19 Mapambano dhidi ya COVID-19: Rais Samia anayo dhamira ya kweli? Kinachoendelea India kinatisha

#COVID19 Mapambano dhidi ya COVID-19: Rais Samia anayo dhamira ya kweli? Kinachoendelea India kinatisha

Naam,ndo maana watanzania wengi wamepukutika sana, inakadiriwa kuwa takribani watanzania milioni 36 wamekwenda kwa korona.
Kwa hiyo hao milioni 36 ndo wabishi? Point yako ni; corona haiui sana! Basi tuseme hajafa hata Mtanzania mmoja ili kila mmoja akaye na extreme yake!
 
Inatisha kidogo kuona mikutano mingi ya futari ambako wanabanana karibu, tena bila barakoa. Kama virusi vipya vimeshafika, tutaona matokeo mabaya karibuni. -- Maana Iran wanategeneza sasa makaburi mfululizo baada ya sherehe yao ya Nowruzi walipokutana wengi ,Uhindi wanakosa kuni ya kuchoma maiti baada ya sikukuu kubwa yenye umati mkubwa wa watu na pia mikutano ya kampeni za kisiasa......
1619867960241.png

Leo hii: Kuandaa makaburi mapya mjini Tehran (In Iran, a massive cemetery struggles to keep up with COVID-19)

1619868099850.png

Multiple funeral pyres of those who died of COVID-19 burn at a ground that has been converted into a crematorium for the mass cremation of coronavirus victims, in New Delhi, India, Saturday, April 24, 2021. © AP Photo/Altaf Qadri
 
Kwa hiyo hao milioni 36 ndo wabishi? Point yako ni; corona haiui sana! Basi tuseme hajafa hata Mtanzania mmoja ili kila mmoja akaye na extreme yake!
Elimu gani? Kweli Covid haiui kama Ebola, lakini inaambukiza wengi zaidi. Hata kama asilimia ya wagonjwa wanaokufa ni ndogo zaidi, kama idadi ya wagonjwa ni kubwa , idadi ya wanaokufa inaongezeka.

Tanzania imebahatika hadi sasa kwa sababu sehemu kubwa ya maisha iko nje, na watu wengi hawaishi nyumba penye madirisha ya kioo inayotunza hewa ndani. Lakini India ilikuwa vile, sasa wamepata virusi vilivyobadilika . . .
 
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

View attachment 1769853
 
Mkuu naungana na wewe kuhusu hili,Mama kama hajijali basi ajue yeye Raia namba moja, jambo lolote kuhusu yeye ni lenye maslahi mapana kwa Taifa.

Hivi hawaoni wazee wanampa ishara, wote wanavaa barakoa kwenye shughuli au anataka mpaka wamwambie kwa mdomo aseme wanawashwa.
Nimeota kuwa mchizi Covid anavuta tena mmoja hapo juu muda mfupi kutokea leo.
 
Elimu gani? Kweli Covid haiui kama Ebola, lakini inaambukiza wengi zaidi. Hata kama asilimia ya wagonjwa wanaokufa ni ndogo zaidi, kama idadi ya wagonjwa ni kubwa , idadi ya wanaokufa inaongezeka.

Tanzania imebahatika hadi sasa kwa sababu sehemu kubwa ya maisha iko nje, na watu wengi hawaishi nyumba penye madirisha ya kioo inayotunza hewa ndani. Lakini India ilikuwa vile, sasa wamepata virusi vilivyobadilika . . .
Jamaa wanaishi ndotoni ni imani zao za giza! Corona ipo na inaua!
 
Kila mtu alimuona Mpango alivyokuwa anakohoa siku ile amefanya press conference baada ya kutoka hospital; huyu bwana aliponea chupu chupu lakini hata baada ya kupona corona bado havai barakoa wala hakai mbali na wenzie to social distance!! Hii ni hatari sana hasa kwa viongozi wenzie anaokutana nao kila siku!! Try to social distance, hata hao walinzi wa Rais pia wajitahidi kukaa mbali ,sometimes wanaonekana kuwa karibu sana na Rais na haijulikani wanakolala!!!
kigogo ndio aliwaambia mipango anaumwa corona,jpm kafa kwa corona,kijazi pia ila akasahau kwamba viongozi waliokuwa karibu na hao hawajachanjwa wangechukua tahadhali tu.
 
Tushazoea kuishi nayo. Vyombo vya Habari vimereport kuhusu variant mpya kutoka Tz, lkn maisha yanakwenda. Tulioko Tz hatuna hofu kabisa.
 
Naona Museveni amezuia ndege kutoka India zisiingie Uganda!
Amekwisha chelewa, juzi hapa nilisoma sehemu Waziri wa afya wa Uganda akiwasihi Indian Community nchini Uganda kwamba wawafichue Wahindi wanao ingia nchini Uganda wakitokea Nchini India hivi karibuni ili wawe Isolated kwa lengo la kuchunguzwa hali zao za kiafya!!

Sasa siijuwi hapa kwetu ili suala hatarishi la kutoka India wanalichukuliaje? Serikali yetu hisifanye hajizi Covid variant ya India ikiingia hapa kwetu tutapukutika kama majani ya miti wakati wa majira ya Autum.
 
Wasukuma muacheni mama afanye kazi, nyi rais wenu ameshakufa, na Wala mlikuwa hamumwambii kuwa achukue tahadhali juu ya covid19, hadi ilipompitia ye mwenyewe,....
Kwani Magu alitutangazia kwamba anaunda kamati ya corona?
 
Kuunda kamati ya kuchunguza uwepo wa Corona na kama chanjo zinafanya kazi ni jibu tosha. Tanzania hamna Corona.

Amandla...
Hamna corona kwa mujibu wa nini/ nani? Kamati ya corona?

Hivi wajumbe wa hiyo kamati ni akina nani? We Fundi Mchundo upo kwenye hiyo kamati?
 
Hamna corona kwa mujibu wa nini/ nani? Kamati ya corona?

Hivi wajumbe wa hiyo kamati ni akina nani? We Fundi Mchundo upo kwenye hiyo kamati?
Shida manyani hamuombi. Sisi tumeomba ndio maana Corona imetuogopa.
Mafundi Mchundo hatumo kwenye hiyo kamati. Mambo yote ni hush hush.

Amandla...
 
Sasa kamati ya Samia ya nini?
Hakuna covid, ila kuna watu wanataka kulazimisha irejee kwa kuanza kupandikiza hofu. Japo wanaona aibu kwenda moja kwa moja hivyo wanajificha nyuma ya dude kamati.

Unpopular comment: Hizo zinazoitwa tahadhari; social distancing, barakoa na sijui kunawa mikono ndivyo vyanzo vyenyewe vya hofu.

Tuache kuwa robots. Tuziruhusu bongo zetu kufikiria. Virusi vikiingia huwa kila mahali; ardhini na hewani. Distancing kwa mfano manufaa yake ni madogo kuliko madhara yake hasi (kuzidi kupandikiza hofu).

Kwa kifupi tumekwisha kujua namna ya kuishi na corona. Siyo kazi kutumia mchanganiko wa vyakula tiba kama vitunguu maji & swaumu, tangawizi, pilipili, malimao nk ambavyo kimsingi ndivyo vimetuvusha walau mara 2 au tatu kwa wiki.

Siyo kazi pia kuanza program za mazoezi mepesi kama kukimbia au kuruka kichura mara 3 kwa wiki. Tusikae tu kama gadgets kufikiri kuwa yale mambo yanayopigiwa chapuo na ulimwengu (ambao umefeli kwenye hili suala) kuwa ndilo suluhisho sahihi.
 
Sasa kamati ya Samia ya nini?
Hiyo ni mitazamo yake ya kiutandawazi kuwa corona ipo kwa kuwa tu hatukutumia mbinu "rasmi" kukabiliana nayo. Bali kwa mkazi yeyote wa Tanzania kwa sasa aliye timamu, hakuna corona.
 
Rais Samia alisema keshaunda kamati ya corona!

Hiyo kamati ndo imemshauri haya mambo ya mikusanyiko ya watu wengi hivi iendelee?

She is not serious about!

Naona alisema kaunda hiyo kamati kuwaridhisha tu baadhi ya watu.

Maana haiingii akilini kabisa…
Kwani mkuu, kisaikolojia unadhani ni nini kinaongeza hofu? Kuzuia mikusanyiko au kuiruhusu, katika wakati kama huu ambapo ni ngumu kumpata mgonjwa wa covid?
 
Mungu wa mbinguni wewe humuamini sis tunamuamini na tunamuishi, ndiyo maana majaribio yote yanashinwa. Mungu akisimama wewe si chochote
Wapo walioishi kwa imani uliyonayo na leo wamebadilika au kwa kulazimisha ama kwa kuadhibiwa.
 
Sasa kwa nini aliunda kamati ya corona?Au ni mwanya na fursa ya kupiga hela?
Kamati imeundwa tayari? Huyu alisema “anakusudia” kuunda Tume. Saying ain’t doing

Labda ameshauriwa otherwise na wahafidhina aliowakuta huko ndani
 
Back
Top Bottom