Mapato ya Filamu ya Royal Tour kule AMAZON ni kufuru, kuingizia Tanzania zaidi ya TZS 1.5 Trilioni kwa mwaka

hao 175 milion customer wa Amazon hata 1% hawataangalia hiyo movie, Amazon kuna movie zaidi ya laki moja na ukipata view laki moja una bahati
Duuuh, Wewe ndio msemaji wao? 😅😅
 
Umesema imegharamiwa na serikali ya Tanzania kwa 100% hapo hapo unasema imegharamiwa na wadau wa mandeleo.
Hii filamu haijatumia thumni ya serikali ya TZ kwa hiyo tusianze ujinga wa kujitapa.
Lengo la filamu lilikuwa nini? Tuanzie hapo kwanza
 
Kuliingizia Taifa mapato ndio lengo la filamu
 
Iko hivi,

Sote tunafahamu, Filamu ya Royal Tour ni mali ya Watanzania kwa 100%

Tanzania imeigharamia filamu hii tangu kurekodiwa kwake mpaka kuzinduliwa kwake huko Marekani,

Inakadiriwa mpaka kukamilika kwa uzinduzi wa filamu hii imetumia zaidi ya TZS 7.2BL fedha toka kwa wadau wa maendeleo endelevu,

Nimeona kiongozi wa CHADEMA anayeishi Ughaibuni Mhe Tundu Lissu amehoji hii kwenye ukurasa wake wa Tweeter akitaka kujua pesa toka Mtandao wa AMAZONI ni mali ya nani?

Kwakuwa Tanzania ni mmiliki halali wa "Tanzania Royal Tour Film " mapato yote yatokanayo na filamu hiyo pia ni mali ya Watanzania ukiondoa gharama za Uendeshaji kule Amazoni,

Mtakumbuka AMAZONI inajumla ya Watazamaji na wanunuzi|wakodiji 175M kwa mwaka,

Gharama ya kukodi tu yaani kuangalia na kuondoka ni US$ 5.99 karibu TZS 15,000,

Wakati huo huo gharama za kuinunua video hiyo ni US$ 19.99 au TZS 46,000,

Kwakuwa Amazon inawanunuzi na wakodiji 157M Wa video zake kwa mwaka,

Hebu tukadirie filamu yetu ya Royal Tour ikodiwe tu na watu 100M kwa mwaka au kwa miaka,

Hii ni sawa na kusema

Chukua hawa wakodiji 100M zidisha kwa elfu 15 utapata jumla ya TZS 1,500,000,000,000 yaani TZS 1.5Trilioni ,

Kumbukeni hii ni pesa toka AMAZONI tu sio Utalii,

Ili kuweka rekodi sawa haya mapato ya TZS 1.5Trilioni ni kwaajili ya kukodi tu achilia mbali yale ya kununua sijayaweka hapa,

Lazima tukubali Rais Samia Suluhu Hassan ni akili kubwa sana na huenda itatuchukua miaka mingi sana kumpata mtu mwingine kama yeye,

Sasa Tanzania huenda ikapata jumla ya zaidi ya TZS 1.5Trilioni toka Amazon kama mauzo ya Filamu yetu ya Royal Tour kila mwaka bila kuhesabu faida kubwa ya Utalii tuliyoilenga,

Wenye masikio na wasikie haya,

View attachment 2195022

View attachment 2195105

Hahaha katika watu wako 20 wanaokuzunguka kuna yoyote mwenye account ya Amazon?

Hao unaotegemea ww watanunua ni wakina Nani?

Kuna mtu gani maarufu kwenye hiyo movie?

Movie ngapi za Aina hiyo ww umewahi kununua online?
 
Wewe umatania, eti viewers 100 million, Seriously!! Hata ingekuwa Netflix kupata 100 million viewers in one year siyo rahisi .....!! Kwa akili yako kama hiyo moview ya Maza inaweza kuingiza hiyo pesa then Amazon kwa mwaka wanaingiza kiasi gani kwa maelfu ya movie walizonazo online!!? May next year urudi hapa kutupa marejesho tuone hata kama wamepata 100 K viewers ....!!

Anyway, movie ilikuwa ni ya kutangaza utalii, sasa kama inauzwa then availability yake inakuwa limited kwa kiasi fulani. Binafsi mpaka sasa sioni kama hivyo movie was a good idea ..... Halafu target USA. But time will tell.

Pia akirudi asisahau kuisafisha nchi kuhusu Ugaidi walioipachika nchi yetu ..... maana USA na ugaidi. Tumemsikia Maza alivyodai kuwa nchi yetu ni ya amani sana ..... anasahau kuwa toka ameingia madarakani wamefuta kesi za Magaidi zaidi ya 50 ....!!
 
Hahaha katika watu wako 20 wanaokuzunguka kuna yoyote mwenye account ya Amazon?

Hao unaotegemea ww watanunua ni wakina Nani?

Kuna mtu gani maarufu kwenye hiyo movie?

Movie ngapi za Aina hiyo ww umewahi kununua online?
Bora hata wale jamaa wa parachichi, hawa hesabu ni zero kabisa
 
Nani amekwambia 7.2B inaweza zalisha movie nzuri ya US standards ili ilirejeshe hizo TrilionMi najua budget za movie za namna hiyo ni 20-100 billion, then actors wanalipwa in percentages hela zinazo zidi hapo.

Kiurahisi nikuambie Tu, tunaweza Rudisha investment yetu Ila faida haiwez directly patikana katika hiyo investment, itapatikana indirectly kutokana na watalii kuongezeka but also uwekezaji kwenye utalii pia
 
... fanyeni kazi acheni kupenda vitu rahisi! Mjikalie tu halafu ziingie 1.5T kila mwaka kirahisi tu? Twendeni tukalime ardhi kisasa; tupate ngano, mafuta ya kula, na sukari ya kulisha hadi na vizazi vyetu ziada tuuze nje tupate fedha za kigeni. Tukafanye mapinduzi ya kilimo.

Tukawekeze kwenye mifugo kisasa tupate nyama ya kutosha na ziada tuuze nje tupate fedha nyingi za kigeni; tuka-export the best leather products; tukahakikishe hakuna mtoto wa taifa hili anatembea peku; hapo ndipo tutakuwa tumeitendea haki akili, nguvu, na ardhi tuliyopewa na Mungu. Royal tour iwe ziada tu.
 
Back
Top Bottom