Ndugu zangu Watanzania,
Nimesoma mapendekezo ya CHADEMA yaliyowasilishwa mbele ya kamati ya Bunge neno kwa neno, msitari kwa msitari na kifungu kwa kifungu.nimesoma kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa kuwa mimi siyo mvivu katika kusoma na huwezi ukanificha jambo kwa kuliweka kwenye maandishi kwa matarajio kwamba sitasoma.
Hii ni kwa kuwa mimi ni mtu ninayependelea sana kusoma hasa vitu vilivyoandikwa kwa urefu sana ndio huwa napenda kuvisoma kwa utulivu ili kujuwa kilicho ndani yake.ndio maana napenda kusoma sana na kusikiliza vyema kilicho andikwa na kinachozungumzwa na mtu hata kama ni hotuba ndefu kiasi gani.
Ili andiko langu lisiwe refu sana basi Leo nitawapitisha katika hoja namba tano inayohusu aina ya wabunge na hoja namba nane inayohusu muundo wa tume na mapendekezo waliyopendekeza CHADEMA.
Ndugu zangu Watanzania imenisikitisha sana tena sana kunihuzunisha, kunishangaza, kuniduwaza, kunisononesha,kunipa mawazo, kunistajaabisha, kunipa maswali yasiyo koma niliposoma mapendekezo ya CHADEMA katika aina ya wabunge katika hoja yao namba tano.
Kwamba sasa CHADEMA wanapendekeza kuwa katika kila jimbo kuwe na wabunge wawili wawili watakaochaguliwa na wananchi kwa kufuata jinsia na makundi, yaani kutakuwa na mgombea mwanamke na mwanaume katika kila jimbo la uchaguzi ambapo mwanaume atapigiwa kura na wanaume tu na mwanamke naye atapigiwa kura na wanawake wenzake. halafu hapo hapo mwisho wa siku baada ya kumaliza uchaguzi mkuu CHADEMA wanataka na kupendekeza tena kuwe na wabunge wa viti maalum wasiopungua 30% ndani ya bunge letu.
Pia kwanini kuwe na viti maalumu tena wakati tayari mmeshapendekeza na kutaka kuwa kila jimbo lazima awepo mwanamke? Sasa hao viti maalum wanaingia kufanya nini tena bungeni? Kwani nini yalikuwa madhumuni ya kuanzisha viti maalumu? Si yalikuwa ni kuleta usawa wa kijinsia? Sasa kama mmependekeza kuwepo mwanamke kila jimbo halafu unataka tena viti maalum vya nini ? Hivi CHADEMA mna akili kweli ninyi?
Hivi nani aliyependekeza ujinga huu ndani ya CHADEMA? Kwa faida ya nani? Kwa jasho la nani ? Kwanini CHADEMA wanataka kutubebesha mzigo Watanzania walipa kodi? Kwanini wanaangalia maslahi yao na matumbo yao na kutusahau wananchi walipa kodi? Kwanini wanataka pesa zote na makusanyo yote ya nchi yaelekezwe katika kulipa mishahara na marupurupu ya wabunge? Kwanini tuache kufanya maendeleo na tujikite katika kulipa mishahara na kuwalea na kuwatunza wabunge kwa jasho letu? Yaani badala ya kufikiri namna ya kupunguza gharama wao wanaongeza gharama? Yaani jimbo liwe na wabunge wawili ? Halafu tena baadaye mpewe tena viti maalumu?
Hivi kwanini ninyi CHADEMA mbatupatia saba hasira na kichefuchefu Watanzania? Kwanini mnatia kinyaa? Hivi kama hamna hoja kwa nini msikae kimya? Hivi huu ndio ujinga na uhayawani mliokuwa mmekalia siku zote mnaujadili kwa ajili ya maslahi ya mimatumbo yenu kuijaza? Tutakuja kula kwenye matumbo yenu? Mtatuwekea bomba la chakula kutoka kwenye matumbo yenu? Yaani sisi tuhenyeke halafu ninyi mnataka kujiwekea uchochoro wa kutafuna pesa za nchi? Mna akili kweli ninyi?
Kwamba tuwe na wabunge wengi kuliko hata uingereza? Nani kasema na kwa hoja ipi na kwa utafiti upi na kwa ushahidi upi na kwa mifano ya wapi na kwa misingi ipi na kwa vigezo vipi na kwa namna gani? wingi wa wabunge katika jimbo moja kunachochea maendeleo katika jimbo? na vipi mbunge mmoja hawezi kuleta maendeleo katika jimbo mpaka wawe wawili? Kwa nini pesa za kumhudumia mbunge wa pili kuanzia mshahara,pesa ya usafiri au gari,posho za kikao,safari,kamati,kiinua mgongo zisipelekwe katika jimbo husika kuchochea maendeleo ya wananchi?
Kwanza kwanini mnataka mlete ubaguzi katika kupiga kura? Kwa kuwa pendekezo lenyewe ni la kibaguzi tu.utaanzaje kusema kila jinsia impigie mtu wa jinsia yake? Siyo ubaguzi huu? Siyo kuvunja umoja, mshikamano, upendo na nguvu katika majimbo na hatimaye Taifa zima kwa ujumla wake na hivyo kuzorotesha maendeleo katika majimbo na Taifa zima kwa ujumla wake?
Kwanini mnakuwa walafi sana na wenye uchu wa madaraka ninyi CHADEMA? Kwanini siku zote mnajifikiria matumbo yenu na familia zenu pekee? Mmegikiria kuwaza maisha ya watanzania na vipato vyao? Mngewaza maisha ya watanzania mngeanzia wapi kupendekeza ujinga wa namna hiyo?
Kwa hakika mlaaniwe kabisa ninyi mliokosa akili za kutambua maisha ya watanzania na vipato vyao na uzalendo kwa Taifa letu .Mungu awaalaani na kuwapiga upofu katika kila kitu. Nawaombea mpigwe pigo kama la 2020 msiwepo kabisa Bungeni ,maana hamna faida yoyote ile zaidi ya kujali matumbo yenu na maslahi yenu na kuja kuleta vivuli mtaani mkishavimbwiwa kodi zetu kama ambavyo mmekuwa mkitutukana kama alivyo fanya Godbless Lema kwa kusema kazi ya bodaboda ni ya laana.
Nitaendelea kuchambua hoja namba nane katika uzi mwingine.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.