Mapigano yanayoendelea Gaza na unafiki wa Dunia

Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu
Mh
 
Inajilinda? Are you insane? Yaani Israel inaikalia Palestina kimabavu kwa miaka 70 sasa alafu anayeonewa akijipambania kupata uhuru unasema mvamizi anajilinda? Kwahiyo Putin naye anajilinda Ukraine?

Huu ndio unafiki anaosema mtoa mada
Inajilinda dhidi ya ugaidi
 
  • Thanks
Reactions: 511
Duniani kote kila Bara kuna mapigano yanayoendelea huku kukiwa na ushawishi sifuri kwenye kusitisha hizo vita. Ninasema mapigano kwa sababu sehemu kubwa ya mapambano hayo yametokana na ushawishi wa makundi yanayolenga kufaidika na vita hizo. Kinachoendelea Ukraine na Urusi ni vita kamili kwa sababu pande zote wanaumizana na kila upande una uwezo wa kujibu mashambulizi ya kutoka upande hasimu. Anayelaumiwa hapo ni Urusi

pale Gaza, kinachoendelea siyo vita (kwa tafsiri yangu), bali ni mauaji ya halaiki ambayo yanadhaminiwa na Umoja wa Ulaya na Marekani kuisaidia Israel kuua watoto, wanawake na watu wa taifa la Palestina. Kwa nini nasema ni mauaji ya halaiki, ni kwamba Israel inatumia zana zote za kivita dhidi ya taifa ambalo kimsingi halijaingiza jeshi lake vitani. Hakuna zana wala kifaa chochote za kivita cha Taifa la Palestina zilizoingizwa vitani. Hakuna jeshi la Palestina lililopo mstari wa mbele kulinda mipaka yao ambayo inaingiliwa bila huruma na Israel. mauaji yanayoendelea yamejengwa kwenye dhana ya kupambana na ugaidi ambapo hata watoto na wanawake ambao kimsingi ni vulnurables kuwa wanawaficha magaidi. Ukiangalia ndani zaidi majuzi hapa Wafanyakazi wapatao 7 wa World Kitchen Centre wameuawa kwa kulengwa na vikosi vya Israel. Shirika hilo lenye makao yake makuu Marekani ndilo pekee lililosalia Gaza kutoa msaada wa kibinadamu ya chakula na maji safi. Hilo linajiri kwa sababu Israel imefunga mipaka ya kila kona kuzuia misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapalestina waliokusanywa eneo la Kaskazini. Humu kwenye mitandao wamejaa washabiki wa kila namna bila kutafakari madhara na madhila yatokanayo na hizi tabia za kuuana kwa kujitetea kulinda utu na ustawi wa wauaji. Lakini anayelaumiwa kwenye mauaji haya ni Palestina

Afrika kuna mapigano karibia eneo kubwa la Bara hili, huku viongozi wa nchi za bara hili yaani zinazounda Umoja wa Afrika wakiendelea kujimwambafai pale Addis Ababa kwa robusta na aina kede za kahawa zinazopatikana mjini hapo. Karibia viongozi wote wapo handicapped kifikra kwa kuweka matumaini makubwa kwa nchi zilizoendelea hususan mataifa yanayotengeneza na kusambaza kwa wingi silaha na zana za mauaji duniani. Sisi Tanzania tumepeleka vikosi vya kulinda amani kwenye mataifa hayo na tunachoambulia ni kuwazika vijana wetu wanaouawa kwenye conflicts hizo zisizo na kichwa wala miguu.

Tutafakari haya

  1. DRC mapigano yanayoendelea, kwa nini hakuna juhudi za kumaliza mapambano yale? Kwa nini wanaouawa ni raia ambao siyo wahusika wa tofauti za kusaka madaraka baina ya makundi yanayopigana?
  2. Juba, mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya Serikali inayoongozwa na Salva Kiir na vikosi vya aliyekuwa makamu wake Riek Machari, mapigano hayo yanasababisha wakimbizi na mauaji ya kutisha kwa wananchi ambao kimsingi siyo sehemu ya ugomvi huo. Je nini kinafanyika kumaliza vita hiyo?
  3. Sudan Kaskazini, vita ni kubwa baina ya vikosi vya serikali na majenerali waliojitenga. wote wanasaka madaraka kuwaongoza watu ambao wanawaua kila kukicha kwa silaha zao... Nani wa kuzuia haya mauaji yasiendelee?
  4. Somalia bado ipo kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
  5. Msumbiji imerudi kwenye kupigana vita vya msituni kutokana na vikundi vya kigaidi kujiimarisha Kaskazini mwa nchi hiyo. Eneo la Cabo Delgado siyo salama kwa raia kuishi kwa sababu wanachinjwa na kutishiwa usalama wao kila kukicha. Matukio hayo yanafanyika jirani na mpaka wa Tanzania na baadhi ya matukio yamejiri ndani ya ardhi ya Tanzania....
  6. Uganda, hakujatulia mapambano ya msituni yanaendelea
  7. Afrika Kaskazini ipo katika hekaheka ya mapambano ya msituni ndani ya nchi nyingi za mataifa ya eneo hilo.
  8. Syria, imekuwa vitani hususan dhidi ya mataifa yanayoongozwa na Marekani wakimpinga rais wa nchi hiyo, na kusababisha maafa makubwa ndani ya taifa hilo.
  9. Yemen, imekuwa katika vita inayopewa chapuo na mataifa makubwa ikiwemo Marekani
  10. Libya, ipo ndani ya Afrika lakini Mataifa makubwa chini ya kibali cha Umoja wa Mataifa yalienda kuua raia ili kumng'oa Gadaffi maradakani na hatimaye kumuua. na mpaka leo hakujatulia....
  11. Mifano ni mingi sana nsana.
Sasa tujiulize:
  1. Sisi Watanzania, tunapata wapi ujasiri wa kushabikia hizi vita zinazopiganwa duniani?
  2. Je, kwa sababu tunaishi kwa amani, tunayachukuliaje maisha ya Watoto na wanawake kwenye maeneo ya vita?
  3. Taifa letu, linapowapeleka vijana wetu kulinda amani kwenye maeneo ya vita, Ni amani ipi inayolindwa ikiwa hakuna upokonyaji wa silaha kwa mahasimu wa vita?
  4. Tunafaidika nini na ukimya ama kuchukua pande baina ya mahasimu wa kila vita?
  5. Taifa limejiandaaje ama linawaandaaje watu wake hususani kukabiliana na changamoto za Vita zinazopiganwa karibu na mipaka yetu?
  6. DO WE CARE?
Uchambuzi wako mzuri, lakini hautofautiani na wachambuzi wengine wanaojikita kwenye udini.

Hapa nilitaraji ungelichambua kwanza na kukiweka dhahiri kiini kilichosababisha chanzo cha mgogoro na hatimaye vita hivyo vya Israel na Palestina kufumuka.

Tunaelewa namna waPalestina walivyovamia kimakame nguvu na kuua raia wa Israel na wa mataifa mbali mbali wakiwemo waTz wasiokuwa nahatia pamoja na kuwachukua mateka.

Kwa nini walifanya mauaji hayo wakati diplomasia zipo kushuhulikia migogoro?

Mtu asiyeanza na uchambuzi wa kina wa tukio hilo ama kulilaani kwanza kabla hajaanza uchambuzi wake, binafsi humuona kama yupo biased na udini.
 
Umejenga hoja ingawa umetanguliza walakini mwanzoni.

Siyo lengo langu kuangalia haya matukio hususani vita unayoiongelea kwa mtazamo wa kidini. Ni vile umefuatilia majibu ama michango ya wanaJF walioamua kushirikisha udini na haya mapigano pale Gaza. Pia niliepuka kujadili chanzo ama sababu za haya mambo kwa sababu zipo threads ambazo wanachambua vyanzo vya vita na ongoing situations.

Lengo la Uzi wangu ni kuangalia impact ya haya mauaji yanayoendelea duniani. Ukiangalia kwa undani unaweza kuona mataifa yanayotengeneza na kusambaza silaha duniani wamekuwa mstari wa mbele kuchochea ama kusababisha vita hizi. Labda Umoja wa Mataifa ambayo imekuwa bias kutetea maslahi ya nchi zilizoendelea imekuwa ni chanzo cha kushindwa kustawisha amani na mshikamano duniani.

Kimsingi si lengo la uzi huu kujadili kwa mlengo wa kidini ingawa kila mchangiaji ana uhuru wa kuweka mtazamo wake huru
 
Lengo lako siyo vita zote ila ni kuelezea vita ya mashariki ya kati. Umezuunguka ila hoja ya ko ya msingi umeiweka katikati pale unapozungumzia mauaji ya halaiki wakati ni vita na watu wa pande zote mbili wanauawa.

Umeogopa kuzungumzia moja kwa moja kwa kuhisi labda utashambuliwa kwamba wewe ni mdini lakini kwa vile ndo lengo lako lilikuwa hilo, hatimae wengi wamekuelewa na mijadala imejikita huko ambako wewe uliona unapakwepa.
Kwa kifupi tu ACHA UNAFIKI.
Unafiki ni nini hapo?
Je unanipangia ama unanitishia? Unachokilazimosha ni kama unataka mwanaume kwa nguvu

Who am I to you? Hutaki kusoma hoja zangu bonyeza ignore button.
 
Mchinje watoto wa wayahudi kisha mtegemee huruma, Myahudi ni katili, yeye huamini kwenye sheria za jicho kwa jicho.
Endeleeni kuua Wakristo Ila kwa wayahudi temaneni kabisa, na mtakufa sana tu.
Kuna picha niliona sehemu za watoto wa Wayahudi mliochinja, yaani inasikitisha mpaka nikatamani mpigwe sana nyie watu,
 
Unafiki ni nini hapo?
Je unanipangia ama unanitishia? Unachokilazimosha ni kama unataka mwanaume kwa nguvu

Who am I to you? Hutaki kusoma hoja zangu bonyeza ignore button.
Naona uneishiwa hadi umeanza kutafuta wanaume. Pole sana
Ila uache UNAFIKI
 
Ila nyie mnaojiita waislamu ,mnaudharirisha uislamu,kama waislamu wote hawana akili kabisa!

Kumbe ni mahaba yenu ya kipumbavu na mihemko kwenye maisha!

Mtu wa kwanza kushambulia alikua HAMAS, halafu mnasema kaonewa! Vita haina macho ,yoyote anafinywa tu!

Jeshi la nchi linalipwa na kodi za wananchi, i mean boss wa jeshi ni wananchi wenyewe, wakiwemo wazee na watoto! Ko boss ndo anaepigwa hapo!
 
Ni kweli kabisa.
Sasa najiuliza kwamba, na Ukristo wangu wote ninawezaje kujijasirisha kuwa Yesu alikuja duniani kuokoa maisha ya watu wakati kinachoendelea ni kinachoitwa Taifa teule linaua watu bila aibu wala haya?
Mkuu,
Mapalestina Yana INDOCTRINATION zao Ukijumlisha RADICAL MUSLIMS
Najua huruma ingekuondoka siku ambayo ungeshuhudia uwapendao wameuwawa na Hamas bila hatia YEYOTE na bado wanaleta chokochoko na DHARAU za kupindukia....

100%% percent nawahakikishiaa Kuna good Palestinians na wameingizwa vitani na Hamas bila kupenda na ubaya wa Vita hazichagui waliopo na wasiokuwepo..

Vita vya Congo Kuna mdau mmoja naungana nae serikali ya Congo haionyeshi jitiada madhubuti kupambana na tatizo sisi tumepeleka vijana wetu na juzi juzi wameuwawa kadhaa
Maoni yangu Tanzania ingewasaidia kudeal na chanzo na chanzo kinacho semwa Sana Ni RWANDA piga kagame na kumwondoa madarakani ie kagame ana support ya mmarekani na for sure atakua na ma drone ndio maana anatudindiaga
 
Walipouawa wa Israel October 7 mbona ulikuwa kimya wewe
 
main-qimg-59203067b5263c40a82fd971fefe35de
 
Duniani kote kila Bara kuna mapigano yanayoendelea huku kukiwa na ushawishi sifuri kwenye kusitisha hizo vita. Ninasema mapigano kwa sababu sehemu kubwa ya mapambano hayo yametokana na ushawishi wa makundi yanayolenga kufaidika na vita hizo. Kinachoendelea Ukraine na Urusi ni vita kamili kwa sababu pande zote wanaumizana na kila upande una uwezo wa kujibu mashambulizi ya kutoka upande hasimu. Anayelaumiwa hapo ni Urusi

pale Gaza, kinachoendelea siyo vita (kwa tafsiri yangu), bali ni mauaji ya halaiki ambayo yanadhaminiwa na Umoja wa Ulaya na Marekani kuisaidia Israel kuua watoto, wanawake na watu wa taifa la Palestina. Kwa nini nasema ni mauaji ya halaiki, ni kwamba Israel inatumia zana zote za kivita dhidi ya taifa ambalo kimsingi halijaingiza jeshi lake vitani. Hakuna zana wala kifaa chochote za kivita cha Taifa la Palestina zilizoingizwa vitani. Hakuna jeshi la Palestina lililopo mstari wa mbele kulinda mipaka yao ambayo inaingiliwa bila huruma na Israel. mauaji yanayoendelea yamejengwa kwenye dhana ya kupambana na ugaidi ambapo hata watoto na wanawake ambao kimsingi ni vulnurables kuwa wanawaficha magaidi. Ukiangalia ndani zaidi majuzi hapa Wafanyakazi wapatao 7 wa World Kitchen Centre wameuawa kwa kulengwa na vikosi vya Israel. Shirika hilo lenye makao yake makuu Marekani ndilo pekee lililosalia Gaza kutoa msaada wa kibinadamu ya chakula na maji safi. Hilo linajiri kwa sababu Israel imefunga mipaka ya kila kona kuzuia misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapalestina waliokusanywa eneo la Kaskazini. Humu kwenye mitandao wamejaa washabiki wa kila namna bila kutafakari madhara na madhila yatokanayo na hizi tabia za kuuana kwa kujitetea kulinda utu na ustawi wa wauaji. Lakini anayelaumiwa kwenye mauaji haya ni Palestina

Afrika kuna mapigano karibia eneo kubwa la Bara hili, huku viongozi wa nchi za bara hili yaani zinazounda Umoja wa Afrika wakiendelea kujimwambafai pale Addis Ababa kwa robusta na aina kede za kahawa zinazopatikana mjini hapo. Karibia viongozi wote wapo handicapped kifikra kwa kuweka matumaini makubwa kwa nchi zilizoendelea hususan mataifa yanayotengeneza na kusambaza kwa wingi silaha na zana za mauaji duniani. Sisi Tanzania tumepeleka vikosi vya kulinda amani kwenye mataifa hayo na tunachoambulia ni kuwazika vijana wetu wanaouawa kwenye conflicts hizo zisizo na kichwa wala miguu.

Tutafakari haya

  1. DRC mapigano yanayoendelea, kwa nini hakuna juhudi za kumaliza mapambano yale? Kwa nini wanaouawa ni raia ambao siyo wahusika wa tofauti za kusaka madaraka baina ya makundi yanayopigana?
  2. Juba, mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya Serikali inayoongozwa na Salva Kiir na vikosi vya aliyekuwa makamu wake Riek Machari, mapigano hayo yanasababisha wakimbizi na mauaji ya kutisha kwa wananchi ambao kimsingi siyo sehemu ya ugomvi huo. Je nini kinafanyika kumaliza vita hiyo?
  3. Sudan Kaskazini, vita ni kubwa baina ya vikosi vya serikali na majenerali waliojitenga. wote wanasaka madaraka kuwaongoza watu ambao wanawaua kila kukicha kwa silaha zao... Nani wa kuzuia haya mauaji yasiendelee?
  4. Somalia bado ipo kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
  5. Msumbiji imerudi kwenye kupigana vita vya msituni kutokana na vikundi vya kigaidi kujiimarisha Kaskazini mwa nchi hiyo. Eneo la Cabo Delgado siyo salama kwa raia kuishi kwa sababu wanachinjwa na kutishiwa usalama wao kila kukicha. Matukio hayo yanafanyika jirani na mpaka wa Tanzania na baadhi ya matukio yamejiri ndani ya ardhi ya Tanzania....
  6. Uganda, hakujatulia mapambano ya msituni yanaendelea
  7. Afrika Kaskazini ipo katika hekaheka ya mapambano ya msituni ndani ya nchi nyingi za mataifa ya eneo hilo.
  8. Syria, imekuwa vitani hususan dhidi ya mataifa yanayoongozwa na Marekani wakimpinga rais wa nchi hiyo, na kusababisha maafa makubwa ndani ya taifa hilo.
  9. Yemen, imekuwa katika vita inayopewa chapuo na mataifa makubwa ikiwemo Marekani
  10. Libya, ipo ndani ya Afrika lakini Mataifa makubwa chini ya kibali cha Umoja wa Mataifa yalienda kuua raia ili kumng'oa Gadaffi maradakani na hatimaye kumuua. na mpaka leo hakujatulia....
  11. Mifano ni mingi sana nsana.
Sasa tujiulize:
  1. Sisi Watanzania, tunapata wapi ujasiri wa kushabikia hizi vita zinazopiganwa duniani?
  2. Je, kwa sababu tunaishi kwa amani, tunayachukuliaje maisha ya Watoto na wanawake kwenye maeneo ya vita?
  3. Taifa letu, linapowapeleka vijana wetu kulinda amani kwenye maeneo ya vita, Ni amani ipi inayolindwa ikiwa hakuna upokonyaji wa silaha kwa mahasimu wa vita?
  4. Tunafaidika nini na ukimya ama kuchukua pande baina ya mahasimu wa kila vita?
  5. Taifa limejiandaaje ama linawaandaaje watu wake hususani kukabiliana na changamoto za Vita zinazopiganwa karibu na mipaka yetu?
  6. DO WE CARE?
Ndugu umemwaga madini haswa ila watu watakuja na mihemko ya kidini!!
 
Mkuu
Nimeshashambuliwa sana.

Vita zote hususan Gaza ni mauaji ya kukusudia.

Ulimwengu umekaa kimya. Kwa sababu Marekani inafadhili vita hiyo
 
Sawa.
Haya tuzungumzie DRC ambapo vijana wetu wameuawa huko jana hapa.

Vipi wananchi wa huko wana haki ya kuishi au nao nikawapiganie?
Wana haki maana wao hawakwenda kuishambulia m23. Bali haom23 ndio wanawafata kwao.
Same applies to Israel. Walifatwa na kuuliwa ndugu zao, wana haki ya kujilinda.
 
Mkuu
Nimeshashambuliwa sana.

Vita zote hususan Gaza ni mauaji ya kukusudia.

Ulimwengu umekaa kimya. Kwa sababu Marekani inafadhili vita hiyo
Kwa nini umuone marekani tu kuifadhiri Israel?
Mbona hujaongelea Iran kuifadhiri Hamas?

Israel inafanya mauaji ya makusudi kama ambavyo Hamas alifanya mauaji kimakusudi, tena kwa kuongozwa na Gen. Wa Iran
Screenshot_20240406-211201~2.png
 
Kihistoria Ukraine ni sehemu ya urusi..... vipi una maoni gani kwa Putin kuchukua eneo la urusi kihistoria? Au Idd Amin alikua sahihi kupora Kagera kisa ilikua kihistoria ina roots za Uganda?
Umechemka kasome tena historia.. Ukraine ndio sehemu ya kwanza kukaliwa na binadamu ukiachia na Russia so historia yako haiwezi kuwa na upended wa kuweka yai au kuku kipi kilianza
 
Ni kweli kabisa.
Sasa najiuliza kwamba, na Ukristo wangu wote ninawezaje kujijasirisha kuwa Yesu alikuja duniani kuokoa maisha ya watu wakati kinachoendelea ni kinachoitwa Taifa teule linaua watu bila aibu wala haya?
Kama unashangaa Israel kuuwa watu sasa hivi, Je kipindi wanatoka utumwani waliua watu wangapi njiani?
Je kipindi wanapigana na wafilisti waliua wangapi? Nani aliwaruhusu kuua?
Walikuwa wanaua mpaka watoto na wanyama kwa agizo la nani?

Je kwa nini Mungu aliwaruhusu kuua?
Wakati wa Yesu mauaji hayakuwepo?
 
Inajilinda? Are you insane? Yaani Israel inaikalia Palestina kimabavu kwa miaka 70 sasa alafu anayeonewa akijipambania kupata uhuru unasema mvamizi anajilinda? Kwahiyo Putin naye anajilinda Ukraine?

Huu ndio unafiki anaosema mtoa mada
Huna hata basic knowledge ya Arabs and jews.. you better ukae kimya maana ni ujinga kukomaa na kuandika upupu.. iwe history, dini tatu uislam,uyahudi na ukristo hautambui Palestine. Quran inayowaongoza Muslim inatambua Jews na ni Nabii Mussa alipewa aeshi na Allah watoto wa Israel wake na wasitoke hadi kiama.. so jua unashindana na Allah kwa issue ya Israel unakufuru unavyopinga ya Allah unakuwa kafir.

Unaposema miaka 70 nenda kwenye historia ya UN ukasome. Walitakiwa waishi pamoja Arabs na waisrael.

Arabs wakakataa na kuanzisha vita ya genocide kuwafuta wayahudi wote from the sea to the river.. Jews wakaone hawabvipi mashetani wanataka kutuua. Ndio vita ikaanza.. watumwa wa Allah wakadundwa..
Sasa kukaliwa kivipi wauaji wale wasio taka amani. So 70 ni ya wao wenyewe wapumbavu na unapozungumzia miaka 70 jua Israel iliwaonea huruma kutowamaliza waanzisha vita
 
  • Nzuri
Reactions: 511
Back
Top Bottom