Haya bwana. siku hizi wala siendelezi mijadala kama hii. Umeshinda. duh, Mzungu alikuwa akinunua watumwa zanzibar!! Maajab haya.
Maajabu? Someni, tafuteni!! Sio mlishwe tu Halelujah mkaitikia «Emen»
Wazungu mpaka.walitumia Sayansi kuwafanya waafrika watumwa!
Bristol and Transatlantiska
Mawazo ya ubaguzi wa rangi
Kadiri biashara ya watumwa ilivyoendelea, Wazungu walianzisha itikadi ya ubaguzi wa rangi ambayo inaweza kutumika kuhalalisha hiyo biashara. Waafrika walikuwa walidhaniwa kuwa daraja la chini ya binadamu, wasio na ustaarabu, na watu duni mbele ya Wazungu katika kila hali. Na kuwa wao watu weusi walikuwa yaani 'si miongoni mwao' (wakisema "not one of us"), walikuwa ni kama bidhaa wanaweza kununuliwa na kuuzwa. Maendeleo ya ubaguzi wa rangi yanahusishwa na biashara ya watumwa.
Biashara ya watumwa isingaliendela bila ya itikadi hii kutumika ili kuihalalisha.
Ubaguzi wa rangi hauwezi kupuuzwa katika utafiti wowote biashara ya utumwa.
Wa Anglikana kwao rangi nyeusi ilishabihishwa na mauti na uovu kwa karne na dahari, kabla ya kukutana watu wowote weusi. Hivyo muonyo wao wa kwanza kwa watu wenye ngozi nyeusi ilikuwa kudhani kwamba walikuwa baadhi aina ya shetani au mnyama wa kutisha. Kutokana na dhana hii mbovu, na kutokana na hadithi za wasafiri, ukazuka ubaguzi wa wa-Afrika, kama washenzi, kuwa ni wepesi kwa mifadhaiko ya ngono, wavivu, wasioaminika na walaji nyama ya watu (cannibalistic). Kulikuwa na watu wachache ambao walipinga mtazamo huu wa kibaguzi. Richard Ligon, katika kitabu Chake Historia ya Kweli na Halisi ya Kisiwa cha Barbados, kilicho chapishwa katika 1657, aliandika dhidi ya dhana hiyo mashuhuri. Yeye aliamini 'kwamba walikuwa waaminifu, wenye imani (faithfull) na miongoni mwao kuna watu wenye utambuzi, kama miongoni mwa wale wa Ulaya.
Na kutoka mwaka 1600, na maendeleo ya kisayansi kuzidi katika Ulaya, ubaguzi wa rangi nao 'ulithibitishwa' (kuhalalishwa) kisayansi. Wanasayansi na wana falsafa kama David Hume alidiriki kusema ya kuwa Waafrika walikuwa 'kijinsia ni watu duni kwa wazungu'. Iliaminika zaidi kwamba Waafrika na Wazungu walikuwa na Maendeleo tofauti.
Wengi, kama Sir Thomas Herbert, kuandika katika 1634, waliamini kuwa Waafrika lazima wanahusiana na nyani na walikuwa tofauti na ni kabila duni. Hii ilikuwa muda mrefu kabla nadharia ya Charles Darwin ya Mageuzi (Evolution), ambayo ilionyesha kuwa binadamu wote asili yao ni moja (Nyani). Katika kipindi cha karne ya 18 na 19, watu wengi weupe walipiga kampeni kwa ajili ya kusitisha biashara ya watumwa na Uhuru wa watumwa. Lakini ni watu weupe wachache tu waliamini katika usawa watu wote, kwamba ni usawa kati ya Jamii ya weusi na weupe.
Katika karne ya 19, itikadi ya ubaguzi wa rangi ilipewa nguvu sayansi 'fake' kama hii phrenology. Iliaminika kwamba sura na umbo la fuvu ndio linaashiria tabia ya mtu. Phrenologists walitumia nadharia yao juu fuvu la Mwafrika na kujumuisha Waafrika Wote kama ni Duni kwa Jamii nyeupe kielimu, kiutamaduni na kimaadili. Phrenology ilionyesha Waafrika kuwa unsuited kufanya Kazi Nyingine Zaidi ya kwamba inasimamiwa na watu weupe. Katika Mawazo ya wengi wao, hii iliwapa haki ya kuwafanya Waafrika kuwa watumwa.
Utafiti wa teleology unalenga katika Ubunifu Asilia (design in nature). Hii iliwapa wazungu haki ya kusema kuwa Waafrika walikuwa, kiasili, wanafaa kwa kufanya Kazi za nguvu lakini si za kufikiri na za ujuzi. Walikuwa, wameumbwa kuwatumikia watu weupe. "Negro kama (wanavyowaita) kwa ujumla alizaliwa awe Mtumwa" aliandika Sir Harry Johnston, Mkoloni wa Kiingereza katika Afrika katika miaka ya 1890.
Anthropology, utafiti wa watu, katika mambo mengine ulikita katika uchunguzi wa ukubwa wa ubongo na maumbile ya kimwili ya watu. Anthropologists nao walithubutu kuhitimisha kwamba wa Afrika walikuwa ni watu Duni kuliko Wazungu, Aina tofauti ya watu yenye ukaribu zaidi kuhusiana nyani kuliko wazungu.
Naturalist wa Kiingereza, Charles Darwin, akaanzisha ya nadharia ya Mageuzi [Evolution] Nadharia yake alipendekeza kuwa Wazungu walikuwa wanahusiana na Waafrika na kwamba binadamu Wote walikuwa wanahusiana na nyani. Wakati hii ilitoa kero kwa ile anthropological theory kuhusu aina tofauti na anwaa za maumbile, Mambo mengine ya nadharia ya mabadiliko bado 'yalithibitisha' ubora wa Jamii nyeupe Juu ya Jamii za wengine Wote. Nadharia yake aliona kuwa Anglo-Saxon, yaani, British, wako daraja ya juu katika kipimo cha mabadiliko [Evolutionary Scale]. Yaani Waingereza walikuwa Juu ya Mti wa Familia ya Wanadamu, zaidi 'kistaarabu' [Most Civilized Race]. Wafrika, as 'primitive' race, wailionekana kuwa kama watoto wachanga na unintelligent. Jamii 'Duni' waliokuwa wamepotea aidha ili watawaliwe au kuangamizwa na Jamii 'Bora' (Weupe). Maisha ya Mwenye Nguvu Mpishe (Survival of fittest theory) ilikuwa ni sheria katika nadharia ya Darwin ya Mageuzi.
Imani katika Ubwanyenye wa Jamii ya watu Weupe Uingereza na Ulaya ndio ulihuisha upanuzi wa himaya (Empire). Himaya ya Uingereza iliongezeka wa Kutoka Wazo 'kwamba Uingereza walikuwa Kabila Bora la Utawala wa Dunia', maoni yaliyotolewa na Cecil Rhodes, mtawala wa kikoloni ambaye alianzisha koloni ya Uingereza ya Rhodesia, katika Afrika kusini ya Equator (Sasa Zimbabwe).
Hizi nadharia za 'kisayansi' nadharia za uduni wa Muafrika kwa ujumla ulikubalika na wananchi wa Uingereza. Ubaguzi wa rangi ilikuwa kuchukuliwa kirahisi kama jambo la kawaida. Kwa mfano, vitabu vya GA Henty vilikuwa vikionekana kama vya umuhimu mkubwa kwa ajili wavulana. Kitabu chake "By Sheer Pluck": Hadithi ya Vita vya Ashanti kiliandikwa Mwaka 1884 na pengine bado kinapatikana katika Maktaba za SHULE Hadi katikati ya karne ya 20 wavulana wanasoma hicho hujifunza kuwa watu weusi ni KAMA Watoto tu. Wao Siku zote ama wanacheka tu au kufanya kugombana. Wao naturally ni wazuri wenye shauku (passionate), goigoi, lakini wenye juhudi ya kazi ngumu kwa muda tu; wajanja hadi hatua fulani, wajinga sana kupita maelezo... Wao hawana uhalisi, kabisa hawana uwezo wa Uvumbuzi (they are absolutely without originality, absolutely without inventive power)
Watu weusi wanaoishi nchini Uingereza, pamoja na wale wanaoishi katika nchi zao wenyewe Chini ya tawala za Ukoloni wa Ulaya, walikuwa lazima wakabiliane na ubaguzi huu. Ubaguzi wa rangi imekuwa ni kitovu cha mazoea kwa watu weusi katika Uingereza, kwa karne nyingi zilizopita.
Makala-Kwa hisani ya Peter Fryer na uchunguzi Juu ya Historia ya watu weusi nchini Uingereza katika kitabu chake "Staying in Power" (Kubaki Madarakani)