Mapinduzi ya siku hizi yanafananaje?

Mapinduzi ya siku hizi yanafananaje?

Kuna nafasi ya mbunge teuliwa inakuwa wazi soon, huyu jamaa tunampeleka huko ubalozini kisha tumuhoji kwanini alitaka kumsigina mama akiwa Tanga?
Intel disclosed. We are watching closely!!!
 
Hii mada ni ya kiutu uzima kwa hiyo tuweke mzaha pembeni kidogo.

Miaka ile ikitokea kuna mapinduzi ya kijeshi, moja ya sehemu ya kwanza ambapo wafanya mapinduzi walikuwa wanachukua ni radio au television ya taifa. Tukumbuke kuwa kipindi hicho kulikuwa hakuna media binafsi.

Hivi katika dunia ya sasa, ya vyombo vya habari binafsi ambavyo vinafika nchi nzima na hata mitandao ya kijamii ambayo inaonekana dunia nzima, mapinduzi ya kijeshi yamebadilikaje au kuna uwezekano siku za mbele kuona mabadiliko ya jinsi mapinduzi yanavyofanyika?

Kwenye 'Arab Spring' nakumbuka mitandao ilitumika sana kuangusha serikali lakini hili ni jambo tofauti kidogo na ninaloliongelea lakini lina muelekeo huo huo.

Tukumbuke pia kuwa hata uvamizi wa kijeshi umebadilika. Marekani alipovamia Iraq alikuta adui amejipanga tofauti na yeye akasumbuka sana kupigana tofauti na alivyozoea.

Hili mnalionaje? Tulijadili kiutu uzima.
Mkuu what are you ploting?

Tunahitaji mapinduzi ya kilimo na kiuchuni. Usitutoe kwenye reli
 
Acha woga mkuu. Tuongee kisomi. Hakuna mtu anachochea lolote litokee ila ni majadiliano ya mabadiliko ya dunia. Kuna mijadala mingapi inafanyika humu mwisho wa siku watu wanajifunza na kuwa na uelewa mpana wa mambo.
Unavyoamini wewe kuongelea mapinduzi ndio kujadili kisomi?
 
Mapinduzi ya siku hizi, ni kupandikiza majasui / Chawa wako, kwenye Serikali, Bunge na Mahakama...
 
Hii mada ni ya kiutu uzima kwa hiyo tuweke mzaha pembeni kidogo.
Mkuu, asante kwa kuleta mada nzuri sana hapa jukwaa. Kwa ufupi sana ni kwamba;

Kulikuwa na uhusiano mkubwa sana baina ya serikali kupinduliwa na siasa za vita baridi (Cold War Politics) kati ya kambi ya Magharibi (NATO) na ile ya Mashariki enzi hizo (USSR na China).

Tangia kusambaratika kwa umoja wa USSR miaka ya 1990s, matishio ya usalama wa taifa yamehama kutoa uvamizi wa nchi moja dhidi ya nyingine na sasa ugaidi ndio umechukua nafasi. Watoto wa kihuni wanakwambia ndio habari ya mjini. Ugaidi sasa umekuwa habari ya mjini.
 
Tukumbuke pia kuwa hata uvamizi wa kijeshi umebadilika. Marekani alipovamia Iraq alikuta adui amejipanga
Hapana mkuu. Umekosea kidogo. Saddam Hussein hakuwa amejipanga. Jeshi la Iraq lilikuwa dhaifu sana kutokana na lundo la vikwazo vya uchumi na silaha ilivyowekewa na Umoja Wa Mataifa (UN) baada ya kuivamia Kuwait kinyume na sheria za kimataifa.

Wakati wa vita ya mwaka 1991 Saddam alikuwa na jeshi kubwa lililoshika nafasi ya 6 duniani ndio maana Marekani alifanikiwa kumfukuza Kuwait lakini hakuweza kwenda mpaka Baghdad tofauti na hii ya mwaka 2003 ambapo alifanikiwa kuivunja vunja nchi nzima.
 
kuna uwezekano siku za mbele kuona mabadiliko ya jinsi mapinduzi yanavyofanyika?
Mkuu, trajectory ya masuala ya dunia hubadilika kulingana na wakati. Mambo ya mwaka 1982 kamwe hayawezi kuwa sawa na haya ya mwaka huu wa 2022. Mapinduzi yaliyokuwa yanafanyika mwaka 1982 sio sawa na yanayoweza kufanywa mwaka 2022 na hii yote huwezeshwa na maendeleo ya kisayansi pamoja na kiteknolojia. Kwa kusema hayo machache ninaomba ujue si kwamba mapinduzi hayafanyiki kwa miaka ya hivi sasa, la hasha, yanafanyika ila kwa uchache na kwa njia za kisasa zaidi. Waingereza wanaita Silent Coups.
 
Unavyoamini wewe kuongelea mapinduzi ndio kujadili kisomi?
Mada haiongelei kupanga mapinduzi. Unadhani mimi mjinga kiasi gani hadi nilete mada ya namna hiyo? Siheshimu mtu anayekumbatia ujinga kwa visingizio mbalimbali, ikiwemo cha woga. Mimi naitwa MWANANCHI, unajua maana yake? Unadhani jukumu la kulinda nchi ni la jeshi peke yake?

Mada kama hii inaweza kuamsha wahusika wafanye mabadiliko muhimu kwa faida ya usalama wa nchi, kama wakiona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
 
Mkuu, trajectory ya masuala ya dunia hubadilika kulingana na wakati. Mambo ya mwaka 1982 kamwe hayawezi kuwa sawa na haya ya mwaka huu wa 2022. Mapinduzi yaliyokuwa yanafanyika mwaka 1982 sio sawa na yanayoweza kufanywa mwaka 2022 na hii yote huwezeshwa na maendeleo ya kisayansi pamoja na kiteknolojia. Kwa kusema hayo machache ninaomba ujue si kwamba mapinduzi hayafanyiki kwa miaka ya hivi sasa, la hasha, yanafanyika ila kwa uchache na kwa njia za kisasa zaidi. Waingereza wanaita Silent Coups.
Hilo unalosema J.F. Kennedy aliliongelea kwenye ile hotuba yake maarufu miaka ya 60. Alisema dunia ya sasa siyo tena ya uvamizi bali ya kujipenyeza...." nimefanya tafsiri tu ila alisema "infiltration instead of invasion".

Mapinduzi pekee ambayo kwa upande wangu naona yalikuwa ni classic infiltration ni ya Misri ya Muslim Brotherhood maana wale walijipanga muda mrefu sana.
 
Mkuu what are you ploting?

Tunahitaji mapinduzi ya kilimo na kiuchuni. Usitutoe kwenye reli
Unaogopa kujadili mada za mapinduzi wakati chama kinachokuongoza kinaitwa chama cha mapinduzi.
 
Mada MBAYA!

UZI utaogopwa kuchangiwa na WATU!!

Two areas in common

"Main Money house and National Broadcasting corporation"

Case study;-jaribio la Burundi la Neyombare lililoshindwa kwa msaada wa mabaka toka Bongoland!
Nakubali ni mada sensitive ila sijaileta kwa ubaya. Naamini humu kuna vichwa vilivyotulia ambavyo vinapenda kujadili mada zinazoweza kupanua uelewa wao na kusaidia wengine wawe na uelewa zaidi.
 
Hilo unalosema J.F. Kennedy aliliongelea kwenye ile hotuba yake maarufu miaka ya 60. Alisema dunia ya sasa siyo tena ya uvamizi bali ya kujipenyeza...." nimefanya tafsiri tu ila alisema "infiltration instead of invasion".

Mapinduzi pekee ambayo kwa upande wangu naona yalikuwa ni classic infiltration ni ya Misri ya Muslim Brotherhood maana wale walijipanga muda mrefu sana.
Upo sahihi sana mkuu. Pasipo kufanya vetting ya kutosha unaweza kukuta nusu ya jeshi/baraza la mawaziri ni mapandikizi wa nchi jirani hasimu (India Vs Pakistan)
 
Nakubali ni mada sensitive ila sijaileta kwa ubaya. Naamini humu kuna vichwa vilivyotulia ambavyo vinapenda kujadili mada zinazoweza kupanua uelewa wao na kusaidia wengine wawe na uelewa zaidi.
Mkuu, mada yako ni elimishi. Achana na wachache wanaokuvunja moyo.
 
Mapinduzi ya siku hizi, ni kupandikiza majasui / Chawa wako, kwenye Serikali, Bunge na Mahakama...
Chawa walikuwa wanapandikizwa tangu miaka ya 1960s sema kwa siku hizi mbinu za kupandikiza zimekuwa za kisasa zaidi kwa sababu ya technology. Alafu human intelligence haitumiki saaana (especially kwa wazungu na sio Africa) kwa sababu ya vifaa vya kunasia mazungumzo (bugs) kuwa bora zaidi ya zile za cold war era.
 
Nenda Bukinafaso ukajifunze huko,maana wao kila baada ya miezi sita wanapindua.

Hata jana walipindua ....
Usituingize kwenye uhaini sisi.
From 1960 to Date Burkinafaso has Conducted 8 Military coups Successful
 
Mada haiongelei kupanga mapinduzi. Unadhani mimi mjinga kiasi gani hadi nilete mada ya namna hiyo? Siheshimu mtu anayekumbatia ujinga kwa visingizio mbalimbali, ikiwemo cha woga. Mimi naitwa MWANANCHI, unajua maana yake? Unadhani jukumu la kulinda nchi ni la jeshi peke yake?

Mada kama hii inaweza kuamsha wahusika wafanye mabadiliko muhimu kwa faida ya usalama wa nchi, kama wakiona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Crap
 
Kuna nafasi ya mbunge teuliwa inakuwa wazi soon, huyu jamaa tunampeleka huko ubalozini kisha tumuhoji kwanini alitaka kumsigina mama akiwa Tanga?
Humo yumo?
Screenshot_20221003-022018.png
 
Back
Top Bottom