Mapya yaibuka ofisa TRA anayedaiwa kujiua hotelini

Mapya yaibuka ofisa TRA anayedaiwa kujiua hotelini

Kufuatia kifo cha ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha, Richard Walalaze aliyedaiwa kujiua kwa kujirusha kutoka ghorofani, familia ya marehemu imeibua mpya baada ya kuuona mwili wake katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Bombo na kufuatilia mahali ulipokutwa mwili huo hotelini.

Familia hiyo imesema haiamini kama kweli alijirusha na kueleza kuwa kifo chake kinatia shaka na kubainisha kuwa imejikuta ikiwa na maswali mengi yasiyo na majibu, hivyo inasubiri taarifa ya uchunguzi wa mwili itakapotolewa na Serikali.

Msemaji wa familia hiyo, kaka wa marehemu, Godfrey Walalaze, ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki amesema hayo akiwa katika Hospitali ya Bombo na kubainisha kuwa mazingira ya kifo cha ndugu yao yanatia shaka iwapo ni kweli alijirusha kutoka ghorofani au la.

"Tumeuchunguza mwili tunapata shaka, sababu ukiacha kovu kichwani, mwili wote hauna mchubuko wala hakuna kiungo chochote kilichovunjika, lakini hata pale hotelini ulipokutwa mwili na michirizi ya damu inatupa maswali mengi mno," alisema Walalaze.

Kitenge Updates
 
RIP na ile nyumba yako nzuri ambayo umetumia miaka 10 kuijenga na kuishi kwa miaka 1 sasa ni mali halali ya wife wako uliyeishi nae miaka 2.
Yatafumuka mengi. Kaka mtu anasema mdogo wake hajawahi kuoa. Wewe wasema kaacha mke aliyeishi naye kwa miaka miwili. Sasa hili linaleta maswali mengi kuhusu nini hasa kilitokea.
 
Gorofa 2 mtu kufa labda Afanye kama anaogelea adive kichwa kitangulieee.. Otherwise its a murder case not suicide sema bongo ndo imeishaa hiyoo!! Na kishindo cha kujitupa hakuna mtu yeyote aliesikia kweli kwa yale mazingira ya ile hotel.
Usipime mzee secondary tulimuwekea dau mkomavu moja aruke ghorofa moja...akatua kwa miguu lakini tulibeba kwenye taxi hadi kwao..
 
Yesu alishanukuliwa kwenye biblia akisema hao wanatangulia:

Mt 21:31 SUV​

Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.
Na sio mtume m au Musa ,hongera

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 

View attachment 2703619


By Burhani Yakub
Tanga. Familia ya Richard Walalaze, ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha aliyedaiwa kujiua kwa kujirusha kutoka ghorofani, imesema haiamini kama kweli alijirusha.

Imeeleza inatia shaka tukio la kifo cha ndugu yao baada ya kuuona mwili wake katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Bombo na kufuatilia mahali ulipokutwa mwili huo hotelini.
Familia hiyo imeeleza kuwa imejikuta ikiwa na maswali mengi yasiyo na majibu, hivyo inasubiri taarifa ya uchunguzi wa mwili itakapotolewa na Serikali.

Msemaji wa familia hiyo, Mchungaji Godfrey Walalaze, ambaye ni kaka wa marehemu alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi, akiwa katika Hospitali ya Bombo.
Alisema mazingira ya kifo cha ndugu yao yanatia shaka iwapo ni kweli alijirusha kutoka ghorofani au la.

"Tumeuchunguza mwili tunapata shaka, sababu ukiacha kovu kichwani, mwili wote hauna mchubuko wala hakuna kiungo chochote kilichovunjika, lakini hata pale hotelini ulipokutwa mwili na michirizi ya damu inatupa maswali mengi mno," alisema Walalaze, ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
Alisema mipango ya mazishi itategemea taarifa za Serikali kuhusu uchunguzi utakapokamilika.

"Tunawaza kufanya mazishi Jumatatu, Mlalo wilayani Lushoto, lakini itategemea na taarifa za Serikali kuhusu uchunguzi wa kifo cha mdogo wangu," alisema Walalaze.

Tukio lake
Habari zilizopatikana juzi na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe, mtumishi huyo alijirusha kutoka ghorofa ya pili ya hoteli ya Ocean Breez jijini hapa usiku wa kuamkia juzi na inaelezwa alikuwa amepanga chumba katika hoteli hiyo tangu Julai 16, mwaka huu.

Mfanyakazi wa hoteli hiyo aliyeomba kuhifadhiwa jina lake, alisema Richard alipanga chumba namba 124 kilichopo ghorofa ya pili kilichokuwa jirani na cha mtumishi mwenzake wa TRA.


Alisema walimtilia shaka Richard kwa kuwa tangu jioni alisikika akizungumza kwa sauti kubwa akiwa chumbani kwake akisema anaogopa.

Alidai mwili wa Richard ulikutwa asubuhi na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi hotelini hapo ukiwa chini usawa wa dirisha la chumba chake, jambo lililoashiria kuwa alijirusha.

“Tulikuta mwili ukiwa na kovu kichwani na damu nyingi. Alikuwa amevaa fulana na jeans. Mlinzi hakueleza kama alisikia kishindo au la…hata sisi hatuelewi nini kilimtokea,” alisema mtumishi huyo.

Alidai tangu alipowasili hotelini hapo alikuwa akisikitika kwamba hana raha, kwa sababu siku chache zilizopita alifiwa na baba yake mzazi na mkewe ambaye ni mjamzito yupo chumba cha wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU).

Hata hivyo, Mchungaji Walalaze alisema mdogo wake hakuwa ameoa wala hakuwahi kuwatambulisha kama ana mchumba.

Kamanda Mwaibambe hakupatikana jana kuzungumzia uchunguzi unaoendelea. Hata hivyo, juzi aliahidi kutoa taarifa utakapokuwa umekamilika.

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Thomas Masese akizungumza na Mwananchi juzi alisema Richard alikuwa miongoni mwa maofisa wa mamlaka hiyo waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu.

Pia soma:
- Tanga: Afisa wa TRA ajirusha ghorofani na kufariki

Credit; MWANANCHI
Miaka 35 Ana ajira hajaoa basi shida
 
By the way hiyo hoteli haina kamera?

Pia huyo mtu ana simu, wanaweza wakatazama simu yake kabla ya mauti kumfika ilikiwa locations zipi, muda upi na duration gani...

Pia kama kajirusha dirishani, wanapaswa wacheck uwepo wa finger prints kila mahali hadi kwenye fremu za madirisha maana kwa mtu anayejirusha lazima walau ashike sehemu ya dirisha n.k

Watazame pattern ya damu, kwa mtu aliyeanguka toka juu muonekano wa dimbwi la damu huwa na pattern yake, ndugu wanaweza wakafanya uchunguzi binafsi pia kwa kuwafikia wale mashahidi wa mwanzo, i believe kuna waliopiga picha...
Hii ndio inaitwa Forensic Investigation?
 
Back
Top Bottom