Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Rhoda Jonathan (46), mkazi wa Kitongoji cha Burunga, Kata ya Uwanja wa Ndege, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, ameripotiwa kuuawa kikatili kwa kukatwa mapanga hadi kufa.
Marehemu alikuwa mke wa Mhandisi Wilson Charles, Meneja wa TARURA - Kagera, ambapo wawili hao wamejaliwa watoto watatu. Imeelezwa Marehemu na mtuhumiwa hawakuwa wakiishi pamoja kwa takriban miaka mitano, lakini walikuwa wakiwasiliana
Tukio hilo lilitokea usiku wa Oktoba 23, 2025, majira ya saa moja na nusu usiku, nyumbani kwa marehemu, ambapo inadaiwa watu wawili waliruka ukuta na kuingia ndani kabla ya kutekeleza mauaji hayo
Mashuhuda walisema mwili wa marehemu ulikutwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali, ikiwemo kiganja cha mkono wa kulia kilichokatwa na kuachwa chini, huku mwili wake ukiwa pembeni ya kitanda na majeraha makubwa kifuani, mdomoni na mikononi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Burunga, James Makuru Marwa, alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti kabla ya kufika eneo la tukio.
Ameeleza kuwa, siku iliyofuata, panga lenye damu lilipatikana jirani na eneo la tukio, na Polisi walilikusanya kwa ajili ya uchunguzi zaidi
Aidha, Kijana aliyekuwa akiishi nyumbani kwa marehemu, Mophati Mwita (14), alieleza kuwa wakati alipokuwa jikoni akipika, mwanafunzi aliyepanga nyumbani hapo alimwona mtu akiruka ukuta na kuingia ndani.
“Yule mtu alimuuliza mwanafunzi kama mama yupo, na ghafla mwanaume mwingine akaingia moja kwa moja hadi chumbani. Shangazi (marehemu) alianza kupiga kelele, mwanafunzi akakimbia kutoa taarifa shuleni”. Alisema alishuhudia watu hao wakiondoka baada ya kufanya mauaji, lakini hakuwatambua
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, amethibitisha kushikiliwa kwa mume wa marehemu kwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo, lililozua mzozo mkubwa kati ya familia za marehemu na mtuhumiwa, ambapo kila familia inataka msiba uwekwe kwao.