MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM


Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​


Haishangazi, ukizingati nukuu ya mkulu, alipokuwa akizindua barabara ya juu, almaarufu kama "fly over" pale Tazara, alisema "Hata Biblia inasema NJOONI KWANGU NINYI WENYE KUELEMEWA NA MIZIGO, NAMI NIPAWAPUMZISHWA; NAMIMI NAWAAMBIA NDUGU ZANGU WA ILE KAMBI, KAMA KUNA ALIYEELEMEWA NA AJE..."

Hivyo huyu naye alionekana kuelemewa kitaaambo!!
 
ahaaaa hivi ndo huyu aliyetupa mashutma kibao kwa yule mkurugenzi mpaka jpm akamshushua mbele za wanainchi au mimi nimechanganya???
Nilimsikia siku ile kwenye mkutano Wa Magu akisema msinizomee na Mimi naweza kuwa mwanaccm
 
haki mmetufanya mazube sana watanzania na vile hatuwezi kuongea mabaya yenu kwa kuhofia ubabe wenu haya endeleeni na nimchezo ya kijinga kutufanya kama misukule...
 
Hakika na Kweli itatamalaki.. Maan kwa sasa hata tusio na kadi ya Chama Chochote Tukisimamia Kweli Tunapewa kadi za Chadema, kwa mantiki hiyo, hawajui hata kesho Chadema ikifutwa, wapinzani watazidi kuongezeka maana Serikali na CCM hawajui wanapambana na Nani zaidi ya Jina La Chama Cha Upinzani tuu.
CHADEMA ya sasa hivi inafukuzana na vivuli tu. Kwa kifupi imepoteana.
Kwasasa CHADEMA ipo sababu upinzani dhidi ya serikali umeimarika sana na wapinzani halisi ni watu, hivyo CHADEMA inaishi kwa kivuli cha upinzani huu lakini wao kama chama na jinsi walivyo dhibitiwa na kubanwa kingekua kimeshajifia kitambo tu.
Ila nguvu watakayoamka nayo, ambayo watapewa na watu wa makundi yote itatisha sana
 
Nawaza tuu, kweli watu tukiamua kuunga juhudi na kusifia, wasifiwa watakubali?
Mkuu mbona unashangaa? Magufuli ni rais mzuri mno,hana kasoro yoyote ile,na Tanzania haitapata rais bora kama Magufuli,tangu aingie madarakani uchumi wa Tanzania umepaa kwa 45%,ajira zimeongezeka kwa 38%, Demokrasia imeshamiri,Uhuru wa vyombo vya Habari umekua,sasa kwa nini wapinzani wasimuunge mkono?
Napendekeza Magufuli atawale milele.
CCM HOYEEEEEEEE......!!!
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​

Magufuli kama alivyojiita mwenyewe kweli ni kichaa amefikia anateka watu wamuunge mkono anaingiza umafia kwenye muhimili.mwingine wa uongozi anachokitafuta kwenye nchi hii atakipata
 
Huyu Marwa Rioba hovyo sana huenda ajitambui..
Hizo juhudi wanazounga mkono ziko wapi..
Majuzi tumeona wanasitisha zoezi la uokoaji/uopoaji, kwa kukosa taa alafu leo anaibuka pimbi mmoja eti anaunga mkono juhudi ,Pumbavu sana.
 
Nitanzania pekee mbunge anajiuzulu na baada ya miez 3 anataka ubunge
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Hawa binadamu wanaoitwa wanasiasa wengi hawana nia njema na vyama vyao, zaidi wanaangalia maslahi yao. Inaumiza na inakera sana kwa wenye nia ya mabadiliko.
 
Walahi

Ni vitu gani huwa wanaunga mkono ?

Salalee!

Hawa watu ni wapuuzi sana....This is another misuse of Public Funds kwa UCHAGUZI HEWA...!!!
Mbunge/Diwani au yeyote kuhamia CCM kwa madai ya kuunga mkono SERA ZA MAGUFULI ni wendawazimu..!!
Hivi nchi hii sana inaongozwa kwa Sera za Magufuli kwerii bamura??? Upinzani upo tangu 1995 kulikuwa na kina Mkapa akaja na Kikwete lakini hatukuwahi kusikia huu ujinga wa mtu kuhamia chama ati kuwuunga mkono Rais....!!!

Watanzania wapenda haki,sheria na Demokrasia alzima tupate Mwarobaini wa ujinga huu ili kukomesha ubazazi huu. Hatuwezi kuwa tunarudia Uchaguzi mara 2 ndani ya kipindi kimoja kwasababu zisizo na mashiko...!!!...Jitu halijafa linajiulu halafu linataka lichaguliwe na watu walewale lirudi Bungeni....Hii si swa hata kidogo!
 
Unaongelea ubunge umesahau uraisi,Lowasa aliingia chadema vuuuu akapewa ugombea uraisi chap chap
Nimeongelea 'uongozi wa kupigiwa kura'. Hujajibu chochote. Akili ipo kwenye uchama tu saa zote; ni kama marobot yaliyokuwa programmed! Awe Lowassa or whatever, unalo jibu?
 
Niliwahi kuandika huko nyuma kwamba Tanzania nchi yangu, Tanzania Nchi yangu, Nakupenda kwa Moyo Wote! Lakini inaangamizwa na ufisadi kwa baadhi yetu kujiita wazalendo. Ebu tufikirie kwa fikra tofauti, au tuone kwa macho tofauti, au tutamke kwa matamko tofauti na kuwa na hisia tofauti: hivi ni kweli hakuna mwenye kuona kwamba huku ni kuchezea bure fedha ya taifa! Kwani kurudia uchaguzi ni bure? Kwamba taifa lenye viongozi wazalendo, hawaoni ufujaji huu wa fedha za umma kwa kisingizio cha kurudia uchaguzi?
Wako wapi viongozi wastaafu wanaoweza kulisemea hili?
Ni awamu ipi tangu tuingie mfumo wa vyama vingi yanatokea haya kwa kigezo cha kuunga mkono kiongozi aliyeko madarakani?
Ni kweli hatuna njia nyingine ya kuunga mkono kazi nzuri ya Rais aliyeko madarakani zaidi ya kujiuzuru ubunge au udiwani ni kusababisha gharama za kurudia uchaguzi?
 
Back
Top Bottom