Walahi
Ni vitu gani huwa wanaunga mkono ?
Salalee!
Nimekuelewa !Hivi wewe unapokaa hapo unaona wanasiasa watz wanakupigania wewe Au maisha yao. Amka wewe.
Hukumsikia Waitara?Mbona wanaohama hawalalamikii internal administration ya chama wanasema sababu kuu ni kuunga mkono ?
Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.
Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.
Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.
Akitangaza kujivua uanachama amesema,
Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.
Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.
VIDEO:
Nilimsikia siku ile kwenye mkutano Wa Magu akisema msinizomee na Mimi naweza kuwa mwanaccm
Yule chizi ?Hukumsikia Waitara?
CHADEMA ya sasa hivi inafukuzana na vivuli tu. Kwa kifupi imepoteana.
Kwasasa CHADEMA ipo sababu upinzani dhidi ya serikali umeimarika sana na wapinzani halisi ni watu, hivyo CHADEMA inaishi kwa kivuli cha upinzani huu lakini wao kama chama na jinsi walivyo dhibitiwa na kubanwa kingekua kimeshajifia kitambo tu.
Ila nguvu watakayoamka nayo, ambayo watapewa na watu wa makundi yote itatisha sana
Mkuu mbona unashangaa? Magufuli ni rais mzuri mno,hana kasoro yoyote ile,na Tanzania haitapata rais bora kama Magufuli,tangu aingie madarakani uchumi wa Tanzania umepaa kwa 45%,ajira zimeongezeka kwa 38%, Demokrasia imeshamiri,Uhuru wa vyombo vya Habari umekua,sasa kwa nini wapinzani wasimuunge mkono?
Napendekeza Magufuli atawale milele.
CCM HOYEEEEEEEE......!!!
Alipokuwa chadema hakuwa chizi? Ha ha ha.Yule chizi ?
Magufuli kama alivyojiita mwenyewe kweli ni kichaa amefikia anateka watu wamuunge mkono anaingiza umafia kwenye muhimili.mwingine wa uongozi anachokitafuta kwenye nchi hii atakipata
Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.
Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.
Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.
Akitangaza kujivua uanachama amesema,
Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.
Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.
VIDEO:
Hawa binadamu wanaoitwa wanasiasa wengi hawana nia njema na vyama vyao, zaidi wanaangalia maslahi yao. Inaumiza na inakera sana kwa wenye nia ya mabadiliko.Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.
Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.
Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.
By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.
Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?
Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Walahi
Ni vitu gani huwa wanaunga mkono ?
Salalee!
kiswahili mkuu, kizuri zaidiWe started this nonsense politics since time in memorial, under CCM regime yet we are nowhere, one of the poorest in the world.
Nimeongelea 'uongozi wa kupigiwa kura'. Hujajibu chochote. Akili ipo kwenye uchama tu saa zote; ni kama marobot yaliyokuwa programmed! Awe Lowassa or whatever, unalo jibu?Unaongelea ubunge umesahau uraisi,Lowasa aliingia chadema vuuuu akapewa ugombea uraisi chap chap