Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Waalimu sita wa shule ya sekondari Makongoro iliyopo wilaya ya Bunda mkoani Mara wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Petro Chisumo (23) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) iliyotolewa leo Agosti 21, 2026 imeeleza kuwa mnamo Agosti 19, 2026 majira ya saa 05:00 asubuhi, wakati mwanafunzi huyo akitekeleza adhabu na wenzake ambao walikua na ufaulu wa chini kwenye mitihani ya kujipima, alichapwa viboko na waalimu hao na kusababisha kuishiwa nguvu hali iliyopelekea kupelekwa hospitali ya wilaya ya Bunda.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakati mwanafunzi huyo akiwa anaendelea na matibabu alifariki dunia na mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo huku sababu za kifo chake zikiendelea kuchunguzwa na zitatolewa mara baada ya madaktari kukamilisha uchunguzi huo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa watulivu kwani Jeshi la Polisi likishirikiana na wataalamu wengine wa taasisi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha kifo cha mwanafunzi huyo.