Mara: Walimu sita wa kidato cha Sita mbaroni kwa mauaji ya mwanafunzi wao

Waalimu sita wa shule ya sekondari Makongoro iliyopo wilaya ya Bunda mkoani Mara wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Petro Chisumo (23) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) iliyotolewa leo Agosti 21, 2026 imeeleza kuwa mnamo Agosti 19, 2026 majira ya saa 05:00 asubuhi, wakati mwanafunzi huyo akitekeleza adhabu na wenzake ambao walikua na ufaulu wa chini kwenye mitihani ya kujipima, alichapwa viboko na waalimu hao na kusababisha kuishiwa nguvu hali iliyopelekea kupelekwa hospitali ya wilaya ya Bunda.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakati mwanafunzi huyo akiwa anaendelea na matibabu alifariki dunia na mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo huku sababu za kifo chake zikiendelea kuchunguzwa na zitatolewa mara baada ya madaktari kukamilisha uchunguzi huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa watulivu kwani Jeshi la Polisi likishirikiana na wataalamu wengine wa taasisi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha kifo cha mwanafunzi huyo.
Aisee
 
Tatizo la Kanda ya ziwa,walioko kidato cha sita ni wake za watu na waume za watu! Umriiiii
 
Sio jambo geni kiivo lakini huo umri ni mkubwa. Mi nlimaliza degree nkiwa na 23. Miaka hii shule wanaanza mapema kidogo.
Mimi miaka 23 ndiyo Namaliza PhD na Siyo hizi PhD za sijui za Jalalani University. Ni Imperial college, Sillwood Park, London
 
Najaribu kuvaa viatu vya hao waalimu sasa..dah..wametoka nyumbani salama na wakijua wanarudi salama..mikosi gani hii jamani😭
 
Nilikuwa nafundisha shule ya private primary, kuna mtoto akaniudhi sana nikamchapa kiboko kimoja!

Aisee yule mtoto alidondoka chini kama kazimia, akaanza kuhema kwa shida huku akipiga piga Miguu!

Niliogopa kinoma alipokaa sawa, nilisema sitakuja kuchapa mtoto wa mtu tena. Nasikuwahi kuchapa tena mpaka nilipoacha kufundisha!
 
Painful

waalimu wanastress sana kimaisha
Hasira zao wanazihamishia kwa wanafunzi,tunajuwa wanafunzi kweli wapo wanao kera,nidham sifuri
Lazima walimu waji control
La sivyo watajaa huko majela

Ova
 
Ukiondoa mwalimu wangu mmoja ninayemkubali wengine wote washenzi sana ikiwemo na hao waliomuua mwanafunzi.Hasira zao za maisha wanahamishia kwa wanafunzi.
 
Form 6 unachapwa?
Binafsi nimesoma advance hakuna mwalimu aliyenichapa
Anyway apumzike Kwa Amani
 
Back
Top Bottom