Mara: Walimu sita wa kidato cha Sita mbaroni kwa mauaji ya mwanafunzi wao

Mara: Walimu sita wa kidato cha Sita mbaroni kwa mauaji ya mwanafunzi wao

Waalimu sita wa shule ya sekondari Makongoro iliyopo wilaya ya Bunda mkoani Mara wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Petro Chisumo (23) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) iliyotolewa leo Agosti 21, 2026 imeeleza kuwa mnamo Agosti 19, 2026 majira ya saa 05:00 asubuhi, wakati mwanafunzi huyo akitekeleza adhabu na wenzake ambao walikua na ufaulu wa chini kwenye mitihani ya kujipima, alichapwa viboko na waalimu hao na kusababisha kuishiwa nguvu hali iliyopelekea kupelekwa hospitali ya wilaya ya Bunda.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakati mwanafunzi huyo akiwa anaendelea na matibabu alifariki dunia na mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo huku sababu za kifo chake zikiendelea kuchunguzwa na zitatolewa mara baada ya madaktari kukamilisha uchunguzi huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa watulivu kwani Jeshi la Polisi likishirikiana na wataalamu wengine wa taasisi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha kifo cha mwanafunzi huyo.
Walimu hamkomi tu. Mwanafunzi kuchapwa viboko tu lazima mkuu wa shule atoe kibali. Sasa wanakwenda kupoteza muda mahabusu au kifungoni kabisa
 
Wabinywe pumbu haswaa. Tumechoka ujinga.

Kama una stress za vikoba acha kazi, usimalizie hasira zako kwa watoto.

Shenzi sana nimechafukwa haswa mpaka nimekunja ndita.

I WISH I COULD BE IGP.

Cc: Dr. Mariposa binti kiziwi Kalpana
Hao mbona safari yao ishaishia hapo, wanaenda kuozea jela,
Natamani adhabu ya kuchapwa mijeledi kama enzi za utumwa irudi, ilipaswa hao wapuuzi wavuliwe nguo zote watandikwe mijeledi iliyopakwa chumvi na pilipili wausikie utamu wa kuchapa watoto wa watu kabla hawajarushwa jela,

Pumbavu kabisa.
 
School candidate kabisa!!
Uzushi! Kuna age limit ya admission kwa kila level - pre-primary, primary, o-level, a-level. Out of that, sit as private candidate.

How comes kibabu cha 32 uliruhusiwa kuchangamana na watoto wadogo? Walioruhusu have case to answer!
 
Uzushi! Kuna age limit ya admission kwa kila level - pre-primary, primary, o-level, a-level. Out of that, sit as private candidate.

How comes kibabu cha 32 uliruhusiwa kuchangamana na watoto wadogo? Walioruhusu have case to answer!
Inawezekana mkuu usilete ubishi, private school hawana masharti hayo kigezo cha kujiunga form five ni uwe na cheti cha form four hata kama hiyo form four ulimalimaliza miaka 15 iliyopita.
 
Tukisema adhabu za viboko hazifai wajinga wanatetea. Kwanza unamchapaje mtu ana miaka 23! Si kudhalilisha utu wake kabisa.
 
Kazi ya ualimu ni ngumu sana ukiichukulia kwa uzito. Walichokifanya hao walimu huwa kinafanyika kwenye shule nyingi za serikali kote nchini. Sema wao wamekutwa na siku mbaya kazini.
 
Hao walimu hawakutumia akili tu
Kijana ana miaka 23 halafu ufaulu hafifu huenda tayari ana majukumu ya mpenzi au watoto hata wazazi.
Kimsingi huo umri kwa miaka hii tayari ameshamaliza chuo yupo home akiwa na mishe zake..
Walimu punguzeni wenge mtaishia jela na wake zenu kutafunwa kavukavu.
 
Eeh viboko ndiyo mbinu ya kufaulu?ila madogo wa siku hizi jau sanaa,form 6 unapigwa mpaka unaishiwa nguvu?Enzi zetu hapo ngumi zishalika sanaa.
NAKUMbUKA 1992 nilishapigana na mwalimu wille, girdasaida na shayo Arusha sec kwa dk 42 mpaka na wao walikaa chini tukaanza kuulizana utarudia kunipiga na wao wananiuliza utarudia kugombana na walimu tuliulizana kama mara 5 wakaniachia nenda zako na ndo mwisho wa fimbo kuanzia form five mpaka namaliza six , siku ya graduation form six nikapewa zawadi ya mwanafundi mwenye nidhamu na mtiifu ahaaaa kumbe waliona aibu sana maaana story zilisambaaa mno hadi shule za bondeni, arusha day, nilikuwa naitwa ngumi jiwe na nilikuwa na bahati nina mwili kubwa na pumzi sana
 
Hao walimu hawakutumia akili tu
Kijana ana miaka 23 halafu ufaulu hafifu huenda tayari ana majukumu ya mpenzi au watoto hata wazazi.
Kimsingi huo umri kwa miaka hii tayari ameshamaliza chuo yupo home akiwa na mishe zake..
Walimu punguzeni wenge mtaishia jela na wake zenu kutafunwa kavukavu.
umenena kweli
 
Duhh miaka 23 bado upo shule na viboko unachapwa mtihani
 
Kuna haja ya wakufunzi na walimu wakongwe kufundisha walimu wapya namna ya kutoa adhabu kwa wanafunzi wao watovu wa nidhamu/wakorofi. Hawa watoto wa miaka hii ni wadhaifu sana hawahimili adhabu, kuwaadhibu kwa mtindo wa kizamani walimu wataishia jela kwa mauaji. Ni kuacha kabisa adhabu ya kuchapa/kipigo. Mwanafunzi mkorofi/mtundu ni kumtimua atoke darasani tu aende bwenini au kumfukuza shule kwa muda akajutie makosa yake. Kama vipi mwalimu unatoka darasani hufundishi kipindi na kuwaachia msala wanafunzi washughulike na mwenzao mtukutu. Ukisema uchape unaweza kuua, hawa watoto wa sasa ni dhaifu sana tofauti na wa zamani unatandika mtu fimbo za kutosha lakini hadhuriki
 
Ila Walimu hasa shule za Gvt sijui wanakumbwa na nini? Stress? Depression? Mental health? Au nini?
Duuh.
 
Back
Top Bottom