Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
AiseeWaalimu sita wa shule ya sekondari Makongoro iliyopo wilaya ya Bunda mkoani Mara wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Petro Chisumo (23) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) iliyotolewa leo Agosti 21, 2026 imeeleza kuwa mnamo Agosti 19, 2026 majira ya saa 05:00 asubuhi, wakati mwanafunzi huyo akitekeleza adhabu na wenzake ambao walikua na ufaulu wa chini kwenye mitihani ya kujipima, alichapwa viboko na waalimu hao na kusababisha kuishiwa nguvu hali iliyopelekea kupelekwa hospitali ya wilaya ya Bunda.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakati mwanafunzi huyo akiwa anaendelea na matibabu alifariki dunia na mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo huku sababu za kifo chake zikiendelea kuchunguzwa na zitatolewa mara baada ya madaktari kukamilisha uchunguzi huo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa watulivu kwani Jeshi la Polisi likishirikiana na wataalamu wengine wa taasisi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha kifo cha mwanafunzi huyo.
Tatizo la Kanda ya ziwa,walioko kidato cha sita ni wake za watu na waume za watu! UmriiiiiWaalimu sita wa shule ya sekondari Makongoro iliyopo wilaya ya Bunda mkoani Mara wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Petro Chisumo (23) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) iliyotolewa leo Agosti 21, 2026 imeeleza kuwa mnamo Agosti 19, 2026 majira ya saa 05:00 asubuhi, wakati mwanafunzi huyo akitekeleza adhabu na wenzake ambao walikua na ufaulu wa chini kwenye mitihani ya kujipima, alichapwa viboko na waalimu hao na kusababisha kuishiwa nguvu hali iliyopelekea kupelekwa hospitali ya wilaya ya Bunda.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakati mwanafunzi huyo akiwa anaendelea na matibabu alifariki dunia na mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo huku sababu za kifo chake zikiendelea kuchunguzwa na zitatolewa mara baada ya madaktari kukamilisha uchunguzi huo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa watulivu kwani Jeshi la Polisi likishirikiana na wataalamu wengine wa taasisi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha kifo cha mwanafunzi huyo.
We ni polisi sio ajabu 😂Ni jambo geni kwako? Mie form six nimemaliza nikiwa na miaka 32.
Mimi miaka 23 ndiyo Namaliza PhD na Siyo hizi PhD za sijui za Jalalani University. Ni Imperial college, Sillwood Park, LondonSio jambo geni kiivo lakini huo umri ni mkubwa. Mi nlimaliza degree nkiwa na 23. Miaka hii shule wanaanza mapema kidogo.
Niliunga unga sio ili niajiriwe mie nachukia sana kuajiriwa napga mishe zangu na ni mwanasiasa.We ni polisi sio ajabu 😂
Huwa mnaunga unga mwana sana.
Ndio maana unatetea wauaji.Niliunga unga sio ili niajiriwe mie nachukia sana kuajiriwa napga mishe zangu na ni mwanasiasa.
Kwamba walimu walioua huyo dogo wa 23 years nimewatetea?Ndio maana unatetea wauaji.
Hasira zao wanazihamishia kwa wanafunzi,tunajuwa wanafunzi kweli wapo wanao kera,nidham sifuriPainful
waalimu wanastress sana kimaisha
Dahhhhhhhhh!!! Apumzike kwa amani