Mara ya kwanza nakanyaga Kigoma na niliyoyaona huko

Mara ya kwanza nakanyaga Kigoma na niliyoyaona huko

Baada ya kufika Kigoma nikakaa siku kama ya 3 hivi nikasema niende mjini , nikaenda barabarani Buzebazeba ( ndo nilipofikia), ilikuwa jioni , nikagundua kumbe

1. Kigoma hakuna foleni barabarani.

2. Hakukuwa na dalalada za mjini kama huku Bali Kuna vibajaji.

Basi nikapanda kibajaji , njiani namwambia dereva

"Vipi hakuna foleni , tutawahi kufika".

Dereva akanishangaa😅, akanambia "huku hakunaga foleni", nikasema "weee, kumbe". Baada ya dakika kadhaa kweli tukawa tumefika Kigoma mjini ( mwisho wa reli).

3. Watoto wa kule ni wakubwa tofauti na umri wao.

Pale kwa wenyeji wetu kulikuwa na Wasichana , ukiwaangalia mimi na wao tulikuwa kimo sawa na wengine walinizidi , kumbe bhana ni vitoto😅 ila miili mikubwa.

Nilijua hayo siku alipokuja mtoto wa mwenyeji wetu kutuona, wakati wa maongezi ndo akataja umri wake , miaka 16 , ukimwangalia sasa huyo msichana wa miaka 16 na mimi wakati huo 21 heee!! Yeye mkubwa mimi mdogo. Nikaulizia na wale wengine eti miaka 15, 16, 17 hakuna 18 , duuh!! Nikasema tembea uone.

4.Samaki fresh kutoka baharini zinanenepesha.

Ndani ya mwezi mmoja wa kukaa hapo nguo nilokuja nazo zikawa ndogo, zinanibana nimefutuka balaa, nikafanya udadisi bhanaa, kumbe ni zile samaki( migebuka) inatoka Moja kwa moja baharini tunaila ikiwa fresh ndo inatunenepesha, kwahiyo vile vitoto vinanenepeshwa na migebuka na marumbu.

5. Mzunguko mdogo wa pesa miaka nenda miaka rudi.

Kumbe ndomna waha wanang'ang'ania dar, kgma mzunguko wa pesa upo taratiibu sanaa, dar unaweza kuishi kwa kuuza barafu na ice cream sio kigoma, unamuzia nani!?.

6. Wanawake ndo watafutaji kwa asilimia kubwa.

Kila utakapokatiza unakutana na wanawake na mashuka Yao, hata wakiwa kwenye mikutano wapo nayo, masokoni ndo usiseme wamejaa, waume zao wapo kwenye vijiwe vya kahawa wanajadili ACT wazalendo, akirudi akute ugali umeiva.

7. Wanaume wa gungu ni wajuaji kuliko sehemu zingine.

Yaani wanaume wa gungu unaweza ukabishana nao mpaka asubuhi bila kuchoka, Kila kitu wanajua wao, hakuna wasichokijua.

Ni mji Mzuri kwa kupumzisha akili ila kimaisha mgumu sana.

Najipanga nirudi tena.
nitatembelea kigoma nile hao "samaki fresh toka baharini mkuu"
 
Umenikumbusha nilipoenda kikazi kigoma kutoa mkono wa kwaheri kwa watu tuliokuwa tunafanya nao kazi za utafiti, Kasulu a lovely place, Kitimoto inauzwa kwenye vibanda kama vya huduma za kifedha, asubuhi unakutana na supu ya migebuka na mihogo mchemsho. Kule kwa kina Mzamiru kunaitwa matyazo wale waha wanaoishi kule jeuri sana, wajivuni sana na ukiwauliza kwann wanakuwa wajeuri wanadai eti sababu airport ya kwanza ilikuwa hapo 🤣🤣

Mkuu kama ulienda kigoma na hujapanda mchomoko "Toyota pro box" basi bado hujafurahia kigoma vizuri, mbele mnakaa abiria wawili, nyuma mnakaa 6 afu kwenye boneti wanajaza madumu ya mawese kama 50 hivi, kuingia na kutoka kigoma ni lazima kitambulisho au barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa, kila baada ya kilometre kadhaa kuna block askari wanakagua watu vitambulisho.

Buhigwe na kibindo sio sehemu za kuishi zile, mzunguko wa pesa ni mdogo sana.

Wakati naenda barabara ya lami kutoka kigoma to kasulu ndio ilikuwa kwenye hatua za mwisho mwisho kumaliziwa na kasulu to kibondo ilikuwa hata mpango wa kujengwa hakuna, nadhan hizo wilaya mbili kwa sasa zitakuwa zimeunganishwa kwa lami.


Mulukoyoyo guest tulivamiwa na askari usiku wa manane tulitwanga maswali ya kijinga sana, Rushwa kwa askari hapo ni nje nje.

Kigoma saa moja na dakika 45 jioni ndio jua linazama kabisa na saa 11 alfajiri ni kama saa nane ya usiku.

Siku narudi waha walianza kubisha kuanzia geita hadi morogoro, waha ubishi upo kwenye damu yao
Barabara lami almost imekamilika imebaki kipande kidogo kama cha km 20 Kibondo to Kasulu.

Buhigwe sababu ya namba 2 imeanza kukua na watu wameanza kuwekeza.
 
Kigoma mtu ufike ujionee mwenyewe.. kuna stories zinaongelewa nje ya Kigoma kuhusu Kigoma hazina hata ukweli.

Nilifika Kigoma nikaiona kwa macho na kuwaona wenyeji wa mkoa husika.
 
Kigoma mtu ufike ujionee mwenyewe.. kuna stories zinaongelewa nje ya Kigoma kuhusu Kigoma hazina hata ukweli.

Nilifika Kigoma nikaiona kwa macho na kuwaona wenyeji wa mkoa husika.
Stori kama zipi sio za kweli!?.
 
Kule hakuna pisi kali ukiona shepu zao ni kama wanapiga chafya na vichwa km wabondwa matofali , uzuri ni wavumilivu sn kwenye ndoa ni wife material..
Weeeee nani kasema kigoma hakuna pisi kali!? Wamejaa telee
 
kwa hawa waha ambao wamemeza mbegu za sidiko warefuke lakin mbolea haikufanya kazi vifupi kama mitungi ya gesi maybe uliona waha wa burundi na congo
 
Wimbo la wahamiaji toka mikoa ya shinyanga na mwanza hususani wasukuma wanaotumia wanyamakazi kwa ajili ya kilimo wameongeza uzalishaji wa chakula mara dufu km zao la Mpunga.
 
kwa hawa waha ambao wamemeza mbegu za sidiko warefuke lakin mbolea haikufanya kazi vifupi kama mitungi ya gesi maybe uliona waha wa burundi na congo
Kwani mnadhani waliopo kigoma wote ni Waha!? Jpo makabila mengi.
 
Back
Top Bottom