Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanangu unapenda sana safari, iv Mullers uliendaga?Deluxe bado ina operate?
Kitendo cha kuuliza kigoma kuna foleni inaonekana hata details ndogondogo za nchi yetu huzijuiBaada ya kufika Kigoma nikakaa siku kama ya 3 hivi nikasema niende mjini , nikaenda barabarani Buzebazeba ( ndo nilipofikia), ilikuwa jioni , nikagundua kumbe
1. Kigoma hakuna foleni barabarani.
2. Hakukuwa na dalalada za mjini kama huku Bali Kuna vibajaji.
Basi nikapanda kibajaji , njiani namwambia dereva
"Vipi hakuna foleni , tutawahi kufika".
Dereva akanishangaa😅, akanambia "huku hakunaga foleni", nikasema "weee, kumbe". Baada ya dakika kadhaa kweli tukawa tumefika Kigoma mjini ( mwisho wa reli).
3. Watoto wa kule ni wakubwa tofauti na umri wao.
Pale kwa wenyeji wetu kulikuwa na Wasichana , ukiwaangalia mimi na wao tulikuwa kimo sawa na wengine walinizidi , kumbe bhana ni vitoto😅 ila miili mikubwa.
Nilijua hayo siku alipokuja mtoto wa mwenyeji wetu kutuona, wakati wa maongezi ndo akataja umri wake , miaka 16 , ukimwangalia sasa huyo msichana wa miaka 16 na mimi wakati huo 21 heee!! Yeye mkubwa mimi mdogo. Nikaulizia na wale wengine eti miaka 15, 16, 17 hakuna 18 , duuh!! Nikasema tembea uone.
4.Samaki fresh kutoka baharini zinanenepesha.
Ndani ya mwezi mmoja wa kukaa hapo nguo nilokuja nazo zikawa ndogo, zinanibana nimefutuka balaa, nikafanya udadisi bhanaa, kumbe ni zile samaki( migebuka) inatoka Moja kwa moja baharini tunaila ikiwa fresh ndo inatunenepesha, kwahiyo vile vitoto vinanenepeshwa na migebuka na marumbu.
5. Mzunguko mdogo wa pesa miaka nenda miaka rudi.
Kumbe ndomna waha wanang'ang'ania dar, kgma mzunguko wa pesa upo taratiibu sanaa, dar unaweza kuishi kwa kuuza barafu na ice cream sio kigoma, unamuzia nani!?.
6. Wanawake ndo watafutaji kwa asilimia kubwa.
Kila utakapokatiza unakutana na wanawake na mashuka Yao, hata wakiwa kwenye mikutano wapo nayo, masokoni ndo usiseme wamejaa, waume zao wapo kwenye vijiwe vya kahawa wanajadili ACT wazalendo, akirudi akute ugali umeiva.
7. Wanaume wa gungu ni wajuaji kuliko sehemu zingine.
Yaani wanaume wa gungu unaweza ukabishana nao mpaka asubuhi bila kuchoka, Kila kitu wanajua wao, hakuna wasichokijua.
Ni mji Mzuri kwa kupumzisha akili ila kimaisha mgumu sana.
Najipanga nirudi tena.
Hata burundi ziwa wanaita bahariWenyewe ndo wanavyoita, hawasemi ziwani Bali baharini
Angejaribu kusogea soko la Sofiya ajionee.Kasulu hakuna chakula mmhh?
Kabsaa uwe na hesabu Kamili ya nini ufanye lasivyo hata nauli utakosa ya kurudi ulipotokaMikoani kuna biashara zake za kufanya. Usikurupuke tu kisa ulikua unauza nguo Dar zinatoka uende na Simiyu ukiwa na matarajio yaleyale utakula chuma.
Mkoani ni sehemu unayotakiwa utumie akili sana kuliko hata Dar ndio upate hela.
Ndio maana ukienda Njombe hapo utakuta vijana wadogo tu wana pesa za kutosha na hawana maduka ya nguo wala vyombo.
Ni sehemu 3 tofautiBaharini / ziwani / mtoni
Uganda ya wapi?Yeah Sina hakika kwakua sikukaa sanaa lakini ndo nimesema pengine maana kule kasulu naskia wamepakana na Uganda Kwahy huenda biashara ikawa changamfu maana nilinunua vitu kwa bei Chee tofauti na kigoma mjini.
KIGOMA KUNA BAHARI?Baada ya kufika Kigoma nikakaa siku kama ya 3 hivi nikasema niende mjini , nikaenda barabarani Buzebazeba ( ndo nilipofikia), ilikuwa jioni , nikagundua kumbe
1. Kigoma hakuna foleni barabarani.
2. Hakukuwa na dalalada za mjini kama huku Bali Kuna vibajaji.
Basi nikapanda kibajaji , njiani namwambia dereva
"Vipi hakuna foleni , tutawahi kufika".
Dereva akanishangaa😅, akanambia "huku hakunaga foleni", nikasema "weee, kumbe". Baada ya dakika kadhaa kweli tukawa tumefika Kigoma mjini ( mwisho wa reli).
3. Watoto wa kule ni wakubwa tofauti na umri wao.
Pale kwa wenyeji wetu kulikuwa na Wasichana , ukiwaangalia mimi na wao tulikuwa kimo sawa na wengine walinizidi , kumbe bhana ni vitoto😅 ila miili mikubwa.
Nilijua hayo siku alipokuja mtoto wa mwenyeji wetu kutuona, wakati wa maongezi ndo akataja umri wake , miaka 16 , ukimwangalia sasa huyo msichana wa miaka 16 na mimi wakati huo 21 heee!! Yeye mkubwa mimi mdogo. Nikaulizia na wale wengine eti miaka 15, 16, 17 hakuna 18 , duuh!! Nikasema tembea uone.
4.Samaki fresh kutoka baharini zinanenepesha.
Ndani ya mwezi mmoja wa kukaa hapo nguo nilokuja nazo zikawa ndogo, zinanibana nimefutuka balaa, nikafanya udadisi bhanaa, kumbe ni zile samaki( migebuka) inatoka Moja kwa moja baharini tunaila ikiwa fresh ndo inatunenepesha, kwahiyo vile vitoto vinanenepeshwa na migebuka na marumbu.
5. Mzunguko mdogo wa pesa miaka nenda miaka rudi.
Kumbe ndomna waha wanang'ang'ania dar, kgma mzunguko wa pesa upo taratiibu sanaa, dar unaweza kuishi kwa kuuza barafu na ice cream sio kigoma, unamuzia nani!?.
6. Wanawake ndo watafutaji kwa asilimia kubwa.
Kila utakapokatiza unakutana na wanawake na mashuka Yao, hata wakiwa kwenye mikutano wapo nayo, masokoni ndo usiseme wamejaa, waume zao wapo kwenye vijiwe vya kahawa wanajadili ACT wazalendo, akirudi akute ugali umeiva.
7. Wanaume wa gungu ni wajuaji kuliko sehemu zingine.
Yaani wanaume wa gungu unaweza ukabishana nao mpaka asubuhi bila kuchoka, Kila kitu wanajua wao, hakuna wasichokijua.
Ni mji Mzuri kwa kupumzisha akili ila kimaisha mgumu sana.
Najipanga nirudi tena.
Huyu alipita akiwa kwenye gari hakutembeaAngejaribu kusogea soko la Sofiya ajionee.