Mara yangu ya kwanza kukutana na malaika(1987)

Yaani hawa Malaika nimewasika weeee!! tangu nikiwa na miaka 13 na sasa ni mtu mzima nimejitahidi weeee niwaone wapi lkn bado mnanitamanisha mweee!!...skia David siku akija huyo Malaika mwambie nime mmiss sana yaani mie nimuone tu!!
Malaika ni kweli na Mungu ni kweli. Kimsingi ili uweze kuona inategemea na mahusiano yako na Mungu. Kutoka moyoni na nikiwa na dhamiri njema moyoni mwangu, nimewaona na kuwahisi malaika wawili. Nitaleta ushuhuda wangu juu ya Yesu, Malaika na Shetani. Hao wote nimeshawahi waona. Malaika ni kweli, zaidi ya miezi 6 nilikuwa nawaona na nahisi uwepo wao maishani mwangu.
 
Jesus Christ !

Endelea mtu wa Mungu!

Nahitaji kuonana nawe ana kwa ana you have something big to share with me!
Kasome biblia takatifu ndio muongozo wa Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Lakini haya anayoyaandika hapa si ya Mungu aliyeziumba mbing na nchi. Shetani huwa anajifanya naye ni malaika wa nuru na kukuletea porojo nyingi kama hizo na kama huna neno la Mungu atazidanganya fikra zako. Mwaka 2019 nilikuwa nataka kujifunzakutofautisha sauti ya Mungu na sauti ya shetani. Siku moja nilimsikia akiongea nami kwenye ndoto na alianza na maneno kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu akamalizia amina. siku ya pili asubuhi niliisika sauti yake nikiwa macho aliongea kwa kebehi sana. sikatai kuwa viumbe kutoka mbinguni kukutana na wanadamu maana mimi pia nimeshakutana nao lakini utawatambuaje hawani kundi la Mungu na hili ni kundi la shetani? uwe na neno la Mungu vinginevyo utapotezwa tu. ndiyo maana Mungu alitupa biblia takatifu iwe muongozo wetu tusipotee kwa udanganyifu wa shetani kama mfano wa huu.

2 Kor 4:3-4 SUV​

Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

2 Kor 11:14 SUV​

Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
 
Daaa! sawa bana ila nakuonea Gele sana!! but uendelee ivoivo!! ...utaona meengi zaidi!!! ila kuna waleee! watoto wa Shetani hawatakulewa!! kwa sababu Biblia imeandika Mwanamke ni Mama wa viumbe vyote!! sasa wale viumbe wa upande wa pili wa mwanamke hawajuagi kitu!.....

Naamini hii ni zaidi ya utajiri!
 
natamani kujua kama ww ulifunuliwa huo mwanga toka mwaka 1987
hadi sasa na ulisoma HAPO ilboru ww ni nani kwa sasa hapa nchini
un autajiri wa kiasi na umefanikiwa vp kuhusu mwanga uliopata toka huo....??
 
Malaika amekuambia nini kuhusu vita ya Urusi na Ukraine?
 
Ulianza kuvuta bange ukiwa na umri Gani?
Bange mbaya
 
duh
 
Soma post zake za mwishoni utamwelewa. Hanamini kwamba hakuna lolote linaloweza kumshinda MUNGU, na kwamba kuna mambo MUNGU hawezi kufanya ikiwemo kutibu baadhi ya magonjwa. Anaamini God's power is limited.Period
Hebu jaribu kwanza kumuelewa mtoa Uzi, tatizo umekuja na negativity Kabla hujaunganisha dots, kwani kila ulichofundishwa wewe katika mambo ya Imani ni kweli 100%? Tulipoambiwa ombeni nanyi mtapewa tafteni nanyi mtapata maana yake ili yatimie hayo nikwamba, vyakutaftwa vitaftwe kweli na vya kuomba viombwe kweli, siyo uombe vinavyostahili kutaftwa Wala usitafte vinavyostahili kuombwa. Nikweli kunabaadhi ya mambo Mungu hujitenga pembeni si kwamba hawezi kuyatatua.
 
Bangi za kuvutia chooni ni hatari sana. Zinaweza kukusababisha siku moja umuone na shetani na ndo ukichaa unaanzia hapo. C ajabu ulikula msuba weeee, ili msuli ukae sawa. Msela kaja kukuchek class ukamuona kama malaika uliyekua unamuwaza.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Humu kila mtu anamapokeo yake mkuu, wewe unaweza usiyapokee vyema ila kunawengine wanayapokea vyema, nibora mkamuacha mtoa Uzi amalize mje na conclusion nzuri. Mfano kipindi shetani hajamuasi Mungu kulikuwa na machafuko? Maana yake machafuko yalianza baada ya wao kutofautiana hivyo wakiungana tena wakaelewana lazima amani iwepo, pia ugomvi alionao Mungu kwa shetani yawezekana ni mdogo mno kuliko sisi tunavyojua, kwanini Mungu hakumwangamiza mara moja tu akapotea ila akamruhusu atusumbue sisi ambao hatukuwa na hatia yoyote, pia Mungu aliamua kumtoa sadaka mwanae wakati anauwezo wa kummaliza adui yake tena kwa sekunde tu.
 
Ulichokiandika kina reflect your thinking capacity.
 
Yesu alipojaribiwa na Ibilisi alisema...IMEANDIKWA. Je, biblia inasemaje kuhusu wafu? Hawajui lolote.

Pia tambua kuwa shetani hujibadili na kuwa kama malaika wa nuru. Tambua shetani ni mwenye sura nzuri na hiyo sura bado anayo, ila michoro mibaya inayochorwa kumwakilisha ni uzushi.

Kuwa makini na mapepo. Utayatambua kwa neno la Mungu pekee. Imeandikwa.
 
Sura ya yesu inaijua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…