Watu wanatafuta maisha baada ya kifo. Kabla ya kuzaliwa na baada ya kufa, hakuna mtu anayeweza kumweleza mwingine. Maana kabla ya kuzaliwa experience ya maisha ni tofauti na sasa. Kila mmoja yupo na namna yake ya kueleza.
Lakini cha kujiuliza ni nini maana ya maisha!? Kama tunaongelea maisha kabla ya kuzaliwa au baada yakufa, na tunaleta tafsiri ya maisha ni kuvuta pumzi, kula, kuvaa na kustarehe, basi kabla ya kuzaliwa na baada ya kufa hakuna maisha.
Mtu anapozaliwa, anapoanza kupata elimu ya dunia huanza kufanya utafiti wa kujua mambo mbalimbali. Kuna vitu atajaribu kuvifanya, vingine vitamletea matokeo hasi. Je, ni nini maana ya mtoto kutafuta kujua kila kitu!? Ni kwamba anataka kujua experience ya existence yake mpya.
Watu wanauliza na wanatamani kujua baada ya kifo kuna maisha!? Kwa tafsiri ya ulimwengu wa mwili na tamaduni za ulimwengu wa mwili, mtu akifa maisha ndio yameishia hapo. Kumbukumbu ya kila mtu imetunzwa kwenye memory yake. Nasema sasa mtu yupo na aina mbili ya memory:-
Temporary Memory na
Inherited Memory
Hizi zote zipo kwenye mwili.
Sasa basi tunapoishi katika ulimwengu wa mwili ni vyema tukajua hakuna thawabu utakayopewa kokote kwa matendo ya mwili. Maana mshahara wa matendo ya mwili hutimizwa kwa matendo ya mwili. Hakuna kumbukumbu itakayobaki popote na kukufaidisha kutokana na matendo ya mwili. Baada ya kifo kumbukumbu za mambo ya mwili hubaki katika ulimwengu wa mwili.
Hakuna taarifa ya matendo ya mwili itakayokupatia thawabu kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa. Mtu hujishuhudia mwenyewe na kutengeneza ulimwengu wake mwenyewe. Ndipo sasa mwenye ufahamu afahamu haya; mtu anajishuhudia mwenywe, mtu anatengeneza ulimwengu wake mwenyewe, yeye anakuwa mfalme, anakuwa Mungu na anakuwa muumbaji mwenyewe.
Sasa basi kama imani ya mwingine inakuudhi, ni bora ukajitenga naye ukawa mbali naye ili uweze kujifurahisha mwenyewe. Furaha yako hapa duniani unaijenga mwenyewe.
Mwenye ufahamu afahamu hayo....