Haya mambo ni halisia kabisa.
Kwa mara ya kwanza Mwaka 2012 nikiwa chuo mwaka wa pili tulikuwa na huduma ya kuhubiri Mangaka Mtwara nikiwa katika hali ya utulivu mkubwa,nimejawa hali ya upendo kwa watu wote yaani niliomba msamaha wa kweli kwa watu wote nilio wakosea pia nikawasamehe watu walionikosea,kwakifupi nilikuwa huru sana.
Ulikuwa usiku wa saa sita nikiwa katika hali ya maombi,nilitokewa na mtu ambaye sijawahi muona kabla akiwa amevalia mavazi meupe na amejaa hali ya upendo usio kifani,ki ukweli nilijisikia amani ya moyo ambayo sijawahi iona kabla.Kwasauti ya upendo aliniambia fanya kazi yangu.
Kwakweli kesho yake tulikuwa na huduma ya kuwaombea watu mbalimbali wenye shida nilikuwa na nguvu ambayo sijawi kuwa nayo kabla,ilifika hatua hata kwa kumpulizia pumzi mtu aliyekuwa na nguvu za giza na alifunguliwa wakati huohuo.Niliogopa kiasi kwani awali nilikuwa siamini kuwa hayo mambo yanawezekana.
Nilichojifunza kutoka mwaka ule, ili uweze kuwasiliana na Mungu kupitia malaika wake kwa njia ya Yesu Kristo,inahitaji uwekezaji wa hali ya juu,vitu muhimu unavyotakiwa kuwa navyo ni;
1.Upendo wa kweli yaani uwasamehe watu wote walio kukosea pia omba msamaha kwa watu walio kukosea(Moyo usio na mawaa )
2.Tenga mda wa kuongea na Mungu wako na nguvu iliyoko ndani yako...hakuna jambo kubwa au zuri linalo patikana kirahisi rahisi.
3.Sehemu kubwa ya maombi yako iwe kuwaombea watu wengine wenye uhitaji mfano wagonjwa,masikini,yatima,wajane na watumishi yaani wachungaji,mapadre,mashehe wanaofanya kazi zao katika mazingira magumu.
4.Kuwa mnyenyekevu.
Nguvu za Mungu zipo, changamoto kubwa ni sisi kuwa na mambo mengi ndani ya mioyo yetu ambayo ni vigumu kutukutanisha na nguvu za Mungu na Mungu mwenyewe mfano,wivu,fitina,kukosa upendo, ubinasfi,zaidi ya yote kuchukia mafanikio ya watu wengine.