Mara yangu ya kwanza kukutana na malaika(1987)

Sijaja kibiblia mkuu, huo mstari ni maana ya Imani, ni katika kuthibitisha hoja yangu wala sio katika kuanzisha mabishano.
 
Baada ya hayo sasa naomba nitoe somo kidogo

IMANI
Katika ulimwengu wetu wa mwili, hakuna namna ya kuweza kuishi pasipo imani. Maisha yetu ya kila siku yanategemea imani.

Imani ipo katika viwango na madaraja tofauti tofauti. Kuna imani inajegwa kutokana na mazoea ya tamaduni kadha wa kadha. Lakini vilevile kuna imani inayojengwa kutoka ndani ya mtu. Pia kuna imani inajengwa kutokana na kusikia taarifa fulani.

Imani inaweza kukusogeza kwenye kuangazia na vilevile imani hiyo inaweza kukufanya ubaki hapo hapo. Imani inaweza kukujengea ukuta mkubwa na kuwa mtumwa wayo, lakini upande mwingine imani hiyo inaweza kukufanya uwe huru na kuangaziwa.

Imani iliyochanganyika na u mimi yaani ego mara nyingi inamdidimiza mtu na kumfanya asiweze kuangaziwa. Kama nikivyosema imani ni hisia. Na hisia huongezeka zaidi kadili ya imani inavyokomaa.

Imani itokanayo na Utamaduni au itokanayo na Kusikia ikikomaa hujenga hisia kali sana kiasi cha kuwa tayari kujinyonga kwaajili ya imani. Watu wanajiua kutokana na imani, watu wanafanya matukio ya kuwaumiza wengine kutokana na imani.

Zipo imani za kisiasa, zipo imani za kibiashara, zipo imani za kijeshi, zipo imani za kidini nk. Zote hizi huamsha hisia kali kwa mtu kutokana na kiwango cha imani. Zipo dini zimejengwa katika msingi wa kuwaona wengine hawafai wasipokuwa kwenye dini hiyo, zingine zimejengwa katika misingi ya kuamini mtu, vitu au vitabu.

Imani ni hisia lazima iendane na akili. Akili ni pamoja na kujua watu wanaokuzunguka na wao wanahitaji pumzi kama wewe, nao wanahitaji kula kama wewe, nao walizaliwa na watakufa kama wewe, vyote unavyoviona ni haki yako pekee nao wanahiyo haki kama wewe.

Ndugu zanguni. Nitaongelea kwa kina zaidi suala hili la imani na akili kadili nitakavyopata nafasi.

Mwenye ufahamu ayafahamu haya...
 
Sijaja kibiblia mkuu, huo mstari ni maana ya Imani, ni katika kuthibitisha hoja yangu wala sio katika kuanzisha mabishano.
Tunafundishana sote kwa pamoja. Mwenye hiki anamgawia mwenzake asichokuwa nacho. Na siyo suala la kubishana. Tukifundishana, tufundishane tu si kwa nia mbaya bali kwa nia ya kujengana.

Asante kwa taarifa yako.
 
Hahahaaa nguvu za giza ndo hizo hizo za mwanga maana yake Mungu ana pande mbili upande mwanga na upande giza yaani amekamilika ok sawa
 
Mkuu acha bangi aka kushabu🤣
 
Kwa maneno haya tu itoshe kusema ulikuwa unaongea na mashetani.

"Baba na Mama wakiungana na kufanya kwa pamoja watajenga familia. Mawazo ya Shetani na mawazo ya Mungu yakiungana tutapata amani."

Nataka uelewe kuwa umizimu ujibadilisha kulibgana na kipindi na uelewa wa mtu.
Mwambie kwa Jina la BWANA apotee halafu amini
 
Ni imani yako tu. Kama inakupatia faida ni kheri kwako lakini kama imani yako inajenga chuki kwa wengine jaribu kufanya adjustment ya imani hiyo. Usitumie imani tu aka hisia, hebu jaribu kutumia na akili kisogo.

Jaribu kujiuliza maswali na ujijibu mwenye kabla ya ku implement imani yako.
 
Ninaweza nisipate nafasi ya kukuona face to face mimi nikutahadharishe kwa wema kabisa kuwa makini mashetani hujigeuza kuwa kama malaika wa nuru.
Swali je utajuaje?
Kipimio ni Neno la Mungu
Ikiwa atatamka maneno ambayo ni kinyume na Neno la Mungu lililoandikwa elewa sio. MKATALIE.
Maana hata Yesu alitokewa na kiumbe kama huyo
 
Kwa namna ulivyo taja Yesu. Najua wewe ni mkristo. Hebu nakuomba usome kwenye biblia katika maandiko haya kisha uniletee maana yake:-

"Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli."
Mambo ya Walawi 16:8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…