Mara yangu ya kwanza kukutana na malaika(1987)

Hii ilitokea mara moja kwa mwaka ktk siku ya UPATANISHO.i.e siku ya hukumu
1. Mbuzi wa Bwana alikuwa anauawa kwa ajili ya dhambi za israel yote na damu yake ilikuwa kwa ajili ya kuwatakasa.
2. Mbuzi wa Azazel hakuuawa bali Kuhani aliweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi huyu, akiwa ametokea ktk hema akiwa kwa mfano amebeba dhambi za taifa lote na kuziweka juu ya mbuzi wa Azazel naye halipelekwa nyikani pasipo watu(Alitengwa milele), hii ni mfano wa kutengwa kwa shetani kwa ajili ya dhambi za watu wote.
Asante
 
Unaelewa maana ya Azazel kupewa sadaka ya mbuzi.
Twende taratibu tu:-
Soma sura yote anzia hapa:-
"Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.
1 Mambo ya Nyakati 21:1"

Kisha soma hapa sura yote:-
"Tena hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, akamtia Daudi nia juu yao, akisema, Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda.
2 Samweli 24:1"

Kumbuka hiyo ni stori moja. Upande imeongelea shetani na upande imeongelea YAHWEH kwenye tafsiri ya original Hebrew.

Niletee majibu katika hili asante.
 
Oya hiyo cannabis ulotumia umenunua wapi na bei gani!?

Let's assume ulikua Nabii
 
Mbuzi wa Azazel yuko kwenye ibada siku ya upatanisho tu..
Sasa hayo mafungu wapi ametajwa mbuzi wa Azazel
 
Watu wanatafuta maisha baada ya kifo. Kabla ya kuzaliwa na baada ya kufa, hakuna mtu anayeweza kumweleza mwingine. Maana kabla ya kuzaliwa experience ya maisha ni tofauti na sasa. Kila mmoja yupo na namna yake ya kueleza.

Lakini cha kujiuliza ni nini maana ya maisha!? Kama tunaongelea maisha kabla ya kuzaliwa au baada yakufa, na tunaleta tafsiri ya maisha ni kuvuta pumzi, kula, kuvaa na kustarehe, basi kabla ya kuzaliwa na baada ya kufa hakuna maisha.

Mtu anapozaliwa, anapoanza kupata elimu ya dunia huanza kufanya utafiti wa kujua mambo mbalimbali. Kuna vitu atajaribu kuvifanya, vingine vitamletea matokeo hasi. Je, ni nini maana ya mtoto kutafuta kujua kila kitu!? Ni kwamba anataka kujua experience ya existence yake mpya.

Watu wanauliza na wanatamani kujua baada ya kifo kuna maisha!? Kwa tafsiri ya ulimwengu wa mwili na tamaduni za ulimwengu wa mwili, mtu akifa maisha ndio yameishia hapo. Kumbukumbu ya kila mtu imetunzwa kwenye memory yake. Nasema sasa mtu yupo na aina mbili ya memory:-
Temporary Memory na
Inherited Memory

Hizi zote zipo kwenye mwili.
Sasa basi tunapoishi katika ulimwengu wa mwili ni vyema tukajua hakuna thawabu utakayopewa kokote kwa matendo ya mwili. Maana mshahara wa matendo ya mwili hutimizwa kwa matendo ya mwili. Hakuna kumbukumbu itakayobaki popote na kukufaidisha kutokana na matendo ya mwili. Baada ya kifo kumbukumbu za mambo ya mwili hubaki katika ulimwengu wa mwili.

Hakuna taarifa ya matendo ya mwili itakayokupatia thawabu kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa. Mtu hujishuhudia mwenyewe na kutengeneza ulimwengu wake mwenyewe. Ndipo sasa mwenye ufahamu afahamu haya; mtu anajishuhudia mwenywe, mtu anatengeneza ulimwengu wake mwenyewe, yeye anakuwa mfalme, anakuwa Mungu na anakuwa muumbaji mwenyewe.

Sasa basi kama imani ya mwingine inakuudhi, ni bora ukajitenga naye ukawa mbali naye ili uweze kujifurahisha mwenyewe. Furaha yako hapa duniani unaijenga mwenyewe.

Mwenye ufahamu afahamu hayo....
 
Huyo ni shetani mwenyewe kabisa, jihadhari mapema
Biblia inasema wafu hawajui kitu, na huyo malaika wako anakuambia wafu wana furahia/wanafuraha
Wafu wapo makaburini- hizo habari zingine ni chenga tu

Mhubiri 9:5​

kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.



1 Wathesalonike 4:13-18

Neno: Bibilia Takatifu

Kufufuliwa Kwa Wafu Na Kuja Kwa Bwana​

13 Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. 14 Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake. 15 Kama alivyosema Bwana mwenyewe, tunawaambieni kuwa sisi ambao tuko hai bado, tutakaokuwa hai mpaka Bwana arudi, kwa hakika hatutawatangulia wale waliokwisha kufa.
16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu; na wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu tukutane na Bwana angani. Na hivyo tutakuwa na Bwana milele. 18 Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.
 
Unaisoma biblia yote au unanukuu vifungu tu!?

Nipatie maelezo kuhusu mistari hii

1 Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.
2 Wakorintho 12:1

2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
2 Wakorintho 12:2

3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);
2 Wakorintho 12:3

4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.
2 Wakorintho 12:4
 
Niambie hapa Yesu alikuwa anaongelea nini!?
Soma biblia:-
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
Luka 23:43
 
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
Ufunuo wa Yohana 20:12
 
Upungufu wa akili huja polepile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…