Marangu Coach imefikia hatua hii

Marangu Coach imefikia hatua hii

Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
Kazi ipo
 
Siyo hawaziamini Dar spare bei kubwa Moshi rahisi.

Mfano gear box ya Fuso Dar inafika 5.5mil wakati Moshi hiyo hiyo used kutoka Dubai/Japan inakuwa 3.5 to 4mill so unaweza ukaona namna huo utofauti unavyokuwa mkubwa,japo kulinda brand ilibidi kwa gharama yoyote spea ipatikane abiria waondoke
Asee nilipewa kazi ya kufufua landrover Tdi na tajiri mmoja hivi sasa nilihitaji spare zake nyingi tu nikacheki kwa hapa dar nilipata ila bei yake mpk tajiri akastuka tukapata duka lingine Moshi asee spare bei rahisi sijui kwanini mzee.
 
Chanzo cha hayo yote ni ubahili tu wa Wachagga
Yani wanataka tu pesa iingie siyo kutoka
 
images.jpeg

Hotelini, jengo pembeni ni choo maarufu kwa wasafiri wa Moshi Dar.
 
Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
...Pole. Heri kuchelewa Kuliko Kutofika Kabisa...
 
Mrejesho, baada ya usingizi kukata kumbe basi liliingia Moshi saa 5 usiku! Hivyo basi lilitumia saa 17 toka Dar mpaka Moshi!
This is Marangu Couch, Welcome aboard, usisite kuwasiliana na wahudumu wa basi endapo utakuwa na tatizo isipokuwa la kifedha na kimwili.
Msalimie Jane
 
Sisi hata mume hamshirikishi mkewe, akifariki ghafla mwanamke hajui walichonacho kifamilia.
Kuna mzee mmoja mtu mkubwa tu tena kitengo anawekeza na hamshirikishi mkewe anatushirikisha watu baki. Tulimkazia sana amuonyeshe mkewe. Lakini kuna muda pia labda kuna madhaifu anayo mkewe tusilaumu sana aisee. Japo ni tatizo. Wamama wengine hawanaga adabu. Mume akitangulia anaenda kula mali za mumewe na viben ten mpk anafilisika
 
Acha nongwa mkuu kwani dogo akila bata, akigonga gari si za babake wewe inakuuma nini. Au wewe hukuachiwa kitu. Hahahaa Pole sana pambana wanao waje wayafaidi maisha bladfool
Kheee.. muone huyu nae. Nani anamuonea wivu sasa? Acha umama. Hapa tunajadili uzembe wake. Unategemea aiendeshe kampuni kwa usahihi? Kidogo no ngumu kwake japo anajitahidi. Halafu koma, sina njaa hizo. Na huo ndo ufala wako mmarangu..
 
Kama kumbukumbu yangu iko sawa, hii kampuni ilimpoteza mmiliki na mwenza wake kipindi kile kigumu cha korona.

Kampuni itakuwa mikononi mwa second hand, lazima challenge ziwepo.

Endeleeni kufurahia Marangu Coach.
 
Alikuwa hisa bado
Okey. I real dont know.
Pale Tarakea wanakijiji wengi walikua wamewekeza. Walinunua hisa ila sikuwahi kuhoji waliwekeza wapi. Kwenye ndege ama lah. Ilikua 2018 kama sikosei tukiwa tunafanya kumbukumbu ya marehem mmoja hivi ya miaka 25 toka afariki. Nilisikia mama zetu wanaulizana zile fedha tulizowekeza hivi ziko wapi. Na hapo hawakuwekeza juzi wala jana. Ni miaka mingi kidogo. Najiuliza alidhulumu ama ziko mahali ambapo wao hawajui wahusika? Ijapokua pia sikuona kama walikua wanaziwazia sanaaa. Naona ni kama waliamua kulichukulia kama sadaka wametoa.
 
Mrejesho, baada ya usingizi kukata kumbe basi liliingia Moshi saa 5 usiku! Hivyo basi lilitumia saa 17 toka Dar mpaka Moshi!
This is Marangu Couch, Welcome aboard, usisite kuwasiliana na wahudumu wa basi endapo utakuwa na tatizo isipokuwa la kifedha na kimwili.
Hahahahahaha umeniuaaa. Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom